
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Walitumia dakika ishirini tu kufika Njiro nyumbani kwa kina John. Walikuta watu watatu wakiwa wamesimama nje ya geti. Mlinzi aliwafungulia na kuingia. John alikuwa bado hajawatambua hadi alipofikia geti kabisa. Mlinzi alifungua geti kubwa na kuliruhusu gari la John kuingia.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
John sasa alimtambua mmoja kati ya wale wageni.
"Namkumbuka mmoja tu, aliyevaa kapelo. Sijui wanataka nini.” John alishuka kwenye gari na kumfungulia Aminata mlango, alimkaribisha kisha kuwafuata wale wachimbaji.
"Mbago bila shaka," John aliuliza.
"Ndiyo mkuu, ni mimi, habari za siku nyingi bosi?" Antony naye alikuwa akitoka nje baada ya kusikia gari likiingia na watu wakiongea. Alisimama mlangoni. Aminata alimwangalia sana kisha kumgeukia John. Hakuona tofauti kati yao. Walikuwa wamefanana sana.
"Salama tu, habari za Mererani bwana Mbago." Aliwasalimia na wachimbaji wengine walioongozana na Mbago.
"Kule hali siyo nzuri kabisa bosi."
"Kwa nini sio nzuri?” Alihoji John.
"Hatuelewi hatma yetu kwani mgodi umeuzwa bila ya kupewa taarifa. Ndio tumechukua uamuzi wa kuja kujua moja ikiwamo kuhoji imekuaje kimyakimya." Alielezea Mbago kwa masikitiko huku wenzake wakiitikia kwa kichwa kuashiria anachosema ni kweli.
"Mgodi umeuzwa?” John na Antony kwa pamoja walitahamaki. Haraka Antony aliingia ndani na kutoka na hati ya umiliki wa mgodi inayoonyesha mmiliki halali wa mgodi ni baba yao Amigolasi.
John aliangaliana na Aminata kwa muda. Hakujua amwambie nini hadi pale Antony alipotoka nje na karatasi iliyoonyesha hati ya umiliki wa mgodi.
"Haiwezekani, hati hii hapa,” Antony aliwaonyesha. “Hii si ndo hati ya mzee? John embu itazame mwenyewe. Ni nani huyo anayeleta mchezo?” Antony alimkabidhi ile hati John ambaye aliiangalia kisha nay eye kumpa Aminata aiangalie.
"Nani kaja kuwapa hizo taarifa? Alihoji John huku akimwangalia Aminata kana kwamba Aminata alijua kinachoendelea. Aminata alikuwa kimya akisikiliza malalamiko na utetezi wa pande zote mbili. Wachimbaji na mabosi wao. Mbago aliwaelezea namna ilivyokuwa hadi wakaamua kuwafukuza kwa mawe na kisha kuitisha kikao cha kujadili safari ya kuja kuonana na wao.
"Mmefanya vizuri sana. nashukuru sana kwa hizo taarifa. Kuna watu wanataka kutudhulumu haki yetu. Labda sio mimi.” John alisema kwa ukweli huku akimrudishia Antony ile hati ili aipeleke ndani.
“Tutalishughulikia hilo, ila waambie wenzako kwamba mgodi haujauzwa, kazi ipo na mambo yakitulia m’taendelea kama kawaida." Antony alihitimisha ili kuwaruhusu Mbago na wenzake wawawahi kuwajulisha wenzao.
"Tunashukuru sana bosi. Siye tunaenda. Mbaki salama." Mbago na wenzake waliondoka baada ya kupata jibu. Hawakujua kwamba wamewaachia John na Antony kazi kubwa sana. John alionekana kuchanganyikiwa.
****
Ni aminata peke yake ndiye aliyeweza kumliwaza John. Aliamua kuwa naye karibu zaidi ili aweze kumtoa katika hali ile. Si kwa hilo tu bali pia Aminata alikuwa anaonyesha kila dalili za kumpenda John kimapenzi. Ni kwa kipindi kirefu sana amekuwa kattika hali hiyo ya upweke kwa ajili ya kazi.
Aminata alikuwa ameshapajua nyumbani kwa kina John na hivyo alifika mara kwa mara ili kuendeleza mipango yao.
Aminata alipata nafasi ya kuongea usiku huo. Hakwenda nyumbani kwake bali aliamua kulala nyumbani kwa kina John kwa ajili ya kuongea mengi. Aminata alimsimulia John yote yaliyomtokea hadi akaamua kuwa mpelelezi.
“Niliamua nikajiapiza kwamba sitawasamehe nan i lazima niwakamate na niwaangamize mimi mwenyewe. Baada ya kukufatilia na kujua wewe ni mtoto wa mzee Amigolas, na bada ya kuona pigo nililolipata mimi na wewe umelipata pamoja na pacha wako. Na pia John wewe unaonekana si lele mama. Wewe na Pacha mnaonekana mmeshiba sana. ni watu wenye nguvu za kupambana. Hivyo kwa mafunzo niliyoyapata tukichanganya na ninavyowaona nyie. Tutawamaliza hata kama wako wengi vipi.” Aminata alimwambia John huku akicheka kwa lengo la kumshawishi wawe pamoja.
John alisimama. Alijiona kama mshindi na asiyeogopa hatari yoyote. Alikumbuka wazazi wake na ndugu zake walivyouliwa. Aliwakumbuka Mbago pamoja na wenzake waliokuja siku chache zilizopita kuwaeleza juu ya migodi. Yeye kama mwanamume iweje akae nyuma wakati Aminata amejitoa kupambana dhidi ya dhulma.
“Tuko pamoja Aminata lazima tuwaangamize. Kesho asubuhi nitaongea na Antony tujue tunaanza lini kazi. Hata kama wameshajimilikisha mgodi lazima tuurudishe. Hizo ni dhuluma. Hatuwezi kuziacha zikatufilisi sisi. Walishachukua roho za ndugu zangu. Sasa wachukue na yakwangu nay a Antony kama wanaweza.” John alisema kwa hasira kali.
Aminata alimfuata na kumshika kisha kumkalisha juu ya kitanda. Pamoja na baridi kali ya mjini Arusha, John alitokwa na jasho kali. Joto lilisababishwa na hasira. Hapo Aminata alimwelewa John kwamba yu tayari kwa mapambano.
“John,” aliita Aminata.... “Wewe ni mwanamume unayeonekana shupavu. Ni mwanamume unayeweza kupambana na pia unamvutia sana mwanamke. Mvuto wako siwezi kuuvumilia pamoja na kwamba unayo hasira. Leo nipo kwako. Sitalala peke angu. Najua Antony ameshalala. Niazime mwili wako kwa usiku huu wa hii baridi,” Aminata alishindwa kuvumilia kila alipomwangalia John ambaye alikuwa amevua shati na kubakiwa na kaushi iliyombana vizuri na kufanya misuli yake itoke nje.
Aminata alipata nafasi ya kuushika mwili wa John kila alipokuwa akimbembeleza. Hapo alijihisi kumvamia John japokuwa alikuwa na hasira. Alijaribu umtuliza mpaka alipoweza kumwambia alichokitaka.
John aliyasikia aliyoyasemaAminata. Hakuonyeshwa kushangaa kusikia maneno yale. Hakuwa na kufanya zaidi ya kunyinyakulia ushindi murua wa mezani baada ya mpinzani wake kuweka mikono chini kuashiria hawezi kushindana.
Ukawa ni mgeuzano wa kila aina katika mbao za futi sita kila upande. Godoro la kisasa zaidi ya lilivyotumika kabla lilionja joto ya migusano na vilio vya mahaba kutoka kwa ofisa mpelelezi Aminata.
Tukio liliendelea tena na tena. Ukawa ni usiku wa bashasha uliolakiwa vizuri na miili iliyokuwa tayari kujifunga na kuwa pamoja. John alisahau hasira zake na kudhulumiwa kwa mgodi. Aminata naye akasahau kazi yake ya ofisa upelelezi. Mtifuano mkali ulimalizika pakiwa panaelekea kupambazuka. Wote walifurahia mchezo huo
Asubuhi John alimfata Antony. Alimwelza juu ya kila alichoambiwa na Aminata. Antony hakuwa na pingamizi kwani alijua hakuna njia nyingine endapo wahusika walishajimilikisha mgodi. Hivyo alijiunga nao ili kuhakikisha wanafanikiwa.
John alimwita Aminata na kumweleza juu ya Antony kukubali. Aminata alifurahi sana. alimwangalia Antony vizuri kwa lengo la kuwatofautisha pindi watakapokutana. Antony ambaye ndiye aliyekuwa mdogo, alikuwa mweupe kidogo kuliko John. Pia Antony alikuwa ni mpole kwa zaidi ya John.
“Mmefanana sana nyie watu. Antony ni mweupe hapo ndo sitawachangamya.” Antony aliangaliana na John kisha wakacheka.
“Acha utania wako Aminata,” John alisema huku akimshika mkono Aminata na kumtambulisha vizuri Antony.
“Huyu anaitwa Aminata. Ni shemeji yako.”
“Nilishaelewa mapema, nilikuwa nasubiri tu nisikie kauli yako. Hongera kaka.”
“Asante.” Hapohapo Aminata nay eye akaongea kuwaambia John na Antony juu ya mpango wake.
“Nataka kwanza mjue kitu gani tutaanza nacho. Kazi ni kubwa sana kuliko huku kutambulishana. Inahitajika mfanye mazoezi hasa ya kulenga shabaha. John we ulikutwa na bastola lakini sidhani kama unajua kuitumia vizuri.”
“Najua sana, sema nakusikiliza.”
“Mmmh. Na mbona wale majambazi walikimbia hukuitumia wakati yule mfanyabiashara alivyovamiwa benki? Au hukujua kama uko nayo?” John na Antony walicheka sana kisha wakasema kwa pamoja.
“Basi tufundishe ofisa.”
Zoezi likaanza mara moja. Aminata aliwapeleka sehemu maalumu wa ajili ya kuwafundisha nyumbani kwake Sakina.
Jambo la kwanza alilofanya Aminata ni kuwafundisha mbinu mbalimbali za kutumia. Aliwafundisha kutumia silaha kwa kulenga shabaha pamoja na namna ya kuwa makini wakati unapokabiliana na adui yako anayekuhisi unamchunguza. Baada ya muda wote walijua.
AMINATA ANAFANIKIWA KUWASHAWISHI JOHN NA ANTONY KUJIUNGA NAYE KWA AJILI YA KUANGAMIZA KUNDI LA MOSSES NDULA. ANAWAPA MAFUNZO AMBAYO ALISHAYAPATA AKIWA KATIKA MAFUNZO YA JESHI.
USIKU wa saa sita. Mosses ndula aliwaita watu wake wote kwa ajili ya kikao cha ghafla. Kikao ambacho ilikuwa ni lazima awahusishe wote. Hakumwacha hata dereva ambaye kazi yake ilikuwa ni kupewa amri ya nenda huku, simama hapo nisubiri au kamchukue Fulani. Wote walikuwepo usiku huo.
Akiwa na sura yenye furaha ya ushindi mkubwa mwezi mmoja baada ya kumaliza kushughulikia hati yake ya umiliki wa mgodi. Sasa alitaka kuwaeleza jambo watu wake.
Alihisi kuna jambo la kuimarisha katika himaya yake ambayo sasa aliona inaimarika baada ya kumpindua mmiliki mkuu wa mgodi, mzee Amigolas na kuumiliki.
“Nadhani imebaki kuanza kazi tu,” alisema Mosses Ndula akiwa na furaha baada ya kuwa amefanikisha kuipata hati ya umiliki ya mgodi. Alikuwa ameinyanyua juu huku akimwonyesha mmojammoja hati hiyo kumaanisha kwamba sasa kila kitu kilikwenda vizuri.
“Mkuu, mi naona bado hatujafanikisha.” Alisema mmoja wa watu wake aliyekuwa amesimama pamoja na Mbashala aliyeitwa Nova, dereva wake wazamani.
“Nisisikie tena….Wewe unasema kama nani? Minasema na wewe unasema?” Mosses Ndula alitoa bastola yake na kumpiga risasi ya kichwa na kufariki papo hapo. Hakutaka kusikia pingamizi lolote kutoka kwa mtu yeyote.
“Sipingwi wala kushushwa, kila nikifanyacho ni zaidi ya mfikiriavyo…. Toa hiyo takataka hapo,” alifoka huku wasaidizi wake pamoja na walinzi wakiwa wanarudi nyuma kwa woga. Wawili kati yao waliutoa mwili wa Nova na kuupeleka kusikojulikana na kuutupa. Kikao kilikuwa kikiendelea ambapo tayari wote walikuwa wakisikiliza tu. Hakuna aliyejaribu kunyanyua mdomo wake kuongea kitu baada ya dakika chache zilizopita kushuhudia mwenzao akitolewa uhai. Wote walisimama kimya wakisubiri Mosses atakachokisema.
Mosses Ndula hakutaka kubadili uamuzi wake juu ya kuachia mgodi. Kufanikiwa kwake kumsainisha kwa lazima Mzee Amigolas ilikuwa ni faraja kwake na kujiona tajiri mkubwa. Alihonga sana polisi na kuweza kujilimbukizia mali nyingi kwa muda mfupi. Alijuana na viongozi wengi na hata baadhi ya kesi zake zilizimwa kimya kimya kwani waliamini yeye ndo angeweza kuwafanikishia biashara zao haramu.
Alipata kujiamini sana. Ni suala moja tu ambalo aliliwaza sana.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi