HATI FEKI (8)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Hawakuona lolote zaidi ya miili ya askari wenzao.

Ghafla John aliwatokea na kuwamiminia risasi ambazo ziliwashtua Mosses na wenzake.

“Wafuateni,” alifoka Mosses akiwaamuru askari waliobaki wawafuate wenzao.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Huko yaliwakuta yaliyowakuta wenzao. Yeye pamoja na walinzi wenzake wligeuza gari na kuanza kuondoka.

Antony alikutana na Mbago pamoja na wachimbaji wengine. Walivamia migodini na kuwatoa watu wote na kuhakikisha hakuna askari yeyote wa Mosses aliyesalia. Antonuy alitaka kuwajulisha juu ya kilichokuwa kikiendelea. Usiku huohuo ambapo hali ya mji wa Mererani haukuwa tena shwari ilisikika tu milio ya risasi.

Msafara ulivurugika. hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Mashambulizi sasa yalihamia barabarani. Mosses na watu wake waligeuza na kuanza kukimbia wakielekea mjini. John na Aminata waliwaona na hivyo hawakuwaachia.

“Wanaondoka. Tusiwaache,” John alisema huku akilikimbilia moja ya magari yaliyokuwa yamebaki. Alifyetua risasi iliyompata dereva na kumlenga ya kichwani. Aminata naye alifyatua na kuwalenga walinzi wengine wa Mosses. Hapo sasa wakawa wamepata gari. Mosses na mbashala pamoja na walinzi wawili na dereva walikuwa wakikimbia sasa. Waliwaacha umbali mdogo na hivyo walijua si rahisi wawafikie.

Hakuna aliyejua aliyeamua kuvamia na kufanya mashambulizi katika mgodi wako. Mosses alikuwa amechanganyikiwa kwani hakuwa na taarifa ya kuwapo kwa John na Antony, mpacha wa mzee Amigolas.

“Tembea na spidi zote,” alifoka kwa nguvu kumkaripia dereva aongeze kasi. Alizidi kuwaza.

Mbashala…. Nani wale? Unawajua?” alimuuliza Mbashala ambaye na yeye hakufahamu lolote.

“Au ni serikali wamewatuma majasusi wao kufanya huu unyama. Nitaongea na kiongozi.”

“Kiongozi gani?”

“Mkuu wangu.. Haiwezekani hili. Mambo yanaharibika sasa…. Sijui ni kina nani hawa wanaharibu mipango yangu,” alisema Mosses ambaye alionekana kukasirika.

John na Aminata walizidi kuwakaribia kwani Mosses alijua hakuna aliyekuwa akiwafuata nyuma. Dakika tano baadaye mlio wa risasi iliyofyetuliwa na Aminata ulilenga gari na kuwashtua kina Mosses.

“Endesha, tuko kwenye hatari,” alifoka Mosses akimwamuru dereva wake. Dereva alipatwa na woga. Alitamani aruke aache gari lenyewe kwa kuhofia maisha yake. Alijua hila zote za Mosses zimefika mwisho na huo pia unaweza ukawa mwisho wake.

Hakuwa na la kufanya. Kuona vile dereva alizidi kukimbiza gari. Alitafuta njia ambazo zilikuwa na kona nyingi ili kuwapoteza lakini hawakuwaacha mbali.

Yule dereva aliogopa sana kwani Mosses alikuwa ameshikilia bastola yake na hivyo hakuweza kusimamisha gari ili kukimbia.

Tayari walikuwa wameshaingia barabara kuu ya Moshi Arusha.

*****

Antony alifanikiwa kuipata ile hati ambayo alikuwa nayo Mosses Ndula. Alikuwa ameihifadhi ndani ya sanduku kulekule mgodini katika ofisi yake ambapo walifanya upekuzi pamoja na wale wachimbaji. Aliichukua kama ushahidi baada ya kupata taarifa juu ya kukamatwa kwake. Antony aliwaeleza wale wachimbaji kila kitu. Aliwataka sasa watulie.

“Polisi walipata taarifa juu ya tukio hilo. Walituma baadhi ya askari kwenda kwa ajili ya kuangalia na kusaidia kule mgodini. Polisi walikuwa tayari wamefika katika mgodi huo na kuwaweka chini ya ulinzi wachimbaji wote pamoja na Antony.

Polisi wengine walikuwa wakiwafuata John na Aminata waliokuwa wakiwakimbiza Mosses na watu wake.

“Wekeni silaha zenu chini,” polisi mmoja alitoa amri. Antony aliwasihi wachimbaji waliokuwa na silaha waweke silaha chini na kuwasikiliza wale polisi.

Mosses na watu wake walikuwa wakielekea eneo la Maji ya Chai. John na Aminata hawakuwa mbali nao. John alijitahidi sana kuwafikia. Walianza kuwarushia risasi ambapo na wao walikuwa wakizijibu kwa nyuma. Mosses alijua mambo yameshaharibika na hivyo aliamuru gari lisimamishwe ili waweze kuwashambulia kwa risasi na kuwamaliza kina John.

Haikuwa rahisi kwani wakati wanarushiana risasi Aminata alifanikiwa kuwaua walinzi wawili. Alikuwa ni mlinzi pamoja na msaidizi wa Mosses ‘Mbashala’ na kufanya wabakie watatu. Dereva alikuwa tayari amekimbia na kuwaacha Mosses na walinzi wake wawili wakiendelea kurushiana Risasi.

Polisi walifanikiwa kufika eneo la Maji ya chai na kukuta bado mapambano yakiendelea. Walisimama na kutoka nje ya magari yao na kuanza kuwafyetulia risasi kina Mosses ambao nao walijibu mapigo.

“Acheni,’ Mosses aliwaamuru watu wake kuacha kushambulia kwani aliona ameshazidiwa na hivyo wangeuliwa. Hakuonekana mwenye kukata tama. Alijua atashinda huko mbele. Aliamua kuwazuia wenzake ambao mmoja wao alikuwa akivuja damu baada ya risasi ya John kumpata ya begani.

Mosses Ndula na wenzake hawakuwa na ujanja tena zaidi ya kutii na kuweka silaha chini na kunyanyua mikono juu. John na Aminata walianza kusogea kuwafuata polisi waliko ili waweze kujitambulisha.

“Heshima yako mkuu,” Polisi mmoja aliyekuwa amewafuata Aminata na John alitoa saluti kwa Aminata. Aminata alikuwa bado amewaelekezea Mosses na watu wake bastola hadi walipoweka silaha chini baada ya kugeuka na kuwaona polisi nao wakiwa wamewaelekezea mitutu ya bunduki na hivyo wasiweze kukimbia. Polisi waliwashangaa Mosses na watu wake wawili.

“Huyu jamaa aliwahi kuja pale kituoni na wanasheria wake,” polisi mmoja alisema huku akistaajabu kulikoni mtu mkubwa vile akimbizwe na gari kama mhalifu.

“Nyamaza… kila kitu kitajulikana huko huko. Waliwachukua Mosses Ndula pamoja na wenzake hadi Kituo cha Polisi. Mosses hakuonekana kutishika wala kujali. Dereva alikimbilia porini na hivyo hakuweza kutafutwa wala kujulikana.

Aminata alimfuata kiongozi wa wale polisi na kumsihi wasikubali akatoroka hadi pale watakapofika mjini Arusha kesho yake.

“Sawa mkuu,” tutawafikisha wote kama amri yako ilivyosema.”

KINA JOHN WANAFANIKIWA KUUVAMIA MGODI. WANASHAMBULUIA NA KUUA ASKARI WOTE.

MOSSES ANAFANIKIWA KUKIMBIA PAMOJA NA WATU WAKE LAKINI NAYE ANATIWA NGUVUNI NA POLISI BAADA YA KUFUKUZWA NA JOHN NA AMINATA.

SAFARI YA KUMPELEKA KITUONI MJINI ARUSHA NDIYO INAYOFUATIA.

MOSSES Ndula na wenzake hawakuwa na ujanja tena zaidi ya kutii na kuweka silaha chini na kunyanyua mikono juu. John na Aminata walianza kusogea kuwafuata polisi waliko ili waweze kujitambulisha.

“Heshima yako mkuu,” Polisi mmoja aliyekuwa amewafuata Aminata na John alitoa saluti kwa Aminata. Aminata alikuwa bado amewaelekezea Mosses na watu wake bastola hadi walipoweka silaha chini baada ya kugeuka na kuwaona polisi nao wakiwa wamewaelekezea mitutu ya bunduki na hivyo wasiweze kukimbia. Polisi waliwashangaa Mosses na watu wake wawili.
“Huyu jamaa aliwahi kuja pale kituoni na wanasheria wake,” polisi mmoja alisema huku akistaajabu kulikoni mtu mkubwa vile akimbizwe na gari kama mhalifu.

“Nyamaza… kila kitu kitajulikana huko huko. Waliwachukua Mosses Ndula pamoja na wenzake hadi Kituo cha Polisi. Mosses hakuonekana kutishika wala kujali. Dereva alikimbilia porini na hivyo hakuweza kutafutwa wala kujulikana.

Aminata alimfuata kiongozi wa wale polisi na kumsihi wasikubali akatoroka hadi pale watakapofika mjini Arusha kesho yake.

“Sawa mkuu,” tutawafikisha wote kama amri yako ilivyosema.”

****

Msafara wa kuwapeleka mahabusu Mosses na mlinzi wake ulianza. John na Aminata wao waliamua kurudi. Walielekea Mererani na moja ya magari ya polisi kwani gari lao lilikuwa limepasuliwa tairi wakati wa mashambulizi ya kurushiana risasi wao na Mosses. Waliingia siti ya nyuma wakiendeshwa na mmoja wa polisi waliokuwa wamefika pale.

“Ninafururaha sana tumekamilisha hii safari yetu ya muda mrefu. Sikutegemea kusambaratisha jeshi zima japo sio kubwa na. kilichobaki sasa ni kujua kama Antony ameshafanikisha kuuzuia mgodi kule Mererani.” Aminata alisema wakati wakiwa njiani kuelekea Mererani kuangalia kilichoendelea usiku huohuo.

John alitoa simu yake kwa nia ya kumpigia Antony.

Lakini kabla hajabonyeza namba alisikia ikiita simu yake.

“Antony anapiga. Utafkiri alijua nataka kumpigia.”

“Akili zenu sawa, kweli nyie pacha,” John alicheka huku akipokea simu yake.

“Haloo kaka,” alisema John akiitikia simu ya upande wa pili alipokuwa Antony.

“Shwari tu kaka. Nawasikilizia nyie. Mnaendeleaje huko?”

“Tumeshawatia nguvuni wawili japo mmoja kakimbia. Nadhani ni dereva wake. Ila mhusika mkuu tayari tunaye.”

“Kwa nini msingemuua broo?”

Polisi waliwahi kumchukua. Hata hivyo hawezi kuleta madhara. Kesho asubuhi tutaenda kwa ajili ya kuanza kumfungulia kesi.”

“Sawa, sasa wapi mnaelekea sasa hivi?”

“Tunakuja huko kuangalia usalama.”

“Huku tumeshikiliwa na polisi. Nadhani Aminata akija itakuwa safi.”

“Usijali. Tunakuja na gari la polisi. Nadhani kila kitu kitakuwa poa. Baadaye kaka.”

“Poa Broo.”

John na Antony walimaliza maongezi yao. Sasa John alimgeukia Aminata ambaye alikuwa amejiegemeza kwenye bega la John na kulala. Alimbusu kwenye paji la uso. Busu lile lilimshtua Aminata na kujikuta akimuuliza John.

“Vipi, kina Antony wako poa huko?”

“Ndiyo mpenzi, wanakusubiri wewe ukawanasue maana wako chini ya ulinzi wote. Wamekalishwa chini. Nadhani linasubiriwa karandinga kuwapeleka kituoni.”

“Haiwezekani bana,” Aminata alisema huku nay eye akitoa simu yake na kupiga makao makuu kwa ajili ya kutoa taarifa za kuwekwa chini ya ulinzi huku akiwataka wasiwaondoe watu hao hadi atakapofika eneo la tukio.

“Tayari mpenzi. Nimeshawaambia wasiwapeleke kokote hadi nifike.”

“Asante mpenzi,” John alimshukuru Aminata huku akimvuta na kunanza kumbusu.

*****

Wakiwa njiani kuelekea Arusha Mjini kuwapeleka Mosses na mlinzi wake Mahabusu. Polisi hawakujua kwamba Mosses alikuwa na bastola.

“Samahani mkuu,” kabla sijapatwa na hili janga nililtokea katika starehe zangu. Nahisi kwenda haja ndogo. Tafadhalin,” alisema Mosses huku akiwa amefungwa pingu. Ndani ya koti lake kulikuwa na bastola.

“Hakuna, mpaka tufike,” Polisi mmoja alisema kwa ukali.

“Hapana, kwa kuwa tumemfunga. Tumwache ajisaidie,” polisi mmoja aliyekuwa akiendesha gari alisema huku akiegesha gari pembeni ili Mosses ajisaidie.

“Nshukuru sana,” Mosses alisema huku akitoka nje ya gari.

Ni katika maeneo ya Tengeru ambapo Mosses anafanikiwa kuwatoroka polisi baada ya kuitoa bastola yake ndogo na kuwapiga nayo.

Alitokomea kusikojulikana pamoja na yule mlinzi wake ambaye muda wote alikuwa amechoka baada ya damu nyingi kumtoka baada ya kupigwa risasi ya begani.

Kuona vile, Mosses aliamua kumpiga tena risasi na kumuua kwani aliona atasababisha wakamatwe.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni