MY EVA (3)
JINA: MY EVA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Danny: eva, nitahakikisha huyo muuaji anapatikana na anapelekwa kwenye sheria..alisema danny bila kujua ni baba yak mzazi. SASA ENDELEA.. Eva:Nilishawahi kumwambia shangaz kuhusu huyo mtu lakin alisema kua niachane na hayo mambo maana hakuna nitakachobadili. Waliongea mda mrefu sana na baada ya maongezi kila mtu alikwenda bwenini kwao. Victor na mkewe rachel walifika nyumbani salama salmini. Baada ya chakula na mapumziko mafupi walikwenda kulala.walipokua chumbani rachel alianza kumuuliza victor tatizo ni nini. Rachel:haya baba danny niambie,nini kimekusibu mme wangu hadi unakosa raha kiasi hicho? Victor:mama danny Rachel: abeee. Victor: huu urafiki wa danny na huyo eva naomba tuukatishe haraka sana kwa gharama yoyote ile. Rachel:mmmh...kwanini mme wangu? Victor: yule binti mimi namfahamu vizur sana.anaishi na shangaz yake na ni yatima.familia yao ni watu hatari sana.halafu kwanza istoshe sio wa hadhi ya danny..ni maskini sana yule. Rac…