
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Alimwona Mosses akiifuata helikopta kwa lengo la kutoroka lakini mara helikopta ile iliondoka na hivyo hakuweza tena kuipata. Aminata aliwahi na kuilenga ile helikopta na kuilipua.
Mosses alishtuka baada ya kuona imemuacha na kisha kulipuka.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Alikuwa bado hajamwona Aminata.
Ghafla alimwona Aminata akimfuata. Alianza kumrushia Aminata risasi ambazo zilikuwa zikimkosa huku Aminata akizidi kumsogelea. Alimfyatulia risasi ambayo ilimpata begani na kukaa chini. Mosses alikuwa akiangaliana na Aminata pasipo kuamini kwamba hajaambulia chochote kutokana na mipango yake.
Hasira zilimvaa huku akihema sana. Bastola yake ilikuwa mbali na alipo na hivyo hakuweza kuiokota. Alisimama ghafla na kunza kukimbia. Alifanikiwa kumtoroka Aminata lakini mbele yake alikuwa amesimama John ambaye alikuwa ameshamwona.
Aminata ambaye alikuwa akija kasi kumfukuza Mosses alishangaa kumwona Mosses akiwa amesimama ghafla huku akiwa ameshika bega. Mbele alimwona John. Alikuwa amemnyooshea bunduki Mosses tayari kwa kuifyetua kumlenga.
Mosses alishindwa la kufanya na kujikuta akiwa amezungukwa na John na Aminata. Mirindimo ya risasi iliendelea huku Mosses akionekana kukata tamaa.
“Ulijua hatutakukamata…. Mshenzi mkubwa wewe.. ulitaka kututisha na jeshi lako la mamia ya wanajeshi… Uwezo wa kikosi chako haukuuweza sasa umeungana na Steve… tumegundua kwamba ulifanya hila za kuchukua mgodi wa mzee wetu Amigolas kwa kutumia Hati Feki lakini tuliurudisha katika himaya yetu….
Ulimuua mwenyewe na sasa tumekupata… huwezi kutusumbua mtu kama wewe…. Tuligundua mengi kuhusu wewe, sasa mwisho wako umefika…. Hata kama ulifanikiwa kutoroka huwezi kukimbilia kokote… huwezi kutukimbia sisi… Tulijua tu ipo siku tutakukamata… na sasa hatukupeleki mahala popote kwani sasa wewe ni halali yetu… utakuwa maiti kama ulivyofanya kwa ndugu zangu,” John alikuwa anaongea kwa hasira na uchungu huku akiangaliwa na Aminata. Mosses alikuwa akijivuta kuelekea sehemu ambayo bastola yake ilikuwepo. Ghafla John alifyetua risasi ambayo ilimpata ya kichwa Mosses ambaye alikuwa akitaka kumfyetulia risasi John baada ya kuishika bastola yake. Alianguka chini na kufariki pale pale.
“Aminata,” aliita John huku akimfuata baada ya kuangalia saa yake na kugundua kwamba ni dakika mbili tu zilibakia kabla ya mabomu kulipuka na hivyo.
“John,” aliitikia Aminata huku akimfuata John. Walianza kukimbia wakielekea katika lango kuu la kutokea. Walikuwa wakisikia milio ya risasi huku wakiwaona Antony na Max wakirudi nyuma huku wakikimbia kuwafuata wao.
Mabomu yalianza kulipuka wote wakiwa wameshatoka nje ya lango kuu. Walisimama karibu na gari ambalo alikuja nalo Aminata na kuangalia lile jumba lilivyokuwa likilipuka.
“Antony… una nini,” Aminata alimuuliza Antony ambaye alikuwa ameshikilia bega lake la kulia huku likivuja damu.
“Tuwahini tumpeleke hospitali alipigwa risasi na wale washenzi.. tuwahini,” alisema Max huku wote wakiingia ndani ya gari ili kuwahi hospitali. Ghafla magari ya polisi yalikuwa yamefika na kuwasimamisha bila ya kujua wao ni nani. Wa kwanza kutoka alikuwa ni Max ambaye alitoa kitambulisho na kuwaonyesha.
“Mkimaliza kutukamata sisi hakikisheni na huyo waziri wa ulinzi anatiwa nguvuni… anayo kesi ya kujibu,” alisema John huku akitoka nje ya gari na kusimama na Max. polisi walielekea katika jengo lile lililokuwa likiwaka moto baada ya kulipuliwa na kuanza kukagua.
Watu walikuwa wengi waliokuja kushuhudia baada ya kusikia mlipuko ule. Wengi walikuwa wakishangilia kutokana na manyanyaso waliokuwa wakipewa na askari waliokuwa wakilinda jumba lile huku wengine wengi wakiuliwa pale walipojaribu kuingia katika barabara iliyokua mefichwa kuingia katika jumba lile.
“Wazari wa Ulinzi anahusika…. Haiwezekani askari wote wale wamilikiwe na mtu mmoja alafu ni mfanyabiashara,” alisema Max wakiwa nje ya Hospitali ya Mount Meru wakisubiri matibabu ya Antony.
“Tusimamieni tuhakikishe anashtakiwa.”
*****
Ilikuwa ni Jumapili wiki moja baada ya shambulio lile. Wengi walikuwa wakilifuatilia kwa karibu ili kujua hatima ya waziri wa ulinzi ambaye inasemekana alihusika pamoja na kundi lililokuwa likiongozwa na Steve na Mosses Ndula.
Katika taarifa ambayo ilikuwa ikirushwa hewani, baadhi ya mambo yalikuwa yakizungumzia ambayo yaligusa sana hisia za watu na kufnya kila mtu afatilie kwa makini sakata hilo.
“Habari ambazo zimetawala katika mkoa wa Arusha na nchi nzima zinasema kwamba, Waziri wa Ulinzi alishirikiana na mfanyabiashara maarufu kuanzisha kambi ya siri ya kihalifu iliyokuwa inatishia amani katika mkoa wa Arusha nan chi nzima. Inasemekana ya kwamba waziri huyo alichukua baadhi ya wanajeshi wan chi na kuwapeleka ili kuimarisha kambi hiyo ya kihalifu iliyokuwa ikisimamiwa na mfanyabiashaara mkubwa Steve Muro. Kambi hiyo ilikuwa Mererani karibu na migodi ya madini ambayo ni maarufu ya Tanzanite na ilikuwa ni kambi ya siri ambayo haikuwa rahisi kujulikana.
Tuhuma zinapelekwa kwa waziri huyo ambaye ameshindwa kusimamia usalama wa nchi kwa kufanya mambo kwa masilahi yake binfsi. Pia katika kambi hiyo alikuwapo mkuu wa vikosi hivyo ambaye alijulikana kwa jina la Mosses Ndula ambaye awali inasemekana kuwa ndiye aliyekuwa akifanya biashara za magendo na baadhi ya viongozi wakubwa wa nchi pamoja na uhalifu.
Katika tukio ambalo linathibitishwa kwamba alihusika nalo ni lile la mauaji ya mzee Amigolas mfanyabiashara mkubwa wa madini ambaye alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Steve Muro pamoja na familia yake kisha kuiba hati ambayo hata hivyo ilisemekana kuwa ni feki na hivyo baada ya watoto wake mzee Amigolas, John na Antony kubaini hayo, waliamua kufanya kila wawezalo ili warudishe haki zote chini yao ambapo walifanikiwa.
Kwa sasa polisi wanamshikilia waziri huyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sharia ili kujibu tuhuma hizo.”
“Mmesikia,” Max alisema akiwaambia John na Aminata wakati wakielekea nyumbani kwa Antony kumjulia hali. Antony alikuwa akiishi peke yake katika nyumba ambayo aliinunua katika maeneo ya Sombetini. Aliwaacha John pamoja na mke wake Aminata wakae katika nyumba yao iliyokuwa maeneo ya Njiro.
“Niliipeleka ile ripoti kwa maofisa wa polisi ili iweze kusomwa kwa wananchi wajue ukweli wa mambo. Nchi ilikuwa imeshaanza kugeuzwa mradi wa wachache. Tumefanikiwa kumdhibiti.
Antony alirudi akitokea Mererani ambako alienda kusimamia na kuhakikisha hali katika mgodi wao unakuwa salama. Aliwakuta kina John na Aminata wkiwa nje ya nyumba yao pamoja na mtoto wao Amigolas na Max.
“Mambo yatakuwa mazuri, kwa muda huu mchache nimeshamalizana na wote.”
“Subiri kwanza,” alidakia John…. “Francis umempa kazi,” aliuliza John.
“Eeeh, kweli. Nakumbuka ulimwahidi.”
“Ndio, yupo kazini na kazi zimeanza,” Alisema Antony huku akikaa chini kwenye bustani ya majani karibu na Amigolas.
“Poa, nadhani mambo hata huku si mabaya,” alisema John. Wote walionekana ni wenye kujivunia jambo moja tu…. USHINDI.
MWISHO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi