USIKU WA BALAA (5)

Zephiline F Ezekiel
USIKU WA BALAA (5)
Jina: USIKU WA BALAA Mtunzi: Kalmas Konzo SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... “Sasa Meselina mimi naona bora nikuache niwahi kazini”. Nilimuaga Meselina. “Hapana huwezi kuondoka hivihivi Ima . Ngoja upate juisi ya baridi ili ulitulize hili joto kali la hapa Kano ”. “Hapana Mese, nitakunywa siku nyingine”. Nilisisitiza nikihofia kuchelewa kurudi kazini. KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI 👉 GUSA INSTALL 👈 ENDELEA... “No! noooo! Ima. Unywe leo”. Mese aliongea huku akiwa amenikata jicho moja ambalo lilikuwa kubwa na limelegea ambalo lilinifanya nisalimu amri kabisa na kuketi tena juu ya sofa. Wakati huohuo Meselina alikuwa amekwenda katika friji na kuchukua bilauri na kulileta mezani. Kisha akaenda kabatini na kuchukua glasi na kuja nayo pale mezani kisha akamimina juisi na kunikabidhi. Naye pia akajimiminia katika glasi yake kisha tukagonga chiazi na kuanza kuzinywa. “Ima nisubiri kidogo, naja sasa hivi”. “Ok Meselina, wala usijali”. Meseli…