HATI FEKI (3)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Aminata alitaka kujaribu bahati yake kwa kumuuliza mengi kuhusiana na kundi lao. Kwa kipindi kifupi cha kujuana na Dula aliweza kuonana na wengi katika kikundi hicho akiwemo Mosses ambaye baada ya Dula kumtambulisha alionekana kumtamani sana Aminata. “Unakaribisha sana shemeji. Wakati wowote.” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alisema Mosses kisha kutoka baada ya kumsalimia Aminata. Aminata alimwangalia sana. Mosses alikuwa ni mrefu mweupe. Sura yake ilikuwa ikifanana na chotara wa Kiarabu. Ni Mnyamwezi wa Tabora lakini maisha yake alikulia Arusha . Alifanikiwa kusoma hadi kidato cha sita. Ni biashara za magendo ndizo zilizomfanya Mosses asiendelee na chuo kwa ni alifaulu vizuri lakini pesa ilimfanya asitamani tena kusoma. Na huo ndio ukawa mwisho wa kurejea yaliyo vitabuni. Alianzisha kampuni ya magendo ambayo haikusajiliwa ya kununua mag…