MY EVA (2)

Zephiline F Ezekiel
MY EVA (2)
JINA: MY EVA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Danny: baba mbona umekua hivyo? Kuna nini? Victor: aaah...mimi...ha..hamna kitu hata. Danny, Eva, na mama yake danny (rachel) walibaki wakimshangaa victor. SASA ENDELEA... Rachel alimwangalia mmewe kwa macho ya wasiwasi lakini victor alivunga kutabasamu maisha yaende. Rachel alijua tu hiyo tabasamu ni ya funika kombe mwanaharamu apite lakini hakutaka kua msumbufu...alimtegeshea victor wafike nyumbani ili amweleze vizuri. Wakiwa kwenye gari victor alikua na mawazo mengi sana juu ya ukaribu wa eva na danny. Jambo hili lilimuumiza sana kichwa.aliwaza kama danny ameshajenga ukaribu mkubwa kiasi kile na eva itakuaje wakati familia zao ni maadui wakubwa?..itakuaje siku siri ikivuja?. Victor akiwa katika mawazo mengi alishtuliwa na mke wake rachel. Rachel: baba danny, nini tatizo? Mbona unaonekana una mawazo mengi? Victor: aaah..hapana mke wangu...hamna kitu hata. Rachel: una maana gani kusema hamna kitu wakati unaonekana kabisa kuna kitu ki…