MAUAJI YA KASISI (1)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KWANZA HOLY FAMILY BASILICA NAIROBI HAKUNA mtu aliyeamini anachokiona mbele yake, kila aliyepita njia alitikisa kichwa na wengine kuangusha machozi. Polisi kutoka kituo cha kati cha Nairobi walikuwa hapo mbele ya kanisa hilo kubwa wakifanya uchunguzi wa hili na lile. Mwili usio na uhai ulikuwa umelala chini na majeraha makubwa kifuani yakiwa yameganda damu nzito. Hakuna asiyejua mwili ule ni wa nani, kila aliyepita alisikitika, wengine hata walighairisha safari zao za kazini, vilio vilitawala eneo lile. Kila mtu alionekana kuguswa kwa namna moja au nyingine na mauaji ya Kasisi huyu wa kanisa la Roman Catholic, Rev Fr Frederick Gichuru , hakuna aliyejua kwa nini na ni nani aliyetekeleza mauaji haya ya kinyama. Baada ya kumsachi hakuna cha ziada walichokikuta katika kanzu ya kasisi huyo zaidi ya rozari iliyokuwa mkononi mwake. “Bila shaka alikuwa katika sala zake za asubuhi” sauti ya kukwaruza kutoka kwa koplo Otholong’ong’o ilipenya siki…