JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (7)

Zephiline F Ezekiel
Mtunzi: 2jiachie

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Mama Anna alijilaza kuangalia miguuni kwa Roi mpaka Roi akashangaa. Alishangaa kwa sababu alihisi mwanamke huyo hakuwa tayari kwa mchezo zaidi ya kupandishana joto la mahaba tu.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Kumbe sivyo, mama Anna alikuwa kwenye pozi lile ili aanze kucheza mchezo kwa mashambulizi ya kuanzia katikati.

Roi alishangaa, mama Anna anamsogelea upandeupande huku akimshikashika sehemu mbalimbali za mwili mpaka wakawa sanjari.

Roi kuja kushtukia, mama Anna ameshaanza mchezo kwa kujihudumia mwenyewe. Roi naye akaunga mchezoni, wakaanza kusakata kabumbu huku mama Anna akiimba mashairi mazuri ya mahaba.

Roi alichanganyikiwa, akatamani kulia kwani kuna ufundi alikuwa akifanyiwa na mama Anna ulimzuzua akili. Mama Anna sijui alifanyaje, Roi akahisi anaondoka kwenye ulimwengu huu na kwenda sehemu nyingine…

“Noo…noo Martha noo. Hebu tuongee kwanza please,” alisema Roi kwa kupiga ukelele kidogo. Mama Anna akatuliza mpira katikati ya uwanja…

“Niambie baba,” alisema…

“Martha,” aliita Roi…

“Sema baba nakusikiliza wewe.”

Roi hakuwahi kuitwa baba na Martha wake hata siku moja. Kuitwa na Martha huyu mwizi kwake pia ilikuwa ni jambo jipya…

“Huna mwanaume mwingine?” aliuliza Roi…

“Aaah! Sina mbona. Mimi niponipo tu,” alisema mama Anna huku akianzisha mchezo polepole kama anayesema kumbe unachotaka kusema ni hicho tu…

“Ngoja Martha…ngoja…”Mama Anna akatuliza mpira tena lakini si kwa kusimama moja kwa moja, kwa mbali alicheza…

“Nakusikiliza dada’angu. Liseme hilo unalotaka kulisema.”

Mama Anna alisogea tena, akanyoosha mikono yake yote na kushika mikono ya Roi…

“Ni hivi…” alikohoa kwanza…

SASA JIACHIE MWENYEWE…

Roi alishtuka kidogo kule kushikwa mikono na mwanamke. Na kama mwanaume alihisi joto la mapenzi likimpanda. Akamtumbulia macho huku akihema kwa mbali…

“Unajua wewe ni mwanaume, tena mzuri na unayevutia, si ndiyo?” alisema mama Anna…

“Pengine wewe ndiyo unaniona hivyo dada.”

“Ni kweli. Hivi, yule Martha kweli ni dada yako kama anavyoendelea kututambulisha kila siku?”

Lilikuwa swali lenye mtego mkubwa kwa Roi. Moyoni aliona nusunusu, akisema siyo hajui nini kingetokea akisema ndiyo pia hakujua nini kingetokea. Akaamua kusema siyo ili kama mama Anna ana jambo la siri anataka kumwambia, amwambie.

“Siyo dada yangu.”

“Ni nani wako?”

Roi aliamini kwa jibu lake kila kitu kiko wazi, lakini kwa vile aliulizwa alijibu…

“Ni mchumba wangu.”

“Ok. Ndiye utakayemuoa?”

“Ndiyo maana yake.”

“Ok. Mnaendana lakini. Hata mimi naunga mkono wewe kumuoa wajina wangu Martha,” alisema mama Anna mpaka Roi akashangaa, moyoni akajiuliza…

“Ina maana hili ndilo alilotaka kuniambia mpaka akawa anakaa vizuri? Siyo hili, huyu ana lake jambo.”

“Kumbe na wewe unaitwa Martha?” aliuliza Roi.

“Ndiyo. Mama Anna, ni kwa sababu ya mtoto wangu tu. Naye yuko kwa baba yake, tulitengana kama mwaka wa nne sasa.”

“Ooh! Sawa.”

Mama Anna akamwangalia Roi kwa macho ya wizi, Roi naye alimwangalia kwa macho ya waziwazi…

“Una lingine dada’angu?”

Mama Anna alimwangalia Roi kwa muda kisha akatoa sauti ya chini sana…

“Lingine mi nakupenda.”

“Oo! Asante sana kwa kunipenda,” alisema Roi huku akimwangalia mama Anna kwa macho ya ujasiri.

Mama Anna alipeleka tena mikono yake kwenye mikono ya Roi na kuishika, akaanza kuiminyaminya kimahaba.

Roi akawa mtu wa kujishtukia tu, ulaini wa mikono ya mama Anna ulimuweka katika wakati mgumu, akahisi akianza kutokwa na kijasho chembamba.

Kwa mtu yeyote aliyewaona alijua wawili hao ni wapenzi kwa jinsi walivyokaa karibu.

“Dada Martha,” aliita Roi.

“Abe.”

“Tubaki kuwa dada na kaka.”

“Ni kweli. Lakini mi nakupenda sana.”

“Ndiyo hivyo, tayari ninaye Martha mwenzako. Akijua je?”

“Atajuaje? Au utamwambia jamaniiii?”

“Hapana! Si unajua dunia haina siri! Hata ukifanyia kitu chumbani, tena ukiwa peke yako, watu watajua tu, sembuse sisi dada!”

“Kwani unataka kuniambia sisi ni utu uzima wetu tunaweza kufanya mambo mpaka yakawa hadharani?” aliuliza mama Anna huku akizidi kuviminyaminya vidole vya Roi. Sasa akawa anakikuna kiganja cha mkono wa kulia, Roi akasisimka…

“Hu…we…zi ku…ju…a,” alisema Roi kwa kukatakata maneno yake.

Roi tayari alishapandisha joto la mwili. Kwa ni kusema ukweli, mama Anna naye alijaliwa. Kila sehemu ya mwili wake ilikuwa ina sifa, sijui wakati wa usichana wake alikuaje kama akiwa mama wa mtoto mmoja tu ndiyo hivyo.

Alijua vyema kuyatumia macho yake. Alipomwangalia mwanaume yalionekana kama ya mtu aliyekuwa akitaka kusinzia ‘flani hivi.

“Hawezi bwana. Mimi nitajitahidi kufanya siri ya hali ya juu. Sitamwambia hata mtu mmoja. We niamini mimi.”

Hivi kweli hawezi kujua? Kila ninapomfikiria, namuona kuwa mwanamke mjanjamjanja, naogopa sana,” alisema Roi, japokuwa naye alikuwa amekwishaanza kuzama katika lindi la tamaa ya mapenzi, lakini akajifanya kukaza.

“Haki ya Mungu hatojua, niamini jamani, kweli hatojua,” alisema mama Anna.

“Mh! Ma…Martha…”

“Abee.”

“Uta…weza?”

“Kufanyaje?”

“Ku…fi…cha si…ri?”

“Mi ni msiri sana usinione hivi,” alisema mama Anna huku akizidi kumkuna kiganjani Roi ambaye sasa damu zilikwenda kwa kasi.

Roi kama mwanaume rijali hakuona sababu ya kulaza damu kwa mwanamke huyo ambaye alijilengesha mwenyewe…

“Afadhali ningemtongoza, sasa mwenyewe tu anajileta halafu nimwachie, nitakuwa si mwanaume,” alisema moyoni huku sasa na yeye akianza kumshikashika mama Anna.

Ilipita kama dakika tatu hakuna aliyekuwa akizungumza zaidi ya kuendelea kushikana kiaina. Kilichosikika ni kuhema kwa mama Anna ambaye sasa alionekana kama tayari amechaji.

Roi alimsimamisha, akamshika mkono na kuondoka naye…

“Tunakwenda wapi sasa?” aliuliza mama Anna.

“Wewe twende tu, wala usiogope,” alisema Roi, tayari akili yake ilikwishahama kabisa, kwa kumwangalia tu, ingekufanya ujue tayari penzi lilimchukua.

Roi alichanganyikiwa, akatamani kulia kwani kuna ufundi alikuwa akifanyiwa na mama Anna ulimzuzua akili. Mama Anna sijui alifanyaje, Roi akahisi anaondoka kwenye ulimwengu huu na kwenda seyemu nyingine…

“Noo…noo Martha noo. Hebu tuongee kwanza please,” alisema Roi kwa kupiga ukelele kidogo. Mama Anna akatuliza mpira katikati ya uwanja…

JIACHIE KIVYAKO…

“Niambie baba,” alisema Martha…

“Martha,” aliita Roi…

“Sema baba nakusikiliza wewe.”

Roi hakuwahi kuitwa baba na Martha wake hata siku moja. Kuitwa na Martha huyu mwizi kwake pia ilikuwa ni jambo jipya…

“Huna mwanaume mwingine?” aliuliza Roi kwa sauti iliyojaa umakini wa hali ya juu…

“Aaah! Sina mbona. Mimi niponipo tu,” alisema mama Anna huku akianzisha mchezo polepole kama anayesema kumbe unachotaka kusema ni hicho tu…

“Ngoja Martha…ngoja…”

Mama Anna akatuliza mpira tena lakini si kwa kusimama moja kwa moja, kwa mbali alicheza…

“Mimi nataka nikuoe wewe Martha…please nikubalie mama.”

Hapo ndipo alipokuwa akipataka mama Anna, kumzidi nguvu wajina wake Martha kama alivyowaambia wapangaji wenzake.

“Mh! Itawezekana kweli? Nahisi itakuwa ngumu baba angu,” alisema mama Anna kwa gia ya kutotaka kuonekana mrahisi…

“Tatizo litakuwa wapi kwani?”

“Si kwa Martha! Si umesema ndiyo unataka ufunge naye ndoa?”

“Nimabadili mawazo Martha, amini hivyo.”

Martha aliendelea kukataa lakini huku akiendelea na mchezo kwa staili ya kushambulia polepole, Roi akajishindwa na kutangaza kuvunja dafu lake huku akikaribishwa.

Huku akijua Roi ameshavunja dafu, mama Anna alibadili upande bila kusubiri mapumziko, sasa Roi akawa anashambulia kutoka upande mwingine ambao awali alikuwa akizuia asifungwe.

Hilo lilimfanya Roi kupata joto tena na hivyo kumudu mchezo kiasi kwamba alijihisi kama hakuvunja dafu tangu aanze. Mama Anna alipotangaza kuvunja dafu yeye, alitumia ufundi wa hali ya juu ikiwemo kuchezesha sauti yake kwa mahaba mazito na kumbembeleza Roi ambapo sekunde kadhaa mbele akavunja dafu.

Wote walikuwa wakihema kwa kasi kutokana na mechi kuwa ya vuta nikuvute mpaka dakika za mwisho ambapo matokeo yalikuwa moja kwa moja.

“Da! Martha, sijategemea ujue,” alisema Roi akiwa anajipindua pale kitandani…

“Hukutegemea nini?”

“Kama upo hivyo.”

“Kwani nipoje?”

“Da! We mwenyewe unajijua,” alisema Roi kisha akambusu mama Anna ambaye naye alitoa sauti ya hisia ya mapenzi.

***

Ilikuwa saa kumi na mbili na nusu, wawili hao walishacheza mzunguko wa pili na kutoka sare ya moja kwa moja kama ilivyokuwa kwenye mzunguko wa kwanza.

“Sasa itakuaje?” aliuliza Roi…

“Kuhusu?”

“Si tunaondoka?”

“Kurudi kule?”

“Yes.”

“Sawa.”

Walitoka kitandani wote, wakaenda kuoga wote, wakavaa, wakatoka wote. Roi aliendesha gari lakini kutokana na foleni, walifika kwa Martha saa moja na nusu usiku.

Bila woga, Roi alifika na mama Anna akiwa ndani ya gari mpaka nje. Wakatulia kwanza kuangalia hali ya hewa, kisha mama Anna akashuka baada ya kujiridhisha kwamba hakukuwa na mashuhuda maeneo yale.

Alianza kuingia ndani mama Anna, Roi akibaki ndani ya gari. Akapitiliza hadi kwenye chumba cha shoga yake mmoja, anaitwa Madam May ambako pia alimkuta shoga mwingine, mama Eli

“Tayari,” alisema mama Anna…

“Acha uongo wako bwana,” walisema wenzake…

“Ohoo! Naapa, tayari. Nimekuja naye mpaka hapo nje, nyie subirini mtasikia akiingia…

“Mlikuwa hotelini?” mama Eli aliuliza kwa sauti ya umbeya…

“Kwake.”

“Mm! Huo sasa uongo uliopitiliza,” alisema Madam May.

“Ngoja nimtumie ujumbe halafu ajibu, ndiyo mtaamini,” alisema mama Anna huku akiandika ujumbe wa simu…

“Baby, nimefurahi sana kwa mechi ya leo. Halafu mechi ya kuichezea nyumbani kwako kama vile ni nzuri kuliko gesti au hotelini. Nimeipenda sana.”

Baada ya kuandika ujumbe huo, mama Anna aliwaonesha wenzake kisha akautuma kwenda kwenye namba ya Roi ambayo aliisevu kwenye simu yake kwa jina la ‘Wa Martha.’

Ni ndani ya dakika tatu tu, meseji ikajibiwa…

“Mimi pia nimeinjoi sana baby. Da! Yaani wewe ni kiboko, umeniteka kabisa Martha. Kesho twende tena nyumbani kwangu kama leo.”

Mama Anna alipoisoma meseji hiyo akawaonesha wenzake, wakacheka mpaka kupiga mikono ‘pa…pa’…

“Mimi nawaambieni, lazima wajina wangu aachike hivihivi anaona. Nimempa biti yule kaka ambazo mwenyewe hajawahi kupewa tangu azaliwe.”

Baada ya mazungumzo yao, Martha aliingia ndani kwake na kuwaacha wenzake wakiendelea na mazungumzo.

***

Roi alikaribishwa chumbani kwa Martha kwa mabusu mfululizo huku akipewa pole kwa kazi za mchana kutwa halafu akaambiwa…

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni