MAUAJI YA KASISI (16)

Zephiline F Ezekiel
MAUAJI YA KASISI (16)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA SITA ILIPOISHIA... “Kuna kazi nyingine anafanya huko mjini,” alipojibu hayo mara simu yake ya mkononi ikaita kutoka katika mfuko wa jeans, Amata akainyakuwa na kusoma jina lililopo hapo juu ‘ Moriyo ’, “Moriyo ndo nani?” Amata aliuliza tena. “Ni mwenzangu yuko hapo chini ananisubiri, tumeambiwa tupeleke haraka hilo begi,” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kamanda Amata hakupenda kupoteza muda, alimuwekea ile bastola katika sikio lake la kuume, “Usiniue kaka, nina watoto mimi watalelewa na nani?” alilia kwa uchungu. “Ungekuwa na watoto unaowajali, ungefanya kazi za kishetani kama hizi, sikuui lakini lazima uwe mlemavu ili siku zote za maisha yako umkumbuke Kamanda Amata,” alipotamka jina hilo, akamuona Yule jamaa akishituka na kuguna kama aliyekutana na jinamizi. “Umesema we nani?” aliliza hata akawa amesahau kama ana jeraha baya la risasi katika…