HATI FEKI (10)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Hawakuweza hata kujiokoa kwani jeshi la Mosses Ndula lilionekana kuwa imara. Alitakiwa kusema ukweli juu ya jambo ambalo Serikali inataka kujua kwani inaonekana kama alitumwa na chombo hicho kikuu cha dola.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Mosses alijua John na Aminata watakuwa wanatumiwa. Alifahamu sana mambo ya baba yake, Mzee Amigolas ambaye alikuwa yupo karibu sana na viongozi wakubwa wa nchi. Amigolas alijihusisha upande mwingine na serikali. Alisaidia viongozi kila mara wakati wa kampeni.

Hakutaka wajue kwamba alikuwa anafanya hila za kuwateka na kuwaua kama alivyodhamiria hivyo aliwauliza maswali ili ajue endapo wangekufa asingeweza kutafutwa na polizi zaidi kwani ni miezi michache imepita baada ya kufanikiwa kumaliza tofauti zake na polisi ambao walikuwa wanamtafuta na kusaidiwa kwa kivuli cha Steve ambaye sasa ndiye bosi wake.

“Tatizo lako John hutaki kuongea ukweli, usipoangalia nitakuangamiza mshenzi mkubwa wewe.” Mosses Ndula alimfokea John. Mlinitafuta mkanipata. Sasa nimewapata mimi. Mi ndio Mosses,” Mosses alisema huku akicheka sana na kumtandika kibao kikali John huku akiendelea kucheka zaidi.

John alijikuta akisukumiwa ngumi mbili nzito huku ikishuhudiwa na Steve, Bosi huyo mkuu anayemiliki kampuni ya uchimbaji madini huko Mererani. Aliyekuwa mpinzani mkubwa wa mzee Amigolas.

Aliongoza genge la wahuni waliotaka kuipindua Serikali ya nchi kwa kuwa alikuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.

Alifanya kila njama kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Serikali ili kufanikisha azma yao. Habari zilienea na kuwapa hofu watu kwamba jeshi la nchi linataka kuipindua Serikali. Habari zilivuma kwamba majeshi ya Serikali ndiyo yaliyotaka kuipindua nchi. Nchi haikukalika hadi pale kiongozi mkuu alipotoa tamko kwamba hakuna habari kama hizo. Nchi ilitulia tena kama kawaida. Vyombo vya habari vilitakiwa kutangaza amani kama ilivyokuwepo awali.

Ndiye huyo Steve. Hela haimpigi chenga. Tajiri wa kutupwa aliyeweza kununua hata robo tatu ya nchi. Ana uwezo wa kununua chochote atakacho. Aliyemchukua Mosses Ndula na kumweka sawa. Akampa uwezo wa kuamua atakalo kwa masilahi yake na genge hilo ambalo Mosses ndiye aliyelitengeneza na kuunda jeshi. Sasa anafanya kisasi kwa Aminata na John.

Ililazimika kwa Serikali kufanya kazi ya ziada ya kuweza kuwabaini wahusika wa mauaji yaliyosababishwa na genge la Mosses ambaye alifanya mauaji mengi kwa kutumia kivuli cha Steve na yeye mwenyewe kwa upande mwingine kwa kuwa aliweza kuwa karibu na viongozi wengi hasa waziri wa Ulinzi Steve na Mosses waliweza kuziteka hisia za viongozi wengi na pale walivyotoa wazo kila kiongozi waliyekutana naye alikubaliana nao. Hakuna kiongozi aliyeweza kufika katika ngome ya Steve.

*****

Max mmoja wa askari wa upelelezi aliyefanya kazi yake imara. Aliaminiwa sana na serikali na hasa katika matukio aambayo yangehitaji ujasiri mkubwa na mbinu nyingi za kikomando. Aliyafahamu mafunzo imara aliyoyapata katika kambi mbalimbali ambazo amekuwa akizipitia ili kujiimarisha mwenyewe.

Baada ya kumaliza mafunzo yake nchini Urusi na kurejea nchini, Max alikutana kwa mara nyingine na Aminata. Mwanafunzi mwenzake waliyekuwa wakisoma pamoja katika mafunzo ya askari upelelezi na baada ya hapo Max alichaguliwa kujiunga na kambi ya kijeshi na kufuzu mpaka alipochaguliwa tena akapate mafunzo zaidi nchini Urusi.

Alipewa jukumu la kufuatilia nyendo za watu mbalimbali wanaoshukiwa ili kujua ukweli wa vikosi hivyo vilivyofanya shambulio la kushtukiza. Shambulio lililosababisha na baruti kulipuliwa katika mgodi wa Amigolas. Ilisemekana ni watu wa Steve wakiongozwa na Mosses ndio waliosababisha mlipuko huo wakati wa usiku baadhi ya wachimbaji wakiwa chini ya ardhi wakitafuta Tanzanite.

Max alitii amri hiyo na kuahidi kuanza kazi hiyo haraka iwezekanavyo. Baada ya mienzi kadhaa ya kufanya uchunguzi wao Mosses Ndula na Bosi Steve walikuwa tayari wamepata taarifa kutoka kwa baadhi ya makachero wao waliowatega karibu na Serikali ili kujua ni nini kinachoendelea na jinsi ya kuendelea kujiimarisha, pia waliwaweka ili kuhakikisha wanachunguza ni kwa kiasi gani Serikali inajua kuhusiana na genge lao. Kwa uwezo aliokuwa nao Steve, aliongeza ukubwa wa genge lake. Sasa alitawala sehemu kubwa ya watu.

Wachimbaji wengi walikufa na wengine kujeruhiwa huku mgodi wa mzee Amigolas ukitishiwa kufungiwa. Hata ilipojulikana kwamba ni Steve ndiye aliyeamuru yafanyike mauaji hayo hakuweza kuchukuliwa hatua na hivyo kesi yake kuzimwa na kuonekana ilikuwa ni bahati mbaya kutokana na kushindwa kulipua vizuri baruti katika mgodi.

*****

“Huwezi kutusumbua wewe mtu mmoja na huyu mke wako leo lazima mtakufa,” Mosses Ndulah alifoka kwa hasira huku amemsogezea John mdomo wa Bastola aliyokuwa ameishika. Kutokana na ngumi mzito aliyopewa na Mosses Ndulah, John damu zilitapakaa usoni. John alikuwa aimwangalia Aminata ambaye alikuwa hajitambui kwani Steve aliyekuwa sambamba kusikiliza kauli za Mosses Ndula alimchapa Aminata kwa kutumia kitako cha Bastola yake na kuzirai.

Vikosi vya Mosses Ndula vilikuwa vimetapakaa kila mahali kuzunguka jengo kubwa la gharama lililotumiwa na Mosses Ndula katika kuimarisha ngome ya Bosi Steve. Jengo la Bosi Steve lililoko Mererani, hakuna aliyejua ndani ya jengo hili kulikuwa kuna nini kwani hata barabara iliyoelekea katika jingo hilo haikuonekana, lilizingirwa na msitu mkali lenyewe likiwa katikati ya msitu huo mkubwa.

Si rahisi kuona barabara inakoingia mpaka kwenye jengo hilo kubwa hivyo wapitanjia wa kawaida hawakuwa na urahisi wa kuingia ndani ya jengo hilo japo kwa mbali waliweza kuliona. Wengi walidhani kwamba lilikuwa halikaliwi na mtu. Wengine walijua linakaliwa na majini kama imani zao zilivyowatuma.

Hata walinzi hawakuweza kuonekana kwa urahisi kwani hawakuwa wakitoka mara kwa mara hasa wakati wa mchana. Wengine walijua ni sehemu ya ajabu kwani wengi walioingia huko hawakurudi waliuliwa ili kuzuia siri kufichuka.

John na Aminata pia hawakujua wako wapi kwani waliingizwa ndani ya jengo hilo walikuwa wakiwa wamezirai kutokana na kipigo kikali kutoka kwa Mosses Ndula na vikosi vyake.

Jioni ya saa mbili na nusu walikuwa ndani ya Land Cruser V8 kabla ya kutekwa John na Aminata, walikuwa wakielekea nyumbani kwa Aminata kwa ajili ya mapumziko kwani ilikuwa ni majira ya jioni. Aminata ndiye aliyetoa wazo kwa John kwamba waende kupumzika.

John alikubali na kuondoka. Walikuwa wakijiburudisha jioni. Hawakuwa na mengi ya kufanya zaidi ya kuwa pamoja.

Baada ya kujifungua mtoto wao Amigolas, sasa waliishi kwa furaha huku wakiamini kwamba mambo yametulia. Mtoto wao alipelekwa shule za bweni ili kumwezesha asome zaidi. Ni miaka mitano baada ya kuzaliwa na kuifanya familia ya John kuwa na furaha baada ya kumpata Amigolas mpya.

Sasa waliishi maisha ya wawili. Walifanya hivyo ili kumwepusha mtoto wao na balaa linaloweza kuwatokea kwani Aminata alikumbuka siku aliyomwona Mosses dirishani na kushtuka. Aqalimsihi sana John wampeleke Amigolas shule za bweni ili asije akapatwa na madhara kwani aliamini bado hawajamalizana na Mosses Ndula.

Wakiwa wanapita barabara iliyotokea Hospitali ya Mount Meru, Aminata alitazama kwenye kioo cha gari na kuona msururu wa magari ukiwafuta huku yote yakiwa yamewasha taa kuashiria jambo fulani.

“John embu geuka nyuma ujionee hayo magari, sijui yanaelekea wapi,” John aligeuka na kujionea, alihisi jambo hivyo akamwambia Aminata aingilie barabara inayoelekea Kijenge kisha aongeze mwendo. Aminata alimshangaa John kwa maneno aliyoyatoa na kukemea kwa hasira.

“Kwani umeambiwa wanatufuata sisi?” John alizidi kumsihi afanye hivyo. Aminata alibaki akimwangalia John ambaye hakuwa hata na wasiwasi huku yeye akiendesha gari kama alivyoelezwa. Wakiwa makutano na Barabara ya Kijenge karibu walikuwa tayari wamezingirwa baada ya gari nyingine kutokea upande wa chini wa barabara ya Uhuru.

Aminata alifunga breki kwa nguvu zote kutokana na gari kuwa katika mwendo wa kasi. Gari zilizokuwa zinakuja mbele yao nazo zilisimama na kisha watu takribani saba waliteremka kuwafuata. John na Aminata hawakuwa na silaha ya aina yeyote hivyo wakajikuta wakiishia katika mikono ya vikosi vya Mosses Ndula.

“Aminata kwani kuna nini?” Aminata hakujibu kitu bali alikaza macho ili kuwatambua watu waliokuja mbele yao kama aliwajua. Alimwona Mosses na watu wake wakija.

“Ni Mosses.”

“What?” John alihamaki baada ya kumwona Mosses akiwafuata huku ameshikilia bastola akifuatana na watu wengine waliokuwa wameshikilia silaha nzito.

“John tutafanyaje hapa na hatuna hata silaha?” Aminata alisema huku akimwangalia Mosses bila kuamini macho yake kwamba amerudi tena na bado anaendelea na ukatili wake. John kabla ya kumjibu Aminata. Mosses Ndula ndiye aliyekuwa wa kwanza kushika kitasa cha gari la kina John na kumchomoa John kwa nguvu. Alimtupia John ngumi nzito na kuzirai. Bosi Steve alimchapa Aminata kwa kitako cha bunduki na kuzirai.

Waliwachukua wote mpaka katika jengo lao kubwa lililokuwa kule Mererani. John na Aminata hawakuweza kutambua waliko. John ndiye wa kwanza kuzinduka na kujikuta akivuja damu sehemu za usoni na kwenye jicho la upande wa kulia.

“Mnataka nini nyie watu, si mseme na mtuachie twende zetu? Kwanza hapa ni wapi”? alifoka John kwa hasira baada ya kumwona Mosses Ndula karibu yake. Mosses Ndula alicheka kicheko cha dharau na kumchapa kibao tena John, wakati huo Aminata alikuwa analia huku kashikiliwa na Bosi Steve.

“Ulitaka kuchukua mali za baba angu, sasa hujaridhika unataka kunichukulia na mimi” haya fanya uwezavyo.”

“Unajidai hujui kilichosababisha kuwepo hapa we nyang’au? leo utatutambua kwamba sisi siyo hiyo Serikali yako inayowatuma kufanya uhuni wakati uhuni wenyewe hamuujui” Bosi Steve alimkaripia John na kumchapa tena ngumi ya tumboni.

“Sisi hatujatumwa na mtu. Wala hatuna tunalolitaka kwenu,” John alisema huku akimwangalia kwa hasira Mosses ambaye alikuwa amemwekea bastola kichwani.

“Kimya, Malaya mkubwa wewe, unataka kuleta upelelezi wa kizamani hapa, leo na wewe utanitambua, baada ya kufa kwa huyu nyang’au wa kiume utafuata wewe Malaya mkubwa, Bosi Steve alimkaripia Aminata ambaye alikuwa akilia.

“Chanzo cha yote haya ni huyu mpumbavu mwenzako….wote leo mtakufa. Namkumbuka sana. Alimlaghai mtu wangu ili kujua mambo yangu…sasa atayajulia aghera.”

Haikuwa rahisi kwa John kuweza kumjulisha rafiki yake Max aje kumwokoa.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni