MWAJUMA UTAMU (4)
Jina: MWAJUMA UTAMU Mtunzi: Juma Hiza SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Kwa kuwa nilikuwa tayari kufanya lolote Savela alinishauri niende hospitali nikautoe ujauzito niliyokuwa nao kwa madai kuwa ingeniharibia soko la biashara yangu ya uchangudoa. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mipango ikaandaliwa kisha nikaenda kwenye hospitali moja ya kibinafsi maarufu sana hapa mjini, sitaweza kuitaja kwasababu za kibiashara. Nilifanikiwa kuutoa ujauzito wa miezi mitatu, hilo lilimfurahisha Savela mno, aliniambia huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kutengeneza pesa na kuwa mwenye mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye. Kichwa changu kilikuwa kikifikiria utajiri ambao ningeweza kuupata kutokana na biashara hiyo ya uchangudoa. Hakukuwa kuna kitu nilichokuwa nikikitamani kama kuwa na maisha mazuri. Niliutamani sana utajiri, nilipokuwa nikimsikia mtu akipiga stori za pesa nilihisi kusisimka mwili. Ki…