
JINA: MY EVA
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Danny: baba mbona umekua hivyo? Kuna nini?Victor: aaah...mimi...ha..hamna kitu hata.
Danny, Eva, na mama yake danny (rachel) walibaki wakimshangaa victor.
SASA ENDELEA...
Rachel alimwangalia mmewe kwa macho ya wasiwasi lakini victor alivunga kutabasamu maisha yaende.Rachel alijua tu hiyo tabasamu ni ya funika kombe mwanaharamu apite lakini hakutaka kua msumbufu...alimtegeshea victor wafike nyumbani ili amweleze vizuri.
Wakiwa kwenye gari victor alikua na mawazo mengi sana juu ya ukaribu wa eva na danny. Jambo hili lilimuumiza sana kichwa.aliwaza kama danny ameshajenga ukaribu mkubwa kiasi kile na eva itakuaje wakati familia zao ni maadui wakubwa?..itakuaje siku siri ikivuja?.
Victor akiwa katika mawazo mengi alishtuliwa na mke wake rachel.
Rachel: baba danny, nini tatizo? Mbona unaonekana una mawazo mengi?
Victor: aaah..hapana mke wangu...hamna kitu hata.
Rachel: una maana gani kusema hamna kitu wakati unaonekana kabisa kuna kitu kinakusumbua?..tangu ulipomwona Eva umebadilika sura na mawazo..halafu unaniambia hamna kitu!!...kweli!!!... Usiponiambia mimi utamwambia nani basi?
Victor aliishiwa pozi na ujanja ikabidi aseme:mama danny, usiwe na haraka..nitakueleza kila kitu tukifika nyumbani.. Wala usijali.
Rachel: hapo sawa umenena..sio kunidanganya hamna kitu.
Victor: jamani wewe mwanamke unakaba hadi penalt..duuh...alisema victor na wote wakacheka.
Huku danny na Eva walikua wakipiga story mbili tatu Baada ya wazazi wa danny kuondoka.
Danny: Eva, unajua nimekaa na wewe siku zote hizo hata sijui habari za wazazi wako na sijawahi hata kukuuliza!!... Hadi nahisi aibu...hebu niambie ilikuaje.
Eva alivuta kumbukumbu kisha akasema: ilikua mida ya saa sita usiku hivi ambapo baba na mama walikua wamelala.mimi na mfanyakazi wetu tulikua chumbani tukiangalia TV kwa siri maana mama alikua ameshatuamuru tukalale..tena hasa mimi.
Mara nikasikia vishindo ndani ya nyumba yetu vya mtu kama ananyata..nilitoka kuchungulia ni nani..nilihisi labda ni mama ametusikia tunaangalia TV.
Sikua mwoga enzi hizo..nilitoka hadi nje kabisa ya nyumba na kuangakia kinachoendelea..mara nilipotoka tu ghafla niliona nyumba yetu inawaka moto ghafla halafu yote kwa pamoja
Nilianza kupiga kelele za kuomba msaada na ndani ya dakika chache majirani walikua wameshafika.
Nililia sana nikiwasii wawaokoe wazazi wangu na bila ya kuchelewa waliita zima moto..
Nilitamani kuingia ndani niwaokoe wazazi wangu au hata nife pamoja nao lakin haikuwezekana maana sikua na huo uwezo wa kuwaokoa halafu hata hivyo watu waliokua pale walinishikilia nisiende popote.
Kwakua zima moto walichelewa,basi wazazi wangu na mfanyakazi wetu walikufa wote kwa moto ule
eva alishindwa kuendelea na alikua akitokwa machozi mengi huku akilia kwa kwikwi.
Danny alimwangalia kwa huruma sana akamshika na kumwegemeza kwenye bega lake na kumfuta machozi kwa kutumia kitambaa alichokua nacho.
Baada ya kimya kifupi danny aliulza: kwahyo sasa hivi unaishi na nani?
Eva: kwa sasa naishi na shangaz yangu ambae alinichukua baada ya wazazi wangu wote kufariki.maisha yetu ni magumu ingawa ni ya furaha na amani maana shangazi yangu ananipenda sana.. Ila shangaz ya ni mgonjwa wa moyo maskini wa mungu.
Danny:kwani nani anae kusomesha?ni shangaz?
Eva:sio shangaz, ni rafiki yake mama ndie anaenisomesha ingawa naishi na shangazi na ndio maana niko kwenye shule ya gharama kiasi hiki.baada ya baba na mama yangu kufariki ndugu zake walichukua mali zote na kuniacha mtupu kwa kisingizio kwamba wanazisimamia na watanilea kwa kutumia hizo.
Shangaz yangu alinichukua na kunilea..pale nilipokua nakwama,shangaz aliwapigia hao waliochukua mali za wazazi wangu ili wanisaidie lakin walimkaripia sana na hakuna alienijali tofauti na shangazi.
Danny alimwangalia eva kwa huruma sana na kisha akasema:pole sana eva, daah,sikujua kama una historia ya kuumiza kiasi hiki
Eva: asante danny, tangu nikufahamu wewe nina furaha sana danny...alisema eva huku akimwangalia danny.. Wote walitabasamu ..Lakin kuna kitu hua bado nawaza.
Danny: kipi hicho?
Eva: kifo cha wazazi wangu haikua ajari kama wengi wanavyoamini...kuna mtu alichoma nyumba.
Danny: kwanini unawaza hivyo?
Eva: kwanza vile vishindo nilivyosikia,pili kipindi nyumba inaungua kuna mtu alitoka nje amevaa kinyago na kupitia mlango wa pembeni...alipokua akitoka alichanwa na msumari kwenye bega lake la kushoto ....niliposema oneni kuna mtu pale,mtu huyo alikimbia.
Watu walipoangalia hawakumkuta wakajua ni sababu tu mimi nilikua nimechanganyikiwa muda huo na hakukua na mtu.lakin kiukweli alikua mtu.. Na ule msumari ulimchana sana na kovu lake nahisi litakua la mviringo flani hivi.
Eva alisema haya asijue kua anaemwongelea alikua victor
Danny:mmmh..pole sana eva, pole sana.
Eva: asante danny.
Danny: eva,nitahakikisha huyo muuaji anapatikana na anapelekwa kwenye sheria..nakuahidi eva... Alisema danny asijue kua ni baba yake mzazi. Je nini kinafuata?