BALAA (21)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Hakujua kabisa alikuwa karibu na mtego. Karibu na hatari! Dokta Kilumba alikuwa anawindwa na wawindaji mahiri sana. Kwa bahati nzuri siku hiyo kulikuwa na 'disco' ndani ya ukumbi wa Masoko by night . 'Disco' ambalo lilikuwa na faida kubwa sana kwa Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi . JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Wingi wa vijana wacheza 'disco' waliozagaa pale nje iliwafanya wasionekane na Dokta Zaidi Kilumba. Hadi kibanda cha vocha kinafungwa Dokta Kilumba alikuwa bado anapata ulabu na kina Dokta Yusha wamejificha palepale. Usiku mnene Dokta Kilumba aliinuka pale katika kile kiti chake alichokalia. Alipepesuka kidogo kutokana na pombe, kisha akakaa sawa. Akapiga hatua za taratibu kutoka katika uwanja wa baa ile. Alifanya yote hayo huku akitazamwa kwa umakini na macho manne. Mhudumu wa baa ya Masoko by nig…