MAUAJI YA KASISI (4)

Zephiline F Ezekiel
MAUAJI YA KASISI (4)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Siku moja alitembelewa na mtu asiyemjua, baada ya mazungumzo marefu sana walifahamiana kuwa kumbe wao ni ndugu, na sasa huyu ambaye angetakiwa kumwita kaka alikuwa ni mtu mkubwa kwatika mji huo wa Achen. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Ndiyo, mimi ni Andreas Schurmman , baba yangu mimi mzee Ernst Schurmman alizaliwa tumbo moja na mama yako Angela Schurmman, wakati wa vita ya pili ya duni ndipo walipopoteza maisha katika mazingira tofauti na wewe ulichukuliwa ukiwa mdogo na babu yako aliyemzaa mama yako, mimi nililelewa na msamalia mwema tu mpaka nimekuwa hivi nilivo.” Gustav alitikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa aliielewa hiyo safari ya maisha jinsi ilivyokuwa. “Umejuaje kama nipo hapa?” “Nina rafiki yangu ambaye ni mfanya kazi hapa ndiye aliyeniambia lakini hata yeye hajui kuwa mimi na wewe tuna undugu, ila mimi nilijua kwa kuw…