BALAA (26)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA ILIPOISHIA... Kufanikiwa huko kwa Inspekta Jasmine kulifanya azidi kutegemewa na nchi, kutegemewa na jeshi la Polisi. Inspekta Jasmine alitegemewa pia na raia wema. Baada ya wiki kadhaa za kuwatafuta wahalifu pamoja na watu na wanafunzi waliopotea katika mazingira ya kutatanisha kugonga mwamba. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Inspekta Jasmine ndiye aliyepewa jukumu na Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania ili kwenda Kilwa kupeleleza juu ya upotevu wa watu hao. Inspekta Jasmine sasa alikuwa na siku ya pili ndani ya Kilwa lakini upelelezi wake ulikuwa haujamfikisha kabisa karibu na adui. Ilikuwa siku ya tatu sasa tangu inspekta Jasmine Wahabu awasili Kilwa ili kwenda kutatua utata juu ya kupotea kimaajabu kwa watu ndani ya Kilwa, tena katika hali isiyoeleweka hadi sasa. Siku hiyo ya tatu asubuhi na mapema Inspekta Jasmine ilimkuta akiwa amela…