CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (7)
Jina: CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA Mtunzi: Global Publisher SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... ina maana atakuwa ndani ya gari analoliona la Musa ambalo yeye baba Shua halijui. “Unaweza kuendesha kwa kasi hadi kulifikia lile gari?” baba Shua alimuuliza dereva ambaye badala ya kujibu aliongeza mafuta kwa kasi. Lakini wakati analikaribia, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... gari hilo likawa limeshaingia barabara kuu. Kwa mbali, ndani aliona watu wawili akiwemo dereva lakini hakuweza kupata mtazamo kamili kama ni wanaume, wanawake au mwanaume na mwanamke kwa vile vioo vya gari vilikuwa ‘tinted’… “Unajua kuna Bajaj inatufuata kwa kasi sana,” Musa alimwambia mama Shua. Ilibidi mwanamke huyo ageuke kuiangalia lakini akaiona kwa gizagiza sana. Kwa hiyo hakujua ndani ya gari lile mlikuwa na nani na ni nani! Baba Shua alimwambia suka waishie pale lakini akaisoma namba na kuandika kwenye simu yake kisha akarudi nyumbani a…