MAUAJI YA KASISI (14)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
“Uuuuhhhhh!!!!” akashusha pumzi nzito kwa mara nyingine, akajilaza kitandani kwake huku mawazo lukuki yakiwa yamemtawala kichwani mwake. Akafikiri la kufanya na kumpigia daktari wao pale Muhimbili, ushauri aliopewa aliuona una maana sana, yule daktari alimshauri ikodiwe ndege ya haraka kutoka Nairobi imlete Dar, badala ya kukodi kutoka Dar.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI

ENDELEA...
Utaratibu ukaandaliwa haraka kwa ushirikiano na Bwana Shikuku kule Kenya. Usingizi haukuja tena kwa Madam S, akaifungua kompyuta yake ya kazini ambayo imeunganishwa moja kwa moja katika kitanda chake, alipojaribu kuingiza password yake, ikagoma, haikufunguhka, akajaribu tena na tena, wapi. Alipoona imeshindikana, akampigia simu Chiba, mtaalamu wa ICT wa kitengo chao, naye akajaribu kuifungua lakini ikawa ngumu, akatumia mbinu zote kuitafuta maana alishajua kuwa wajanja wameiiba kimtandao, na kwa maana hiyo siri zote za usalama wa Tanzania ziko hatarini kuvuja, kijasho kilimtoka Chiba, usingizi ulikatika, akiwa mezani kwake alikuwa akishindana na mtandao kuloitatua tatizo hilo huku Madam S akimuahidi kufika hapo mapema ili kujua kulikoni.

Majibu yalikuja na kugundua kuwa kompyuta ya Madam S imekuwa ‘Hiked’ sehemu Fulani huko Nairobi, mchezo ukaanza kunoga, sasa mapigano ya kimtandao, Chiba hakukubali, alifanya juu chini kuinusuru, ‘Kamanda Amata wanataka kumuua na mtandao wanataka kuukamata, shiit,” alijiwazia kisha akaiacha kompyuta yake na kuelekea kwenye kabati lake, akavaa nguo haraka haraka na kuibeba ile kompyuta kisha kuchukua gari yake haraka akawahi katika ofisi ya mawasiliano ya Usalamawa Taifa, pale kuna kompyuta kubwa zaidi inayoweza kujua vizuri sana, ni wapi na ni nani aliyefanya hivyo, haikuchukua muda aliinasa, na kuifunga kabisa kwa namba ambazo mwingine asingeweza kuzifungua. Akasimama na kumtazama kijana aliyekuwa akisaidiana naye kazi hiyo, Man’sai.

“Dah, hatujui ni kiasi gani wamepata siri zetu,” Chiba alimueleza Man’sai aliyekuwa kasimama karibu na meza kubwa yenye screen kubwa sana ya kompyuta inayoweza kuzileta kompyuta nyingi za ulimwenguni na kutafuta kila wanachokitaka.

“Sasa Bro, cha kufanya ni kiunguza kabisa hiyo kompyuta yao waliyotumia kutu ‘hike’,” Man’sai alisema.

“Tutafanyaje, maana inabidi tupate code namba ya BIOS,” Chiba alisema

“Ah no, siku hizi huwezi kuua kompyuta kwa kuiharibu BIOS maana technolojia imepanda kaka, Operating System za sasa zina uwezo wa kutest kila hardware na software zilizopo katika kompyuta bila kupitia kwenye BIOS, cha kufanya hapa tuondoe taarifa zetu kisha mi nitaweka kirusi kibaya sana kwa jina la faili moja, najua kwa vyovyote watafungua tena, maana kwa sasa wanaonekana wapo offline, kisha huyo kirusi atavuruga system yote ya kompyuta yao,” Man’sai alijibu kwa kujiamini, kijana mwenye elimu ya ICT kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.

“Ok, fanya hivyo wakati mi nafanya mengine,” Chiba alimalizia. Kijana Man’sai alikaa makini kwenye laptop yake akitengeneza shetani hilo alilolipa jina TOP SECRET, kazi iliyochukuwa kama lisaa limoja hivi na kuifanikisha akiwa kachoka sana. Kisha akamwendea Chiba na kumwambia kazi tayari ili apate ruhusa ya kufanya mlipuko huo, akakubaliwa, kazi ndogo, akaingiza kile kirusi kwenye mfumo wa kompyuta ya Madam S na kukiacha hapo, wakati document zingine zote akiwa zimebanwa na Chiba kwa pin ngumu.

˜˜˜

REJEA NAIROBI… kanisa la familia Takatifu…

Ilikuwa ni kazi ngumu kwa Black Cheetah na Mellina kutoka ndani ya wigo wa kanisa maana tayari sergeant Maria na koplo Kariithi walikuwa pale na wengine wanne wenye silaha, walitanda kila upande kuhakikisha majambazi hao hawatoki bila kuacha roho zao.

Gichui, aliyekua akiendesha gari siku hiyo aliwapa taarifa kwa simu kuwa jamaa wamejipanga vipi huko nje, wakamuamuru, aanzishe show kwa kupiga risasi za hewani. Naye akafanya hivyo, mlio wa risasi zile ukawafanya wale askari kuchanganyikiwa kidogo, Black Cheetah alitoka katika mlango mkubwa akiwa na lile begi na kukimbilia upande wa pili wa ukuta huo ambako ndiko waliokoingilia, huku Mellina akitambaa mwendo wa nyoka kulifuata geti kubwa akiwa na bastola yake aina ya revolver mkononi mwake.

Gichui alipiga norinda na kutimua vumbi liliwachanganya Mellina na Kariithi ambao walikuwa tayari kujibu mashambulizi, Sargeant Mellina alijitupa chini na kubingirika kwa usatadi mpaka kwenye ukuta wa wigo wa kanisa hilo huku akishuhudia vijana wake wakijiweka tayari, “Freeze!!!!!!” sauti ya askari mmoja lisikika upande wa pili, Kariithi bado alikuwa akijaribu kuona afanye nini, akajitoa na kukimbilia upande wa sauti ile ilipotokea, akiwa anakata kona ya ule ukuta alisikia mlio wa risasi na kushuhudia mwili wa yule askari ukijibwaga chini kama kiroba,

“Shiittt!” akng’aka kwa hasira, alimuona Cheetah, aliyeifanya kazi hiyo akiishia gizani, akajaribu kulenga na kufyatua risasi mbili lakini hakumpata, mara ile gari yao ilipita kwa kasi na kuelekea upande ule alipo Cheetah, haikuhitaji kusimama, kawani Cheeta alirusha begi ndani ya gari na kujirusha kupitia dirishani, lakini kabla hajamalizi miguu risasi moja ilipita katikati ya mguu wake na kufumua mifupa ya ugoko, Gichui aliizungusha gari kwa ustadi na kumfanya Cheetah kutumbukia ndani, “Aaaaaaaaiiiiggggghhhhhh!!!!” ulikuwa ukelele wa maumivu kutoka kwa Cheetah.

“Vipi brother?” Gichui aliuliza huku akiizungusha tena ile gari na kumgonga askari mwingine, sasa alikuwa akilielekea geti kuu la kanisa lile.

“They have shot me, bastards!” wamenipiga wanaharamu alimwambia Gichui, huku akiiweka tayari bastola yake. Sergeant Maria akiwa pale chini aliilenga sawia ile gari na kabla hajapiga risasi alihisi kama kitu kimenguka pale alipolala kwa nyuma yake alipogeuka aliona mwanamke kibonge akitua juu ardhi kavu na bastola mkononi, akiwa pale chini alijigeuza na kupiga mtama mmoja maridadi, Mellina alilipokea pigo hilo na kubwagwa chini, alijitahidi kujiinua kisarakasi lakini kabla hajawa wima mtama mwingine wa Mellina ulimrudisha chini na kumfanya hoi pale ardhini, sasa alishindwa kujiiunua. Bastola ya Mellina ilicheua na risasi ikapita mililmita chache kwenye uso wa Maria aliyekuwa pale chini, teke moja kali la afande Maria lilipeperusha bastola ile kutoka mikono ya Mellina ikapaa juu, kisha aliushusha mguu wake na kuutuza juu ya uso wa Mellina.

Koplo Kariithi alijitoa mhanga na kucukua ile SMG ya askari ambaye aliku marehemu, kuilenga gari ya Gichui, ‘nice shot’ risasi moja alipiga tairi ya nyuma na kuipotezea muelekeo ile gari, ikayumba na kuyumba lakini ikakaa tena barabarani, risasi ya pili kutoka kwa Kariithi ikakishusha kioo cha nyuma na bila kukosea ikafumua kisogo cha Gichui na ile gari ikayumba myumbo mkuu na kugonga mti.

Wakati Kariithi akiifuta, ghafla nyuma yake kulitokea gari aina ya BMW kwa kasi ya ajabu ikafunga breki kali karibu kabisa na ule mti ilipogonga ile gari ya Gichui, kwa haraka watu wawili walishuka na kuifungua milango wakamtoa Cheetah na kulibeba begi kisha kurudi ndani, ile gari nayo ikazungushwa kwa mtindo wa U turn na risasi moja iliyotoka ndani ya gari ile ilimpata koplo kariithi mkononi, ukelele wa maumivu ulimchanganya sergeant Maria, akamsahau Mellina na kumkimbilia Kariithi, “Soldier!!!” Askari, sergeant Maria aliita kwa sauti na askari wote wakaja eneo hilo na kumbeba mwenzao wakimpakia kwenye gari, wengine wakabaki kufanya utaratibu wa kumuondoa Gichui ambaye alikuwa hana maisha tena na kichwa chake kikiwa kimevurugika kwa risasi ya Kariithi, moja kwa moja walimfikisha katika hospitali ya taifa ya Nairobi.

5

MADAM S alisimama kwenye mlango maalum wa kioo akimtazama Kamanda Amata aliyekuwa amelala kitandani akiwa ndani ya mitambotiba, sasa alikuwa ameamka baada ya kazi kubwa ya daktari wa muhimbili ya kumtoa sumu mwilini, alifumbua macho, aliweza kuongea japo kwa shida, alikutana macho na bosi wake, akamtazama, “Karibu Nairobi Madam,” Kamanda alimkaribisha madam S.

“Aliyekwambia hapa Nairobi ni nani?” Madam alimuuliza Kamanda.

“What?” akajiinua na kuketi, “Niko wapi?” akauliza.

“Upo Muhimbili, karibu sana Dar es salaam, Kamanda umefanya mambo ya kijinga sana Kamanda, siwezi kukuvumilia hata kidogo, tumekaa kikao na kuona kukutoa wewe katika cheo chako cha TSA 1 na kumpa mtu mwingine,” Madam S akameza mate, “Kila mara nakuonya na wanawake wako hutaki kunisikia, kwa nini? Sasa wlitaka kukuua, mshukuru bwana Shikuku na kijana wake Ndege, ulikuwa marehemu tayari, na sasa tungekuwa tunautafuta mwili wako.

Kamanda huna maana tena kwetu na kwa serikali kwa ujumla, tunaandaa utaratibu wa kukustahafisha hasa kwa uzembe unaouonesha, unajua wewe ni kama roho ya serikali, wakikubana wewe watakuwa wamepata kila kitu, kila siri, na sumu waliyokupa si ajabu imekufanya utoe siri nyingi bila kujijua.” Madam akageuka na kuondoka zake na kufunga milango nyuma yake, Kamanda Amata akabaki kajiinamia kisha akajitupa kitandani kwa hasira, “Biiiiiillllllllllllllll !!!!!!!” alipiga ukelele wa nguvu kisha akapoteza fahamu…

Ilikuwa ni zamu ya madaktari na wauguzi kuhakikisha wanaokoa maisha ya Kamanda Amata katika dakika hizo, haikuwa rahisi maana ilionekana mapigo ya moyo yakishuka zaidi, walijaribu mbinu zote za kitaalamu lakini bado hali ilikuwa tete, baada ya kuhangaika kwa muda refu, kidogo hali yake ilianza kurudi na mapigo ya moyo yalirejea kwenye hali ya kawaida ingawaje bado alikuwa katika usingizi mzito uliogubikwa na taswira ya Bill kama mtu wa kutisha na hatari, aliyetaka kuyakatisha maisha ya Kamanda kwa mtindo ambao hakuutegemea, wauguzi na madaktari walishusha pumzi wakiwa wamekizunguka kitanda cha Amata, walifarijika zaidi walipomshuhudia akiwa amefumbua macho akiwaangalia mmoja baada ya mwingine, “Kuna nini?” aliuliza, “Mbona mmenizunguka hivyo?”

“Kamanda! Ulikuwa katika hali mbaya sana, kiasi kwamba bila jitihada za hawa wote tungekukosa,” Daktari alimueleza akiwa amemuinamia. Ilikuwa kama hali ya mshangao kwa Amata, alijitazama kama mtu aliyerukwa na akili, “Yuko wapi Bill?” aliuliza. “Bill?! Bill ni nani?” aliulizwa na daktari, Amata alizungusha shingo yake na kuona wauguzi tu na madaktari, akajilaza kitandani kwa mara nyingine. “Ok, tumuache apumzike sasa,” ilikuwa ni kauli ya daktari akiwaambia wale wauguzi pamoja na wasaidizi wake, wote wakakiacha kile chumba na kurudi katika idara zao. Akili ya Kamanda Amata haikutulia, muda wote ilimuwaza Bill, hasira zikaanza kuuteka moyo wake, maneno ya Madam S yakamvunja nguvu,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni