USIKU WA BALAA (6)
Jina: USIKU WA BALAA Mtunzi: Kalmas Konzo SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Nilipogeuka nilitamani kuzimia kwa kila macho yangu yalichokishuhudia. Mwili wangu ulikuwa umeshikwa ganzi na kuufanya ushindwe kujongea zaidi. Mbele yangu alikuwa amesimama Rose yule binti mrembo wa kazi nyumbani kwa mzee Mwaitambo kule ambako lilinikuta balaa la kufumaniwa na mrembo Nancy na kunisababisha niuhame mtaa kwa aibu. KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI 👉 GUSA INSTALL 👈 ENDELEA... Mgongoni alikuwa amembeba mtoto mdogo kabisa ambaye alinipa maswali kidogo kichwani. “Rose!”. Niliongea kwa staajabu iliyochanganyika na aibu. “Ndiyo mimi Ima . Unachokishangaa kwangu ni nini hasa?’. Nilipigwa swali. “Huyo mtoto ni nani?”. Nilimbandika swali hilo Rose. “Huyu ni matokeo ya mahusiano yetu ya kimapaenzi”. Rose alinijibu kwa mkato huku akiwa amejawa na hasira kali sana. “Ina maana huyu ni mwanangu?”. Nilimwuliza tena Rose. “Ina maana majibu yangu huyaelewi Ima?…