MAUAJI YA KASISI (12)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
kisha akayarudisha macho yake na kuyatuliza kule aliko Kamanda Amata na kuendelea kuona kinachojiri, huku akiendelea kunywa kinywaji chake. Mara alihisi, akipapaswa kwa nyuma maeneo ya kiunoni, akageuka na kukutana macho na mwanamke mshumami, aliyejiremba akarembeka,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
yule mwanamka aliyeonekana ana kila dalili ya ulevi machoni mwake alizunguka na kusimama mbela ya Melchior, akamrembulia macho, Melchior hakuonesha hata kumjali kwani yeye alitaka kujua tu nini kitatokea kule ndani, “Mwanamke unataka nini? Kama kinywaji chukua uende, mi sihitaji mwanamke saa hii,” Melchior alimwambia yule mwanamke, akamnunulia kinywaji kisha kwa akapewa shukrani ya sonyo kali na refu, “Go fish!” yule mwanamke alimwambia Melchior.

˜˜˜

“Bado mnanifuata Kamanda!” Bill alimwambia Amata huku akimimina kinywaji katika glass yake.

“Kwanza nashangaa kukuona huku, umekuja kufanya nini?” Amata alimuuliza Bill, cheko kali lilimtoka mpaka walinzi wake waligeuka kutazama ndani.

“Kamanda Amata, mimi si motto mdogo au punguani, najua ninachofanya na ninajua kila anayeingia katia wigo wangu popote pale katika pepo zote nne za dunia,” Bill aliongea kwa kujiamini, “Nina macho Kamanda, siyo haya mawili, mengi tu, na nilijuwa kuwa utakuja, maana una kiu na mimi, lakini ujue hata mimi nina kiu na wewe, umeshaniharibia mambo mengi sana,” akapiga fuinda moja kinywaji chote kikaishia tumboni mwake, akabeua kwa shibe ya kinywaji.

“Bill Van Getgand, unajua unachokizungumza? Nimekuja Nairobi, nashangaa naambiwa wewe unanihitaji, nisingeshindwa kuwararua hawa nyau wako hata kama wangekuwa hamsini, lakini kwa heshima yako nikawaacha na kuwatii kwa kuwa umeniita, na ungependa kuniona kabla ya jua la kesho kwa kuwa unajua kuwa jua la kesho sitaliona, ok, niambie ulichotaka kuniambia, unataka kunipa deal?” Kamanda Amata aliuliza.

“Oh, Kamanda, mi nipo hapa takribani wiki mbili sasa, nimekuja kibiashara, lakini nilijuwa safari yako ya kuja hapa Nairobi, nikajua wazi kuwa wewe ni mgeni wangu, ndo maana nikakukaribisha uje tustarehe, lakini nataka uniambie umekuja kufanya nini hapa Nairobi,” Bill alihoji kijanja.

“Bill, maswala yangu ya kikazi siwezi kukwambia wewe kuwa nimekuja kufanya nini, kama hilo ndilo uliloniitia basi hutopata jibu,”

“Hivi unajua kuwa upo mikononi mwangu?” Bill aliuliza

“Hata kama, lakini huwezi kunilazimisha nikwambie nimekuja kufanya nini,”

Bill akachomoa bastola yake na kumnyooshea Amata, “Utaniambia tu, maana hata nikikuua hapa hakuna atakayejua kama umekufa zaidi ya mimi na wewe mwenyewe,”

“Sitishiki na hiyo bastola ya Kirussi Bill,” Amata alijibu kijeuri, lakini kabla hajakaa vizuri, bastola ya Bill ikafyatuliwa, risasi ikapenye katikati ya paja na paja la Amata, ile sofa ikatimua vinyoya kidogo, Amata alitetemeak ka hofu, kijasho chembachemba kikamtiririka, akaona kuwa kumbe hapo hakuna usalama wala mzaha, hakuna urafiki kama upo basi ni wa mashaka.

“Usifikiri nakutania, nataka unieleze lile lililokuleta, na ukijifanya mjanja nakuua,” Bill aliongea huku akimlenga na ile bastola yake iliyoonekana wazi iko tayari muda wowote kufanya itakachoamuliwa, kabla hajajaibu, Bill alifyatua risasi kadhaa, moja katikati ya mapaja ya Amata, ya pili upande wake wa kushoto nay a tatau upande wa kulia, hali ile ilimfanya Amata aweweseke na kushindwa kujua atfanye nini, alibaki kutetemeka na kulowa jasho mwili mzima, akabana meno kwa hasira, “Nimekuja kukufuata wewe hayawani, na nakupa muda mchache tu utakuwa mikononi mwangu, Bill, ndipo dunia itakapojua kuwa roho moja dhalimu imeondoka duniani.”

“Aaaaaaa ha ha ha ha ha!” Cheko la Bill lilipasua anga la chumba kile, “Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency, hapa mmefika, nitawaacha hapa na mi nitaondoka na kile kilichonileta. Kama hauamini hujiulizi nimejuaje kuwa huko hapa! Ujue kuwa muda wowote nitaitwaa roho yako kabla ya jua la asubuhi inayofuata.” Bill akamalaiza risala yake na kugugumia tena glass nyingine ya kinywaji kikali, “Nimefurahi kukuona!” alimalizia na kuichukua fimbo yake ya kutembelea kisha kuondoka eneo lile.

“Tutaonana tena soon,” Amata alijibu kijeuri na kunyanyuka kuelekea mlango, kabla hajatoka mlangoni alisimama na kugeuka nyuma akagongana macho na Bill, wakatazamana, “Siku yetu inakuja,” alimwambia na mara wale walinzi wakamvuta kumtoa katika mlango ule alioutumia kuingilia na kenye ngazi alikuwana na yule mwanadada aliyemjia chumbani akiwa ameweka pozi akitazama yanayoendelea ukumbini mle, wakatazamana kwa sekunde, “Unahitaji lifti yangu?” yule mwanadada alimuuliza Amata huku tayari akiongozana nae kumsindikiza, mara simu ya yule mwanadada ikaita, “Yes Boss…” aliitika, sauti ya upande wa pili ilisikika vizuri masikioni mwa Amata japo ilikuwa ndogo, “Nakupa usiku huu tu ukamstareheshe Kamanda, maana ana msongo wa mawazo, kisha urudi kabla jua alijachomoza,”

“Sawa boss, umesomeka,” alijibu kisha akamwangalia Amata, “Leo mimi na wewe mpaka kuchee, boss ameruhusu,” kisha akamshika mkono Amata na kujichnganya nae katikati ya watu ndani ya casino ile…

˜˜˜

Nyimbo za masifu ya jioni zilikuwa zikirindima katika masikio ya walio jirani na eneo hilo la kanisa la Holy Family, masista waliokuwa kanisani mida hiyo walikuwa wakimalizia sala zao za jioni kabla ya kwenda kulala, kusubiri siku inayofuatia, ikiwa ni siku chache tu tangua mazishi ya Fr Gichuru yamalizike, bado mioyo yao ilikuwa imejawa na huzuni ukizingatia kwao kasisi huyo alikuwa ni mtu wa pekee sana, mwenye karama ya uponyaji ya hali ya juu, mpole, mcheshi, mwenye upendo na mcha Mungu.

Ibada ilimalizika na watawa hao wa kike walianza kutoka kuelekea nyumbani kwao, nyumba iliyo umbali wa kama mita mia mbili kutoka kanisa hilo, taa za nje zenye mwanga wa njano zilipendezesha eneo hilo, maua na miti michache ilifanya kabaridi kawe kakali kiasi. Masista wote walimalizika isipokuwa sista Rose ambaye alikuwa akimalizia kupanga vitu vya ibada itakayofuatia, kisha afunge sakristia. Haikumchukua muda alimaliza na kujianda kutoka ndani ya jengo hilo ili akaungane na wenzake. Alipoukaribia mlango tu alijikuta akibanwa na mkono wenye nguvu, uliombana barabara katika shingo yake hata akajikuta anakosa pumzi na mwili wake kukosa nguvu, mkono ule ulilegezwa kidogo na kumruhusu sista Rose kuweza kufurukuta kidogo, akataka kupiga kelele lakini alibadili mawazo ghafla baada ya kukutana na bisu kubwa na kali lililoshikwa na mkono wa mwanamke, Mellina alimkazia macho mwanamke mwenzake kana kwamba anamwangalia kuku au sungura.

“Monstrance! Onesha haraka iliko,” ilikuwa sauti ya Mellina ikimtoka huku mkononi bado kalishikilia lile jisu lake tena akiwa kalinyooshea kwa sista Rose. Ilikuwa ni wakati mgumu sana kwa mtawa yule wa kike, hakuwa na ujanja, hatari zote zilimkabiri, “Tuoneshe ilipo monstrance, tunaitaka monstrance sasa hivi, ukileta ujuaji nakutumbua na hili bisu,” Mellina alimwambia Sista Rose huku akiwa bisu lake kaliegesha nchaye katika ziwa moja la mtawa yule aliyekuwa akitetemeka kwa hofu kuu huku akilisukuma kama anayetaka kutoboa.

“Utaonesha au tukumalize kama yule kasisi wenu? Maana na ye alikuwa mbishi kama wewe” Cheetah alimuuliza kutoka nyuma yake, ndipo yule sista akajua kuwa aliyemkaba alikuwa ni mwanaume. “Ni ni nitawaonesha!” alijibu yule sista. Kisha wote kwa pamoja wakaongozana kuelekea milango mingine iliyotengenezwa vizuri kabisa ndani ya vyumba hivo vya kanisa hilo kubwa. Baada ya kupita milango kadhaa mara waliteremka ngazi kuelekea chini na huko walikuta stoo kubwa lakininzuri yenye vitu vingi tena vya thamani kubwa, sista Rose akawaonesha kabati moja kubwa lililofungwa ukutani, Mellina akaliendea na kufungua milango yake, “Waoh!” alijisemea kwa sauti ambayo kila mmoja alisiikia. “Nini Mellina?” Cheetah aliuliza, alipokaza macho yake alishuhudia monstrance kubwa ya dhahabu safi ikiwa imetulia kabatini, akamuacha yule mtawa na kuliendea kabati akainyanyua ile monstrance kwa umakini wa hali ya juu na kuiweka mikononi mwake, kisha kwenye begi walilokuja nalo maalumu kwa kazi hiyo. Sista Rose alikuwa akitetemeka sana akiangalia walivyokuwa wanaichuku bila heshima yoyote kwa chombo hicho kitakatifu.

“Tafadhali muiache hiyo monstrance,” sista Rose aliwasihi Cheetah na Mellina.

“Acha ujinga wako,” alijibiwa na mellina huku akipata pigo moja la ubapa wa kile kisu kikubwa. Sista Rose akabaki kimya huku machozi yakimtoka baada ya pigo lile, walipohakikisha wameiweka sawa katika begi lile la ngozi, Cheetah akalibeba na kumtazama sista Rose, akacheka cheko la dharau, “Kazi yetu imekwisha, kwa heri msalimie paroko,” Cheetah alimwambia sista Rose huku akimpita na kuuelekea mlango waliouingilia. Pigo moja la judo lilitua mwilini mwa sista Rose, akapepesuka, kabla hajajitambua, mellina akampa pigo lingine lililompoteza akili na kumbwaga chini kama mzigo, kisha guu nene la Mellina lilikanyaga koromeo la sista yule kwa sekunde kadhaa likimkandamiza chini na kumfanya kurusharusha miguu na mikono huku na kule na kuzimika. Ilikuwa tabu kuujua mlango waliongilia, kila walipoufungua huu walijikuta eneo lingine kabisa, walipojaribu huu hali ilikuwa ileile, Cheetah alionekana kuchanganyikiwa maana alipoingia aliona milango michache lakini sasa anaona milango mingi kuliko ile ya kwanza, iliwachukua dakika nyingi kuutafuta mlango ule bila mafanikio.

˜˜˜

Melchior Ndege, aliendelea kupepesa macho yake maangavu ndani ya casino lile lililosheheni watu wa kila aina, muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu walivyoongezeka ndani yake, alihakikisha hampotezi Amata machoni pake, na liona wazi jinsi alivyokuwa amegandwa na mwanadada yule. Melchior alijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi amekwisha wahi kumuona yule mwanadada lakini jibu hakulipata kirahisi japokuwa sura ilikuwa ikimjia.

Alimuona Kamanda Amata akiwa anakunywa kinyaji kikali huku mwanamke yule akiwa pembeni yake na akionekana kumhamasisha, mara amsike kiunoni mara ambusu mara ampapase hapa na pale, kisha aliwaona wakikokotana kutoka nje ya casino ile.

Melchior alishusha glass yake taratibu na kuiweka katia meza ya kaunta kisha akateremka kutoka katika kile kiti kirefu na kuuendea mlango wa casino kutoka nje, akachukua bastola zake pale mlangoni nakuiendea lift iliyompandisha hadi juu na kutoka mlango mkubwa wa hoteli. Katika maegesho ya magari alimuona Amata akiwa na yule mwanamke, sasa ilionekana wazi kuwa mapenzi yanachukua nafasi yake, akajifanya anapiga simu, ili kupoteza muda ajue kitachoendelea.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni