BALAA (16)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI NA SITA ILIPOISHIA... Na siku atakayoyokea tu huyo jamaa amkonyeze, kwa bahati nzuri siku ileile Tano alienda TigaTisa , na Daniel Mwaseba ndipo alipokonyezwa na yule Mhudumu. Daniel Mwaseba pale alipokaa alimuona vizuri sana Tano. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Bila wasiwasi wowote Tano alichagua meza moja iliyokuwa tupu na kukaa. Yule Mhudumu alienda Kumsikiliza Tano. Kisha alirudi tena kaunta kuchukua alichoagizwa. Daniel Mwaseba alimshuhudia Mhudumu akipeleka bia mbili katika meza ya yule jamaa, kisha akaondoka. Daniel Mwaseba alinyanyuka pale alipokaa na kuifuata ile meza aliyokaa Tano. Ghafla, Tano aliushuhudia ugeni asioujua katika ile meza yake. Tano alimwangalia kwa umakini mkubwa sana yule kijana mgeni aliyeivamia meza yake bila kukaribishwa. Yule kijana nae ( ambaye sisi tunamtambua kama Daniel Mwaseba) alitulia tuli, kama hakuwa amefanya jamb…