USIKU WA BALAA (2)

Zephiline F Ezekiel
USIKU WA BALAA (2)
Jina: USIKU WA BALAA Mtunzi: Kalmas Konzo SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Rose aliongea huku akionesha wazi ya kwamba alikuwa na hofu. "Kimejiri nini kwani Rose?". Ilinibidi minwulize Rose baada ya kuyasikia maneno yake. "Ndoo imepasuka". Rose aliongea huku akionesha dhahiri alikosa raha. KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI 👉 GUSA INSTALL 👈 ENDELEA... Habari ile hata mimi ilinitisha kidogo. Nilijua swala lile litaleta matatizo makubwa sana nyumbani kwa akina Rose. Sasa nitafamyaje? Ni swali ambalo nilijiuliza na lilikosa majibu ya papo kwa papo. Ghafla nikapata wazo ambalo nililiona ni jema sana. Nikaona hapo sasa nimekwishalitatua lile tatizo. Nilienda ndani mwangu na kurudi na ndoo ambayo ilikuwa ni ya aina na rangi za ile iliyovunjika. Nikaenda bombani na kuiikinga maji. "Haya njoo nikutwike mama". Nilimwambia Rose huku nikitabasamu. "Mwone kwanza, sasa hivi siuhitaji msaada wako. Najitwika mimi …