HATI FEKI (6)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
John na Aminata waliamua kuendelea kuwafatilia wale watu wa Mosses.

“John, tuwawahi kabla hawajatuwahi, kwa sasa hawajui tulipo. Tumeanza na hao watatu. Tuhakikishe tunawamaliza wote,” Aminata alisema baada ya kuona mambo yamekwisha tulia.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
“Itabidi tusilale kwenye hii nyumba Aminata wala kwako tusiende, huenda wameshajua niko na wewe,” John alimsihi Aminata wasiendelee kuishi hapo badala yake wahamie hata hotelini ili wafanikishe kwanza mipango yao kisha watarudi.

Walifunga nyumba na kisha kuondoka jioni na kwenda hotelini kuishi huko, waliamua wawe wanabadili hoteli mara kwa mara ili wasijulikane wako hoteli gani. Huko walikua wakifika usiku tu.

Mchana kutwa walishinda barabarani wakiangalia baadhi ya watu wa Mosses ili kuwamaliza. Waliangalia pia njia ambayo wataitumia kuvamia ngome yao iliyokuwa kambi ya Fisi.

Antony,” Aminata alisema baada ya kumkumbuka Antony.

“Amekuwa kimya sana huko Nairobi,” alisem John.

Anarudi lini sasa?”

“Alisema anarudi kesho. Nadhani tumtaarifu juu ya wapi tulipo ili asije akaenda Njiro.“

“Kweli John,” John alitoa simu yake na kumpigia Antony.

“Nadhani kila kitu kina kwenda swa. Mi nakuja kesho.”

“Sawa lakini usifike nyumbani, ukishuka uwanja wa ndege nitakujulisha wapi utufuate.”

“Sawa kaka, nitakufahamisha nikifika.”

Antony alikuwa ndo anajitayarisha kwa ajili ya safari ya kurudi Tanzania.

*****

Mambo mawili kwa wakati mmoja. Huku mapambano huku mapenzi. Vyote vilimtawala Aminata. Hakuweza kutul;ia tu juu ya mwili wa John. Safari hii alivuka mipaka iliyomfanya John astaajabu. Hakuwa na la kujibu wala kuongea pale alipomwona Aminata akichojua nguo moja baada ya nyingine na kubakiwa na nguo za ndani. Mawazo ya kupambana aliyokuwa nayo yalikatika na kujikuta akimvamia Aminata kama vile Aminata alivyokuwa tayari kumpokea.

Safari hii walifikia katika hoteli ya 7’7 iliyoko katikati ya mji wa Arusha. Walijivinjari taratibu kwa kipindi hicho amabacho walikuwa wakijiandaa kwenda kuendeleza tena mapambano.

Mikono yao haikutulia katika kushambuliana wenyewe pale katika mbao za futi sita kila upande. Ofisa alizidisha utundu wake na kuhakikisha mtuhumiwa wake katika penzi hashindi kesi.

Alimpagawisha John kwa kila aina ya vimbwenga ili mradi aiweke safi nafsi yake na kukata kiu aliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.

Mpaka asubuhi ambapo walipata wazo. Wazo la kwenda Mererani. Hiyo ni baada ya kuwakosa pale Kambi ya Fisi na baada ya kujulishwa na Mbago ya kwamba mgodi ulikuwa ameshaanza kufanya kazi chini ya usimamizi wa mmiliki mwingine aitwaye Mosses ndula.

Jambo hilo liliwashangaza sana na hivyo John aliona pasipokuchelewa ni bora wawafuate kulekule kwani endapo wangewashirikisha polisi hakuna ambacho kingefanyika. Walijiamini kwa kuwa hati miliki ya ukweli wanayo wao na kujua ya kwamba lazima ile aliyomiliki nayo Mosses Ndula ni feki.

****

Ilipita wiki moja pasipo kufanya chochote. John na Aminata walikuwa bado wakiendelea kukaa hotelini. Huko walikula raha zote wakisubiri mambo yatulie ili Mosses Ndula asijue kama kuna mpango wa kufanya uvamizi. Pia Antony alichelewa kurudi na hivyo walikuwa wakimsubiri arudi ndipo waende pamoja.

Ni baada ya kufahamishwa na Mbago ndipo walipoaamua kuwafata huko huko waliko na hivyo ilibidi zoezi la kufanya uvamizi kusimama baada ya kuwakosa eneo la Kambi ya fisi ambapo Mosses Ndula na genge lake walikimbia na kutelekeza kambi yao.

Baada ya kuzipata habari zile, John na Aminata waliondoka baada ya siku mbili. Waliamua kutangulia na kumwacha Antony. John alimweleza Aminata ya kwamba wangefika kwanza kisha wampigie simu na wamwelekeze ni wapi walipo.

Alfajiri ya saa kumi na moja John na Aminata walikuwa njiani kuelekea Mji mdogo wa Mererani. Walitaka kwanza kujua hali ya mgodi. Walikwenda taratibu pasipo kuwa na haraka. Walifika ni kuchukua chumba katika moja ya nyumba za kulala wageni iliyokuwa maarufu na iliyotumiwa zaidi na wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakifika Mererani kwa ajili ya kununua madini au hata kukagua migodi yao.

Ni usiku huohuo ambapo Aminata alijihisi mabadiliko. Mabadiliko ya kimwili na hivyo alijua bado yupo kazini na asingeweza kumwambia John kwani hajui ambalo angeamua na kushindwa kuendelea na kazi. Siku hiyo Aminata aliimwonyesha John hisia zake zote na kuficha hali yake hata pale alipohisi kichefuchefu.

Mara kwa mara alimtoroka John ili asimgundue. Alirudi na kuendelea na raha zao na mipango yao ya uvamizi. Alihakkisha John hahisi jambo lolote kwake.

Asubuhi waliamua kutoka kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa eneo zima la mgodi. John alikuwa amesahau sehemu nyingi na hivyo aliishia kuangaza tu macho. Waliamua kwenda moja kwa moja wakifuata njia ambayo aliikumbuka.

Walifika na kushangaa mabadiliko makubwa ikiwemo kuzungushiwa kwa uzio mzito wa umeme ili kudhibiti watu kuingia. Ndiyo hukuhuku Mosses Ndula na genge lake waliweka makazi yao. Walijenga nyumba ndogondogo kwa ajili ya kambi yao. Uzio huo ulilindwa na walinzi waliokuwa wakisimama imara mlangoni na wengine walikuwa juu ya vibanda maalumu vya kuangalizia wezi na watu wanaokuja na kuondoka. John na Aminata waliwafuata baadhi ya wakazi wa huko na kuulizia kinachoendelea.

“Samahani sana ndugu, habari yako,” walimsalimia mkazi mmoja aliyekuwa akizungukazunguka maeneo hayo.

“Nzuri tu,” aliitikia salamu yule kijana.

“Siye hatufahamu nani ameingia hapa maana hata sisi tuna hofu kubwa ingawa hawajawahi kutudhuru wala kutufanyia fujo. Hata mkuu wao anaonekana ni mtu mwema sana,” alikuwa ni mmoja wa wakazi wa mji huo ambaye alielezea ujio wa Mosses Ndula na kikosi chake ambao waliweka kambi hapo bila ya kuwadhuru wakazi wa eneo hilo.

“Umeshazunguka na kuona mwisho wa uzio huu uliozungushiwa?” Aminata alimuuliza yule mkazi.

“Njooni niwapeleke,” yule mkazi aliwachukua na kuwazungusha kila kona ili wauone uzio huo ulikopita na ulikoishia.

Aliwaeleza ni namna gani wanapalinda pale na mtu yeyote akitaka kuingia lazima akaguliwe na kwamba unalindwa na askari wanaojiamini sana.

Ilikuwa saa tatu asubuhi…pilikapilika katika eneo lile hazikuwepo kama awali. Ulinzi ulifanya watu kulikimbia lle eneo kwani lililindwa sana. baadhi ya viongozi wa serikalini walifika pale wakiongozana na Mosses Ndula.

Viongozi hao ni wale waliojihusisha naye katika biashara za dawa za kulevya kabla hajaacha na kuamua kufanya umafia na kumiliki mgodi.

Walifanikiwa kusimama katika moja ya nyumba ambazo zilikuwa karibu na uzio ule na uanza kuangalia ukubwa wa uzio. John alikuwa amemwona moja ya walinzi wakija. Aliwashtua Aminata na yule kijana nay eye kuzunguka kwa nyuma.

Yule askari alifika na kuwaweka Aminata na yule kijana chini ya ulinzi lakini kabla hawajatii amri ile John alikuwa ameshafika na kumpiga kabala moja iliyomfanya ashindwe kujigeuza. Haraka Aminata alimnyang’anya silaha yake na kumficha kule ndani yule askari.

Walimhoji juu ya Mosses na kuhusu mgodi. Yule askari alilazimishwa hadi akasema. Aminata alichukua kiwambo cha bastola yake na kukifunga kisha alimpiga risasi yule askari wa kuhofia akipata nafasi ataenda kuwaelezea wakuu wake.

Waliamua kuondoka katika ile nyumba na kwenda pamoja na yule kijana hadi hotele waliyokuwa wakikaa. Walipanga waende tena jioni ili wapaone kwani kwenye giza wasingeweza kuonekana vizuri. Yule kijana alikuwa bado hajawaelewa John na Aminata pamoja na kwmba liongozana nao. Jua lilizama na wote waliamua kwenda tena.

Ilikuwa ni saa mbili na nusu jioni. John, Aminata pamoja na yule kijana walianza kuzunguka uzio ule. Hakuna aliyemweleza yule kijana zaidi ya kumwomba tu waonyeshe kama alivyowaambia. Walikuwa bado wakizunguka ule uzio. Wao walichotaka kujua ni jinsi gani watakuja kuwavamia.

Waliangaza kila walipopitishwa ili wajue wataingiaje. Hakuna aliyewaona kwani giza lilikuwa limekuwa kali kiasi katika eneo hilo. Yule mkazi aliwashangaa ni kwa nini wanapafatilia kiasi hicho wakati hawataweza kuingia kwani ni hatari.

“Kwani kuna nini kati yenu na hawa jamaa?” alihoji yule mkazi.

“Sikiliza….. hiyo siyo kazi yako…tunachotaka ni kuujua huu mgodi uzio wake unaishia wapi,” John alidakia kwa kumtaka yule mkazi asiingilie lakini ghafla Aminata aliingilia.

“Hapana John, huyu jamaa anatusaidia. Inapasa tumweleze kwani bila yeye tusingeweza kufika hapa.”

“Okey… ni kwamba huu mgodi ni mali yetu na hati tunayo….kwanza jina lako nani?” John alikatisha aliyokuwa akiyaelezea kuhusu mgodi na kutaka kujua jina la yule mkazi.

“Mi naitwa, Francis. Ni mkazi wa huku na kuna kipindi nilishawahi kufanya kazi katika huu mgodi. Nakumbuka kipindi hicho ulikuwa ukimilikiwa na mzee mmoja ‘bonge’ hivi alikuwa akiitwa Amigolas. Yule mzee ndiye aliyetuajiri sisi na kipindi hicho ndiyo huu mgodi ulikuwa ukianza kukua kwani kabla ulikuwa hautambuliwi.

Nasikia kwa sasa ni marehemu na kabla ya kifo chake aliamua kuuuza huu mgodi, alikuja akatutoa wachimbaji wote na kuamua kuajiri wachimbaji aliyewataka yeye na nadhani huyu jamaa ndiye aliyeununua. Inaonekana pia ni mtu mkubwa sana.

“Hapana,” John alimkatisha…. “Huu mgodi haujauzwa. Mzee unayemsema ni baba yangu. Hakuuza mgodi huu ila umechukuliwa kwa nguvu na ndiyo chanzo cha kifo cha mzee wangu. Hivyo nataka kuurudisha huu mgodi kwani hata hati halali ninayo na hati wanayoitumia ni feki.

Hapa tulipo tunataka tuwaangamize wote na kumaliza huu mtandao wao. Kama utaona hatari usijihusishe maana hapa haponi mtu.” John aliongea kwa hasira akimtaka Francis azingatie aliyosikia na awe tayari kwa lolote kama alivyoona kwa yule askari ambaye walimuua jana yake.

Ghafla simu ya John iliita. Ilikuwa ni simu ya Antony. John aliwahi kuizima mlio ili wasije wakasikiwa. Aliipokea na kumtaarifu Antony kwamba atampigia baada ya dakika tano.

Baada ya dakika tano, John, Aminata pamoja na Francis walikuwa wameshafika hotelini. John alimpigia simu Antony na kuongea naye.

“Vipi kaka, uko poa?”

“Niko poa kaka, mko wapi?

“Tuko Mererani. uje maana mgodi umeshavamiwa. Jamaa ameuchukua kweli. Njoo tuanze kazi mkuu.”

“Dah, haiwezekani. Nakuja.”

Antony alichukua gari yake na kuanza safari ya kuelekea Mererani kuungana na John na Aminata. Alijipanga vizuri kuhakikisha kweli anakwenda kwa kazi moja tu, kukomboa mali za baba yao.

*****

USALAMA katika ngome ya Mosses uliwatisha kidogo kina John. Walifika na gari karibu na uzio wa mgodi ule na kuangalia kwa mbali kidogo shughuli zilizokuw zikiendelea kule ndani.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni