NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (2)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... “Utanilisha nini?” aliniuliza swali dogo sana ambalo lilikuwa na maana kubwa. Nilibaki kimya nikimwangalia, sikutarajia kupata swali kama hilo kutoka kwake. Ni kweli alikuwa na uhuru wa kuuliza kuhusu majukumu yangu kama mwanaume kwake. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alikuwa akipendeza sana, hii ilimaanisha kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya kazi hiyo, yaani kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akishughulika na mavazi tu, mwingine nauli za usafiri mwingine viatu na mwingine make up, sasa mimi ningeshughulika na nini? Hata kama angeniambia nishughulike na vocha tu nisingeweza kutokana na kiasi cha pesa kilichokuwa kikihitajika. “Kwani wewe unataka nini?” nilimuuliza ili nijue. “Matunzo! Mtoto mzuri kama mimi nitunzwe, nitolewe out, niletewe baga, pizza, ice cream, uninunulie pafyumu, ninukie, au hutai demu wako ninukie …