
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Watu wote mle ndani walikuwa na nakala ya gazeti la Shupavu mkononi, wakisoma habari ile mbaya sana iliyoandikwa na Mwandishi wetu. Wote walikuwa wamejiinamia chini, wamekuwa wadogo mithili ya piriton. Gazeti la Shupavu lilianika kila kitu kuhusu wao na mipango yao.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
"Kuna msaliti kati yetu" Moja wa six killers aliropoka kwa sauti kubwa. Wengine wote walikaa kimya, kama hawakuisikia ile kauli toka kwa Moja. Kilipita kimya cha dakika kama tano, Tano ambaye sasa alikuwa amepata nafuu kile kidonda cha goti alivunja ukimya. "Hakuna msaliti..." "Ilaaa...." Moja alidakia kabla Tano hajamalizia alichotaka kusema. "Mimi nina wasiwasi Sita ametekwa, na ni yeye ndiye aliyetoa siri zetu hizi" Tano aliongea kwa upole. Don Genge alimwangalia Tano kwa jicho Kali huku akitetemeka mikono kwa hasira. "Sasa kama Sita kakamatwa si muda wowote nasi tutakamatwa?" Dokta Sharifa aliuliza huku sauti yake ikionesha woga dhahiri. "Hatuwezi kukamatwa. Hata huyo Sita hapajui mahala hapa kwa usahihi wake, kama usivyopajua wewe, ila tatizo hatutofanya kazi yetu tena, maana pale, hospitalini kutakuwa na ulinzi mkali sana baada ya taarifa hii" Don Genge alifafanua. "Kipo tutakachofanya, jamaa wanataka mioyo ya
maiti kumi na tano kila siku, hawajari maiti ya mtoto mdogo au mkubwa. Itabidi twende mashuleni, tunawateka watoto, tunawauwa na kisha tunawatoa mioyo, zoezi la kutoa mioyo tutalifanyia hapa" Moja hakukubali kushindwa, alitoa wazo ambalo kila mmoja alilikubali kwa kichwa. Don Genge sasa akaelewa, kwanini jamaa amepewa namba moja katika kundi la six killers, alikuwa katili sana. Alikuwa na akili sana. Mpango wa kuwateka watoto wa shule ulibarikiwa na wote. Wakisubiri kesho yake waanze kuufanyia kazi mpango huo mpya. Sasa askari walijigawa kulinda shule zote za mjini Masoko.
Na wazazi wengine waliingiwa na uwoga sana, hawakuruhusu watoto wao waende shule. Kuruhusu mtoto kwenda shule ilikuwa ni sawa na kumpoteza kabisa! Vilio ndani ya Kilwa vilizidi na kupaa zaidi, vikafika hadi nje ya mipaka ya Tanzania. Umoja wa mataifa kupitia shirika lake la watoto wakatoa kauli, na kuitaka Serikali ya Tanzania kuongeza nguvu katika kuwasaka wauaji hao. Marekani nayo ikatoa kauli, na kulaani pia vitendo hivyo vya kinyama. Hadi sasa watu wa Kilwa wakiwa hawajui chanzo cha mambo hayo kutokea. Mji ulipoa, watu wakiishi kwa woga mkuu. Watu wazima waliogopa, watoto wadogo waliogopa! Uwoga ulioathiri hadi shughuli za kiuchumi za Kilwa. Wakubwa waliogopa kwenda makazini, watoto waliogopa kwenda shuleni. Wakati ulinzi ukishamili katika shule zote za Msingi na Sekondari Kilwa.
Polisi wakigeuka walinzi wa shule, kundi la Six Killers walibadirisha aina ya pigo sasa. Walevi saba walitoka majumbani kwao jioni lakini hawakurejea kwao usiku wa manane kama ilivyo ada yao. Walipokuwa wanarejea majumbani kwao usiku baada ya kulewa, njiani walidakwa na Six killers na kupelekwa porini ngome. Six Killers walikuwa wanahitaji mioyo, iwe ya watoto, iwe ya wakubwa, iwe ya walevi ama ya wazima. Kwa bahati mbaya kabisa, miongoni mwa walevi waliokamatwa usiku ule mbaya ni mama Kindumba, rafiki kipenzi wa Mwanasheria mlevi.
*****
Ilikuwa ni wiki kadhaa tangu Mwanasheria mlevi kutoonekana katika kilinge chao cha ulevi. Ilikuwa huzuni kwa walevi wote kutoonekana kwa Mwanasheria mlevi. Huku lawama zote zikiienda kwa jeshi la polisi ambao ndio walimchukua kwa mara ya mwisho. Lakini pamoja na kutoonekana kwa Mwanasheria mlevi, walevi hawakuacha kunywa pombe. Waliendelea kunywa pombe huku wakimlilia Mwanasheria mlevi. Hakuna hata mlevi mmoja aliyewaza kwenda kituo cha polisi kujua hatma ya Mwanasheria mlevi. Wao wenyewe walikuwa wanajihisi wakosefu. Waende kituo cha polisi halafu.... Ndipo ulikuja usiku huu, usiku ambao walevi saba walipotea katika mazingira ya kutatanisha. Ukiwa ni muendelezo wa kupoteza kwa wanafunzi.
Six killers walifanya kazi kwa umakini mkubwa sana, kila Mlevi alikamatwa kwa namna yake. Huku mama Kindumba akiwa mlevi wa mwisho kukamatwa usiku ule. Mama Kindumba alitoka kilabuni saa nane ya usiku. Alikuwa na furaha sana, alikuwa kalewa barabara, akiimba nyimbo yeye mwenyewe na kucheza yeye mwenyewe. Alikuwa anakata mitaa usiku wenye giza nene bila wasiwasi wowote. Watu husema pombe hupunguza uwoga kwa mlevi, inawezekana ikawa kweli maana mama Kindumba hakuwa na uwoga wowote usiku ule. Nyimbo zikizoimbwa kwa sauti ya kilevi na mbwembwe za kilevi zilikoma alipokutana na Bedui, Moja wa Six Killers.
Pombe zote ziliishia hapo, nyimbo ziliishia hapo. Kwanza aliona Kivuli kirefu cheusi, kisha kivuli hiko kilirusha kofi moja la nguvu toka katika mkono ulioshiba wa Kivuli, mkono uliochanganyika na dawa za kulevya ulimlaza Mama Kindumba usingizi nzito. Mama Kindumba alilala katika mtaa wa Kariakoo pale karibu na ukumbi wa Hall fear na kuamka katika pori la Ngome. Na mama Kindumba kukamilisha idadi ya walevi saba waliotekwa siku hiyo. Mpelelezi Daniel Mwaseba ilikuwa ni sawa na askari Polisi wa kituo cha Polisi Masoko. Kila alipojaribu kuweka mtego wake kuwatega wahalifu kundi la Six killers waliutegeua mtego wake.
Wakina Don Genge walikuwa wajanja sana walibadili aina ya watu wanaowateka mara kwa mara. Wakati wanawateka wanafunzi wa shule ya Msingi Masoko, siku ya pili yake Daniel Mwaseba alienda kulinda katika shule ya Msingi Mnazimmoja. Lakini Six killers hawakwenda kuteka tena wanafunzi wa shule ya msingi, walibadili mbinu, walienda kuteka wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilwa. Wakati Daniel Mwaseba alienda kulinda shule ya Sekondari Mtanga, kundi la six Killers walibadili tena mtindo walienda kuwateka walevi. Daniel alikuwa anatabasamu kila tukio linavyotokea, ishara kwamba alikuwa anakasirika sana. Huyo ndiye Daniel Mwaseba hutabasamu kila mambo yanavyokuwa mazito. Kwa upande wa kundi la Six killers kwao ilikuwa ni furaha, vifijo na nderemo. Walikuwa na mateka wengi sana. Sasa walitulia katika kambi yao wakiwa na uhakika wa kupata mioyo kumi tano kwa siku kadhaa.
Walikuwa na mateka wengi sana. Sasa walitulia katika kambi yao wakiwa na uhakika wa kupata mioyo kumi tano kwa siku kadhaa.
Mwezi ukapita, bila tukio lolote lile la kushangaza katika mji wa Kilwa Masoko wala mji wa Kilwa Kivinje. Baadhi ya watu walianza kusahau matukio ya kutisha yaliyotokea mwezi mmoja nyuma. Watu walianza tena kutembea usiku. Baadhi ya askari Polisi pia walisahau kasheshe iliyotokea mwezi mmoja nyuma. Lakini wazazi na ndugu wa watu waliotekwa hawakusahau kabisa, waliomboleza kila siku juu ya upotevu wa ndugu zao. Wao walikuwa na mawazo sawa na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba, ambaye hakuwa amesahau juu ya vifo na upotevu wa watu kiajabu wa raia wema na alikuwa kazini kila jua lililokuwa linachomoza.
Hatimaye Daniel Mwaseba sasa alikusanya taarifa za kutosha juu ya sakata hii, na kuingia kazini rasmi. Jioni moja ilimkuta Daniel Mwaseba katika baa ya Tiga Tisa. Baa ileile iliyokuwa chanzo cha kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa. Pale Tano alipoikosa shabaha yake ambayo ilikuwa ni Mwanasheria mlevi na kumuua Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa. Daniel Mwaseba hakwenda kunywa katika baa ile. Daniel Mwaseba alikuwa kazini. Alikuwa makini kwa kila kilichoendelea pale Tiga Tisa, alijua lazima atapata kitu kitakachompeleka hatua nyingine katika upelelezi wake.
Naam, Daniel Mwaseba alishakusanya taarifa za kutosha. Taarifa ambazo zilizomjurisha kwamba, kwa mara ya mwisho Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa alikuwa katika baa hiyo kabla mauti hayajamfata hadi nyumbani kwake. Bila shaka Israel mtoa roho alitoka naye hapo, hivyo ndivyo Daniel Mwaseba akivyoamini. Hiyo ndio sababu pekee iliyompeleka Daniel Mwaseba katika baa ya Tigatisa. Alikaa kwenye kona moja, iliyokuwa gizani kidogo lakini ilimuwezesha kuona watu wote wanaoingia na kutoka katika baa ile maarufu Kilwa. Saa nne alikaa pale baa ya Tiga Tisa. Hakukuwa na kitu chochote cha kukitilia shaka. Baa ilikuwa na ushwari wake uleule alioukuta tangu alivyoingia. 'Mvumilivu hula mbivu' Saa sita ya usiku katika baa ya Tiga Tisa aliingia mtu mmoja mrefu, mtu ambaye Daniel Mwaseba alimtilia shaka kidogo.
Alikuwa jamaa mmoja mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, alikuwa amevaa vest nyeupe huku chini akiwa amevaa pensi fupi aina ya timberland. Pamoja na ujabari uliokuwa unaonekana katika mwonekano wake lakini alikuwa anachemenea mguu mmoja. Sifa hizo hazikumfanya Daniel Mwaseba astuke sana, mpaka pale Mhudumu wa baa ile alivyomkonyeza Daniel Mwaseba. Daniel alishaenda katika Baa hiyo mida ya jioni na kumhoji Mhudumu wa Baa ile. Mhudumu aliyemthibitishia kuwa anamtambua mtu anayemuhisi kuwa ndiye alimuuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa. Mhudumu alimwambia kuwa alimtilia shaka mtu huyo pindi tu alivyoingia katika Baa ile.
Mhudumu alianza kumpeleleza mtu yule kwa siri. Ingawa Mhudumu hakuwa mtaalamu wa wahalifu, lakini macho ya mtu yule yalimjulisha kwamba yule jamaa alikuwa Mhalifu! Aliyashuhudia macho mabaya ya jamaa yule yakimwangalia Mwanasheria mara kwa mara. Na pindi tu Mwanasheria alivyopanda gari lake na kuondoka, na yule jamaa naye aliondoka. Zilipokuja taarifa kwamba Mwanasheria kauwawa kwa kisu nyumbani kwake, yule Mhudumu alimtilia shaka sana yule mtu aliyemwona akimwangalia Mwanasheria kwa jicho baya. Lakini hakuwa na mtu sahihi wa kumueleza. Upelelezi wa Polisi ulikuwa wa ajabu sana.
Hawakwenda kabisa kupeleleza mahali ambapo Mwanasheria alionekana kwa mara ya mwisho (Tigatisa). Mhudumu yule aliwasubiri askari waje pale angalau awaambie anachokifahamu kuhusu kifo cha Mwanasheria, lakini Polisi hawakwenda. Naye hakuwa na amani ya kwenda kituo cha Polisi kueleza hisia zake, kwanza zilikuwa hisia tu. Mhudumu alikaa na dukuduku moyoni mpaka leo hii jioni alivyokuja askari huyu kijana, Daniel Mwaseba. Baada ya Daniel Mwaseba kumchokonoa Mhudumu yule Mhudumu alimueleza kila kitu Daniel, na kumuhakikishia kuwa anamtambua huyo mtu endapo atatokea tena katika baa ile.
Ingawa Mhudumu alisema huyo mtu hakuja tena katika baa ile tangu usiku wa tukio lile. Daniel Mwaseba hakuwa na wasiwasi, alimwambia Mhudumu kuwa atakuwa anaenda Baa kila siku. Na siku atakayoyokea tu huyo jamaa amkonyeze, kwa bahati nzuri siku ileile Tano alienda TigaTisa, na Daniel Mwaseba ndipo alipokonyezwa na yule Mhudumu. Daniel Mwaseba pale alipokaa alimuona vizuri sana Tano.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi