CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (6)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
“Hivi ni kwa nini umeng’ang’ania hilo suala?”

“Nasema kwa sababu najua bwana, usinidanganye.”

“Niamini kweli kabisa.” “Sikuamini hata kidogo, kwanza nimeshajua iko siku nitajikuta umeniambukiza virusi lakini mimi kama nitakufa itakuwa kwa ajili yako,”

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI

ENDELEA...
alisema mama Shua.

Mazungumzo hayo yalimfanya mama Musa kukosa hali ya kucheza mechi na kujikuta akipitisha madakika bila kumaliza kibarua chake. Mama Shua alianza kubadilika sauti huku akiendelea kuonga baada ya kuanza kufikia hatua ya mwisho wa mchezo ambapo aliweweseka.

Musa naye, kuona mama Shua yuko kwenye kituo cha mwisho na yeye aliweweseka hadi akajikuta akitaka kupoteza fahamu.

***

Siku za baba Shua kukaa Arusha zilibaki mbili, lakini akarudi nyumbani kwake Dar bila kuzimaliza. Alifika saa kumi na mbili na nusu jioni na kukuta mkewe yuko bafuni anaoga, akachukua simu yake na kukaa sebuleni akaanza kupekua meseji moja baada ya nyingine.

meseji ya kwanza ilikuwa ya mama Shua kwenda kwa Musa, iliandikwa…

“Vipi leo, nahisi kama kuna ulazima. Au wewe unasemaje? Nakusiliza.”

Akafungua majibu ya Musa huku moyoni akisema…

”Huyu Musa huyu…si ndiyo huyu kijana mgeni aliyehamia humu ndani?”

Mara, mkewe akatokea. Alipomwona mumewe ameshika simu yake na anajua mna meseji za Musa, mwanamke huyo huku akiwa amejifunga kanga moja tu, aliruka kama chui na kufika kwenye mwili wa mume wake…

“Baba Shua nini bwana unasoma meseji zangu?” alisema mama Shua lakini aliikosa simu yake kwani baba Shua aliinua mkono juu zaidi na kumfanya mkewe huyo kuangukia mapajani mwake… “Una siri gani humu kwenye simu mpaka unanikataza kuangalia? Kwanza umeanza lini?”

Mama Shua alikosa jibu, lakini akabaki hapohapo kwenye mapaja ya mumewe akizuia mumewe asisome meseji zake…

“Sasa nahisi unataka kupigwa ndiyo unijue mimi ni nani!” alisema baba Shua, mama Shua akaogopa lakini hakumruhusu mumewe kusoma meseji zake.

Kitendo hicho kilimfanya baba Shua kuzidi kuhisi vibaya kwani kama kweli mkewe angekuwa mwema kwenye simu hiyo asingetumia nguvu vile kumzuia asisome meseji…

“Na kwa taarifa yako nimeshaona meseji ya Musa,” alisema mwanaume huyo.

Mama Shua akazidi kuogopa, akaweweseka ile mbaya huku akisema…

“Mimi sina uhusiano naye mbaya. Labda mawazo yako tu.”

“Kama mawazo yangu acha nione meseji nyingine…” “Sitaki na simu yangu, kwani mi nimesoma meseji zako?”

Ilibidi baba Shua atumie nguvu ya ziada kumchomoa mkewe kwenye mapaja yake, akaanguka chini lakini na yeye simu ikaanguka chini, mkewe akaidaka na kukimbilia chumbani. Kule chumbani, mama Shua alizifuta meseji zote kisha akamtumia meseji moja Musa…

“Kimenuka, usitume meseji wala kupiga simu mpaka nitakapoanza mimi.”

Akaifuta meseji hiyo na kutoka na simu…

“Eee, simu hiyo angalia kama kuna kitu,” mama Shua alimwambia mume wake… “Hivi wewe kumbe siku zote ulijua unaishi na mwanaume asiyekuwa na akili siyo? Unaweza kunichezea akili mimi?”

Mama Shua alimwona mume wake amabadilika rangi, akatambua upuuzi wake.

Baba Shua alisimama, akaenda kumgongea mlango Musa… “Dogo!”

“Naam.”

“Toka nje.”

“Mh! Kweli kimenuka,” alisema moyoni Musa huku akitoka. Moyo ulikuwa ukimdunda sana… “Oya! We unachati na mke wangu siyo?”

“Mimi bro?”

“Si ndiye ninayeongea naye hapa. Sasa unaniulizaje mimi bro?”

“Mwite athibitishe.”

Mama Shua aliposikia Musa anaruka kimanga na anataka aitwe athibitishe, aliifuta namba ya Musa kwenye simu kisha akaibadili namba ya mfanyakazi mwenzake anayeitwa Xsaver kuwa Musa.

Alitoka mwenyewe bila kuitwa…

“Baba Shua si nimekukatalia pale kwamba sina uhusiano na huyu kijana. Mbona unanilazimisha?” “Unataka kuniambia huna namba yake ya simu?”

“Sina.”

“Lete simu yako.”

Baba Shua alisachi jina la Musa kwenye simu, likatokea, akaipiga ile namba akiwa ameiweka simu sikioni. Iliita lakini si ya Musa yule japo yeye aliishika simu yake…

“Niambie dada angu?” upande wa pili wa simu ulisikika ukisema, baba Shua akakata simu na kumrudishia mke wake…

“Sawa, lakini nitaendelea kuchunguza,” alisema akirudi ndani. Mama Shua naye akarudi ndani, pia Musa. Sasa ikawa, Musa ana namba ya mama Shua lakini mama Shua hana.

Siku hiyo ilipita, ikafuata siku nyingine. Asubuhi Musa alikwenda kuoga, akamkuta mama Shua na msichana wake wa kazi wako uani. Alisalimia, akaingia bafuni kuoga. Alipotoka, alimkuta baba Shua na mtoto Shua nao wapo uani. Musa akamsalimia baba Shua kisha akamwinamia Shua…

“Mchumba…mchumba…hujambo?”

“Mwambie sijambo,” alisema mama Shua akimfundisha mtoto wake…

“Sijambo…”

“Sasa leo vipi, tutakutana saa ngapi tukale raha mchumba?” alisema Musa akiwa bado amemwinamia Shua…

“Mwambie wewe tu ukitoka kazini unitafute.”

“Tafute mimi,” alisema Shua akiwa amekosea lakini ujumbe ulifika…

“Sasa tatizo wewe mchumba huna simu…” “Mwambie wewe si unayo unipigie ukitoka kazini.”

Muda wote huo, baba Shua yeye alikuwa akicheka jinsi mwanaye anavyojibu…

“Piga wewe… kazini,” alisema Shua kwa kukatakata maneno.

“Haya nitakupigia ujiandae.” “Mwambie usiwe na wasiwasi mchumba.”

“Wasiwasi …chumba,” alisema Shua akiuma kidole kimoja cha mkono.

Musa alijiandaa akaondoka zake. Mama Shua naye alijiandaa akaondoka zake. Lakini alijitahidi sana kutafuta namna ya kuwasiliana na Musa mchana akashindwa. Musa naye alihisi kumtafuta mwanamke huyo kwa simu kunaweza kuleta kizaazaa baadaye kwa mume wake. Akaogopa.

***

Giza likiwa limeshaingia, Musa anarudi sasa, akakutana na

mama Shua njiani… “Musa vipi? We unajua namba yako sina, kwa nini usinitafute wakati we unayo? Kwani ule ujumbe wangu asubuhi kupitia kwa mtoto hukuulewa?”

“Ujumbe upi?” aliuliza Musa…

“We si tulipanga tukitoka job unipigie!”

“Tuliongea wapi mama Shua?”

“Kwani hukunielewa muda ule asubuhi ulipokuwa unajibizana na mwanangu Shua?”

“Oh! Kumbe pale ulikuwa unanipa ujumbe wa moja kwa moja siyo?”

“Sasa je?”

“Ungesema sasa.”

“Sasa pale ningesemaje we unavyodhani?”

“Basi yaishe…sevu upya namba zangu.”

“Zitaje, lakini sitazisevu, nitaziweka kichwani tu.”

“Sawa,” alijibu Musa huku akimtajia mama Shua namba zake.

Kisha, haraka sana mama Shua alirudi ndani akimtaka Musa kuchelewa hata dakika tano ndipo aingie…

“Usiingie sasa hivi, itajulikana. We kaa kwanza mahali, baada ya dakika tano ingia, sawa mpenzi wangu?”

“Sawa. Lakini da! Jamaa naye anafuatilia sana bwana,” alisema Musa akirudi alikotoka.

Alikwenda kwenye duka la jirani na kuomba soda ili apotezee muda. Alikunywa, alipomaliza alikwenda kwake. Ni baada ya dakika kama kumi na mbili hivi.

Chumba kilikuwa kizito kwa Musa kwani muda mwingi alijikuta akimuwaza mama Shua na mambo yaliyojitokeza kuhusu mume wake…

“Nahisi hii nyumba si ya kuishi mimi. Kama ndani ya mwezi mmoja tu jamaa ameshtuka kitu. Je, nikikaa mwaka mmoja si nitakatwa masikio mimi!”

***

Kwa upande wake, mama Shua hali ilikuwa ya utulivu wa kimawazo. Yeye alishatekwa na kijana huyo hivyo alikuwa akiwaza namna atakavyodumisha penzi…

“Musa ni kijana mzuri sana. Lakini sasa itakuaje wakati mista naye kama hataki kumsikia achilia mbali kumwona?” alijiuliza, akakosa jawabu.

Muda ulivyozidi kwenda, alipanda kitandani akalala. Alitamani sana kumtumia meseji Musa lakini mume wake alishalala hivyo aliamini angeweza kuzua mapya jambo ambalo hakulipenda hata kidogo!

***

Kulikucha, oyaoya za kujiandaa ndani ya nyumba zilipamba moto. Baba Shua, mama Shua, Shua walikuwa uani na msichana wa kazi. Musa yeye alivaa bukta na singilendi huku taulo akilitupia begani kwa ajili ya kwenda kuoga.

“Hujambo mchumba?” alianza Musa. Safari hii alikuwa tayari kupokea ujumbe kutoka kwa mama Shua kama alivyomwambia jana yake…

“Mwambie sijambo, nimekumisi sana.”

“Jambo…misi sana.”

“Hata mimi. Sasa leo tutapata wapi lanchi mchana mchumba?”

“Mwambie unipigie, popote ulipo nitakuja.”

“Nakuja…”

Walicheka wote kwani Shua alishindwa kunyoosha Kiswahili, Musa akaendelea…

“Mchumba, kweli utaweza kuja nikikuita mahali kwa ajili ya lanchi?”

“Mwambie nitaweza bila shida,” hapo alisema baba Shua…

“Aweza.”

“Haya, basi nitakupigia.”

“Mwambie sawa usikose, iwe saa saba kamili,” hapo alidakia mama Shua…

“Saa saba …amili.”

Walicheka tena, Musa akaingia kuoga chapuchapu. Alitoka, akaingia mama Shua. Yeye alioga akifurahia kusikia raha anaoga huku akiyaona majimaji yaliyobaki kwa kuoga Musa.

Alipomaliza naye alitoka kwa kasi akisema amechelewa sana siku hiyo…

“Mbona siku ile nakwenda Arusha ulichelewa sana na sikukusikia ukilalamika. Imekuaje leo?” aliuliza baba Shua.

“Hata siku ile nililalamika, sema sikukwambia tu.”

“Mh!” Aliguna baba Shua.

Musa alitoka, wakati anapita kwenye dirisha, mama Shua alimwona, naye akajiandaa haraka sana huku moyoni akisema…

“Kwani akinipa lifti mbele kwa mbele kuna tatizo gani? Yaani mume wangu yeye anawaza mabaya kila wakati.”

Tangu, Musa atoke, mama Shua alitumia ndani kama dakika tano, naye akatoka lakini alishamtumia meseji Musa kumwambia amsubiri ampe lifti. Na Musa naye alijibu…

“Mh! Huogopi?”

“Wala!” alijibu mama Shua.

Mama Shua alitoka mbio kiasi kwamba mumewe akashtuka sana…

“Kinachokufanya ukimbie ni nini mama Shua?”

“Nawahi baba Shua, si nimekwambia wakati natoka kuoga jamani mume wangu!?” alijibu mama Shua huku akikimbia kitendo kilichomfanya baba Shua kushindwa kuendelea kuhoji au kusema lolote jingine.

Mama Shua alipotea akimuwahi Musa, mumewe akiwa ndani ya bukta na singilendi kwa juu naye alitoka mbio akimwambia msichana wa kazi…

“Dada nakuja sasa hivi.”

Mbele kidogo, baba Shua alikutana na Bajaj inashusha abiria…

“Eee bwana niwaishe mahali,” alimwambia suka wa Bajaj.

Bajaj iligeuzwa kwa kasi kutokana na hali ya uso wa baba Shua, dereva akajua anawahi sehemu kwa dharura.

“Nipeleke kule, kanyaga mafuta kama unafukuza mwizi.”

***

Mama Shua alizama ndani ya gari la Musa…

“Ondoa gari, maana kama sijamuelewa mume wangu, anaweza akafuatilia,” alisema mama Shua.

Ile anafunga mlango tu, Bajaj aliyopanda mume wake ikatokea kwa mbali kidogo.

Baba Shua alitumbua macho mbele akiamini kama mke wake atakuwa anaondoka na daladala lazima angemwona anakaribia kituoni na kama hayupo, ina maana atakuwa ndani ya gari analoliona la Musa ambalo yeye baba Shua halijui.

“Unaweza kuendesha kwa kasi hadi kulifikia lile gari?” baba Shua alimuuliza dereva ambaye badala ya kujibu aliongeza mafuta kwa kasi. Lakini wakati analikaribia,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni