NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (4)

Zephiline F Ezekiel
NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (4)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Alininunulia kitanda cha chuma, chumba kikapigwa rangi na kunipa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya matumizi yangu mengine. Kumbuka mpaka kipindi hicho sikuwa nimeiuza ile almasi kwa sababu sikujua soko lipo wapi na sikuwa na mtu wa kumwamini hata kidogo. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili niliendelea kutafuta soko taratibu. Siku ziliendelea kukatika na baada ya siku mbili nikapata taarifa kwamba rafiki yetu, Mrisho aliuawa na mwili wake kutupwa baharini. Nilishtuka sana, huyu Mrisho alikuwa mlinzi mwenzangu pale Kariakoo na alikuwa miongoni mwa watu ambao tulimsaidia yule mzee kumpeleka hospitalini. Msiba wake uliwagusa watu wengi, alikuwa kijana mpole, sasa ilikuwaje awe na maadui na wakati kila wakati alikuwa mcheshi na hakubagua ni nani wa kuongea naye? Tulihuzunika sana hiv…