MWAJUMA UTAMU (1)
Jina: MWAJUMA UTAMU Mtunzi: Juma Hiza SEHEMU YA KWANZA Nakumbuka ulikuwa ni mwaka 2010, nilipata bahati ya kufanya kazi za ndani katika nyumba moja iliyokuwepo maeneo ya Kijitonyama . Ilikuwa ni familia ya Mzee Gidion pamoja na mke wake ambapo katika maisha yao walifanikiwa kupata watoto wawili, mtoto wa kwanza alikuwa ni wa kiume aliyejulikana kwa jina la Daniel na mwingine wa mwisho alikuwa ni wa kike aliyejulikana kwa jina la Naomi. Mzee Gidion alikuwa akimiliki kampuni moja hapa mjini iliyomuingizia kiasi kikubwa cha pesa, aliishi maisha mazuri yeye pamoja na familia yake. Baada ya kupita miezi mitatu tangu nilipoanza kufanya kazi za ndani katika nyumba hiyo Mzee Gidion alianza kunitamani, alichokuwa akikihitaji ni penzi langu tu, aliahidi kunifanyia mambo mengi sana katika maisha yangu endapo kama ningekubali ombi lake la kulala naye kitanda kimoja. Kiukweli lilikuwa ni jambo gumu mno hasa ukizingatia mke wake ndiye aliyenileta katika nyumba hiyo kwa lengo la kufanya kazi, sikuwa tayari…