MKONO WA JASUSI (21)
Jina: MKONO WA JASUSI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Kwa mbali alimwona Don akifanya uhakiki wa tiketi zake, jicho la Kamanda likatua kwa mwanadada aliyekuwa akiifanya kazi ile, ‘Bingo!’ akajisemea kisha akasubiri Don na vijana wake waondoke katika eneo lile ili naye akafanye yake. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alipohakikisha Don keshaingia ndani kabisa, akavuta hatua na kuwapita baadhi ya wasafiri waliokuwa kwenye foleni huku akiwaomba samahani na moja kwa moja akafika kwenye kidawati cha Yule mwanadada. “Habari msichana! Mimi ni mwanausalama,” akamwonesha kitambulisho ‘feki’ cha upolisi wa Afrika Kusini. “Ndiyo nikusaidie nini?” Yule mwanadada akamwuliza, na kamanda akaeleza shida yake; bila hiyana akapatiwa maelezo yote kuwa Don anaelekea Canada katika jiji la Ontario kwa ndege ya shirika la USA, IATA Airlines . Akamshukuru na kauondoka eneo hilo. §§§§§ “Yes! Madam S, …