CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (4)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
Kitendo cha kuingia na bodaboda nyumbani kwake,

kikamshtua Musa ambaye tayari alikuwa amejiandaa kudumbukia chumbani kwa baba Shua ili kumkabili mama Shua.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Alipomuona baba Shua tu, akajifanya anatoka nje moja kwa moja. “Za asubuhi baba Shua,” alisema Musa kwa sauti ya chini. “Salama tu kijana mwenzangu,

daah halafu nilisahau kukwambia kuwa nasafiri na hapa nimerudi mara moja kuna kitu nimesahau.” Musa akacheka kimoyomoyo. “Angejua najua kila kitu na hapa nimenusurika kufumwa hata asingeongea yote hayo.” Alimwacha baba Shua akiingia chumbani kwake. Alipofika alimkuta mama Shua akiwa katika kanga moja tu kwenye kochi.

“Vipi tena, leo kazini huendi?” “Baba Shua! Hapa nilikuwa natafakari nitawezaje kuvumilia kukaa mbali na wewe hasa huyu mtoto wetu Shua,” alimuongopea na kumuuliza swali. “Vipi kulikoni tena mume wangu, hakuna safari?” “Safari ipo ila nimesahau karatasi zangu muhimu ambazo natakiwa kuwa nazo huko niendako,” aliongea baba Shua huku akiwa katika haraka na kufungua baadhi ya karatasi zake za kazini kisha akamsogelea mama Shua na kumbusu shavuni. “Narudia tena mke wangu, kuwa mwangalifu na mbaki salama.”

Hadi anaingia chumbani kwake, bado Musa hakuelewa picha lolote linaloendelea, kila akishika simu yake na kutaka kutuma meseji, alikuwa akisita kwamba lazima baba Shua atashtukia. “Hivi kweli mama Shua alikuwa anataka kunifanyia mtego?” alijiuliza Musa bila kupata jibu. Ndani ya muda mfupi akasikia tena mlio wa bodaboda ikiondoka, hajakaa sawa simu yake ikaingia meseji. “Ameondoka tena!” “Ujue umenitia presha?” “Kwa nini tena mpenzi?” “Si umeniambia ameshasafiri kumbe bado yupo mjini?” “Acha woga wangu, kuna kitu alisahau na hata hivyo hawezi kurudi tena we njoo.” “Kwako?” “Ndiyo!” “Kama ni kwako, hapana aisee, asije akarudi tena.” “Sasa wewe unataka wapi?” “Gesti!” “Ondoa uoga wako, basi sehemu za kukuficha hapa chumbani zipo kama itatokea, lakini jua harudi tena na hapo alipo anaenda kulifukizia basi.” Meseji ile ilimkosha Musa, akajiandaa upya na kuanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwa mama Shua.

Alipoukaribia mlango, akafungua na kuchungulia kwa ndani akakutana uso kwa uso na mama Shua. “Ingia sasa unaogopa nini?” Musa akadumbukia na kuongoza hadi kwenye kochi. “Mchumba wangu Shua yupo wapi?” “Shua muda huu, bado kamelala huko chumbani.” “Haya niambie, hapa au chumbani?” “Tuanze hapahapa kisha uhondo ukizidi tunamalizia chumbani,” alisema mama Shua huku akiinuka na kuusogelea mlango kwa lengo la kuufunga. Nyuma Musa alikuwa akifaidi kwa macho kwa kuitazama ile kanga moja aliyokuwa amejifunga mama Shua ambapo ndani yake hakukuwa na nguo ya ndani. “Sogea nikwambie kitu,” alisema mama Shua baada ya kuhakikisha ameufunga mlango.

“Hapo!” “Ndiyo njoo hapa kwangu!” Mama Shua alianza mbwembe, mbwembe kama zile za kwenye filamu za Kihindi. Musa akasogea hadi karibu yake. Kabla mama Shua hajaanza kumbakili Musa mara sauti ya meseji kwenye simu yake iliyokuwa kwenye kochi ikasikika. “Mpenzi umesikia meseji kwenye simu yako,” alisema Musa. Kwa hofu, mama Shua akaifuata na kusoma ujumbe kisha akaguna. “Mitandao mingine bwana, eti furahia kutumia mtandao huu.” Akaifuta ile meseji lakini kabla

hajairudisha ile simu pale kwenye kochi mara ikaita, mama Shua akabaki akiitolea macho huku akishindwa kuipokea kutokana na simu yake kuwa na mlio mkubwa pindi akiongea na mtu. Muda wote Musa alikuwa akimtolea macho. “Pokea sasa,” aliongea Musa na

kumfanya mama Shua apokee. “Haloo baba Shua!” “Sijui nina mkosi gani mimi, umeshaenda kazini?” aliongea baba Shua kwenye simu......

“Bado…” “Leo mbona umechelewa sana, kuna nini mama Shua?”

“Ndiyo najiandaa hapa baba Shua.”

Wakati huo, siku nyingi Musa alishafika chumbani kwake na kukaa kwenye kitanda akihema.

Yeye alipomsikia baba Shua akisema ‘sijui nina mkosi gani?’ alikuwa njiani anarudi alisahau kitu kingine tena…

“Oke, sasa hapo juu ya kabati kuna fedha kwenye bahasha, chukua ukanitumie kwa J-Pesa.”

“Sawa…kwani umeshaingia kwenye basi?”

“Ndiyo linaondoka muda huu.” “Haya, safari njema mume wangu.”

“Sawa mke wangu, baki salama lakini take care.”

“Usijali.”

Mama Shua, japokuwa muda ulipita kweli, alitakiwa awe njiani anakwenda kazini, lakini hakukubali, alichukua simu na kumtumia meseji Musa…

“Oyaa! Vipi wewe? Mbona uliingia mitini?”

“Mh! Si jamaa kasahau kitu tena?”

“Hamna, kuna pesa alitaka nimtumie alizisahau kwenye bahasha,” alisema mama Shua. “Kwani amesema basi limeshaondoka?”

“Ndiyo.”

Musa, sasa alikuwa ndani ya bukta, kifua wazi akachomoka na kuingia ndani kwa mama Shua. Mama Shua naye hakuwa na sababu ya kucheleweshana, alimzamisha chumbani Musa huku akiwa anachojoa kanga yake moja na kuitupia chini. Musa kuona mwili wa mama Shua stimu ilipanda, akapagawa. Macho yake yalihisi kizunguzungu, akajikuta akihema kwa nguvu.

Licha ya kwamba ni kijana lakini ujana wake ni ule wa ‘kukurupuka’, kwamba akichelewa sana anaweza akamalizia mambo mlangoni.

Alivua bukta kwa fujo, akaitupa chini kisha, akamrukia mama Shua, wote wakaenda kitandani, Musa akaingia uwanjani lakini hapohapo akapata ushindi kwa kuvunja dafu lake moja.

“Aaah! Kwa nini sasa?” mama Shua ambaye alikuwa hajafika popote, alimuuliza Musa kwa mshangao mkubwa…

“Hata mimi sijui, huwa inanitokea kama mwanamke nimempenda sana halafu mara ya kwanza,” alisema Musa huku akionekana kujisikia aibu…

“Kwa hiyo mara ya pili hali hii haitatokea?” aliuliza mama Shua…

“Haiwezi kutokea. Loo! Hakuna kitu kama hicho.” “Sawa! Sasa twende makazini, jioni tukutane tena, si itakuwa mara ya pili?”

“Ndiyo,” alisema Musa huku akitoka kwa kasi kurudi kwake kisha akaenda bafuni kuoga huku moyoni akisema…

“Da! Hii ni aibu kweli. Yaani mtoto mzuri vile nimeshindwa kumfikisha kwenye nyavu? Mimi naye bwana! hii aibu ya kuwahi sijui itakwisha lini?”

Musa alianza kuwakumbuka mademu zake ambao walimkimbia au kumpiga chenga kufuatia tabia yake hiyo ya kidogo tu, haooo!

Mama Shua alisubiri Musa alipotoka bafuni kuoga, akaingia na yeye huku moyoni akisema… “Siamini kama leo nimelala na Musa…kijana nimempenda sana, saizi yangu kabisa.”

Musa ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka akakimbia hadi kwenye gari lake, akaliwasha na kumpigia simu mama Shua…

“Oya vipi, nikusubiri?” Musa alimuuliza mama Shua… “Nisubiri mpenzi wangu, tayari nimeshatoka.”

Mama Shua alitembea haraka mpaka kwenye gari la Musa, akafunguliwa mlango na kuzama ndani…

“Da! Leo nimechelewa kweli, nadhani hata wewe?” alisema mama Shua…

“Sana. Lakini kazini kwangu hakuna noma, labda kwako.”

“Mimi pia, ila noma ipo kwa mume wangu…mume wangu anaweza akampigia bosi wangu kutaka kujua kama nimefika.”

“He! Ana tabia hiyo mumeo?”

“Sana tu.” “Kazi unayo. Lakini anaonekana anakupenda sana.”

“Ah! Ananipenda ndiyo lakini wivu wake kwangu ni wa kijinga.”

“Ha! Wivu wa kijinga ndiyo wivu gani baby wangu?”

Mama Shua alijisikia raha kuitwa ‘baby wangu’…

“Si wa kumfuatilia mtu mpaka kero.”

“Mh!” aliguna Musa, mama Shua hakujua ni kwa nini kijana huyo aliguna.

Musa alimshusha mama Shua nje ya ofisi yake, yeye akapitiliza hadi kazini kwake. Lakini siku hiyo alianza kuona ubaya wa ‘kumaliza’ haraka, hasa kwa demu mzuri kama mama Shua.

Unaweza kulisikia jina la mama Shua ukahisi ni mwanamke aliyekwenda ‘eji’ kwa sababu ya kuzaa. Lakini alikuwa na miaka 23 tu!

Sura yake ilivutia kwa vile alivyo na mvuto wa kisichana, macho kama gololi. Nyusi nyingi juu ya macho, ungemwona ungesema Mhindi.

Kuanzia kiunoni kwenda chini alitengenezwa kama wa kuchora kwani alibinukia nyuma. Sehemu ya matiti ilijichomoza kwa mbele huku yakiwa yamesimama na kulifanya tumbo lake kujificha kwa ndani.

Kwa mwanaume yeyote rijali aliyekutana na mama Shua njiani alilazimika kugeuka kumwangalia hata kama alikuwa ameongozana na mke wake mtata.

***

Saa saba kamili, mama Shua alimkumbuka Musa, kwamba ni muda wa lanchi, akamtumia meseji…

“Baby, lanchi, umeshapata?” “Da! Ndiyo najiandaa kutoka. Lakini nikitoka muda huu sirudi tena, nakwenda home.”

“Kuna nini?”

“Nimechoka sana leo, sijui kwa nini?!”

“Jamani, au na mimi nitoke tukalale hotelini, nikupetipeti halafu tuingie ile mara ya pili uliy-oniahidi?”

 Musa alikosa raha ghafla, akajikuta akikumbuka mambo ya asubuhi. Alijilaumu sana kwa kushindwa kumuda kudumu kwa hata dakika kumi kwenye sita kwa sita…

“Lakini sasa hata kama namaliza haraka, basi si nitumie hata dakika kumi,” alisema moyoni.

Kabla ya kumjibu mama Shua, alizama kwenye mitandao ya kijamii kwanza na kusachi mada inayosema; ‘je, una tatizo la kumaliza haraka tendo la ndoa? Soma hapa!’

Musa alizama kwenye mada hiyo na kukutana na elimu mbalimbali ikiwemo kuambiwa akiwa kwenye sita kwa sita asiweke mawazo kwa asilimia mia moja. Pia, asimshobokee kivile mwanamke aliye naye.

Akaambiwa asimuone mwanamke huyo ni kama ‘malaika’ na kwamba wengi wanawaona wanawake kama ‘malaika’ ndiyo hujikuta wakimaliza mapema kwa kuwa wanakuwa hawaamini.

Alipomaliza, ndiyo akashika simu ili amjibu mama Shua…

“Kwani we unaweza kutoka muda huu?”

“Naweza baby.”

“Poa twende,” alisema Musa lakini huku moyoni akijiuliza. Je, ni kweli mara ya pili hiyo atamudu kudumu kwa muda na kumfanya mama Shua ajisikie yupo na mwanaume rijali?

Musa ndiye aliyetangulia kutoka kazini, akatafuta hoteli, akalipia. Akamjulisha mama Shua…

“Poa, nakuja ndani ya dakika kumi tu kipenzi changu,” alisema mama Shua huku akifungafunga kazi zake na kutoka.

Njiani, mama Shua alimuwazia sana Musa…

“Leo nikapate hiyo raha. Asubuhi alisema akirudia anakuwa ngangari. Maana muda ule sikufika popote pale,” alisema moyoni mama Shua.

***

Kule hotelini, Musa alikuwa vizuri kiasi kwamba aliamini yote aliyoyasoma kwenye mtandao ni ya kweli…

“Mbona kama niko vizuri sana muda huu. Akitokea hapa hakuna kupoteza hata dakika moja…ni kazi tu,” alisema moyoni Musa.

***

Ndani ya dakika kama nane, mama Shua akawa amefika hotelini. Alifuata maelekezo mpaka akafika kwenye mlango wa chumba alichokuwemo Musa…

“Ngo… ngo… ngo…” aligonga mlango. Musa alisimama haraka na kwenda kufungua.

“Karibu baby…” “Asante baby…mmmwaaaa,” mama Shua alikaribia na kumpiga busu zito Musa…

“Asante sana baby,” alishukuru Musa huku akimkumbatia.

Ile mama Shua anakaa tu kitandani,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni