MY EVA (3)

0
JINA: MY EVA
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Danny: eva, nitahakikisha huyo muuaji anapatikana na anapelekwa kwenye sheria..alisema danny bila kujua ni baba yak mzazi.

SASA ENDELEA..
Eva:Nilishawahi kumwambia shangaz kuhusu huyo mtu lakin alisema kua niachane na hayo mambo maana hakuna nitakachobadili.

Waliongea mda mrefu sana na baada ya maongezi kila mtu alikwenda bwenini kwao.

Victor na mkewe rachel walifika nyumbani salama salmini.
Baada ya chakula na mapumziko mafupi walikwenda kulala.walipokua chumbani rachel alianza kumuuliza victor tatizo ni nini.

Rachel:haya baba danny niambie,nini kimekusibu mme wangu hadi unakosa raha kiasi hicho?

Victor:mama danny

Rachel: abeee.

Victor: huu urafiki wa danny na huyo eva naomba tuukatishe haraka sana kwa gharama yoyote ile.

Rachel:mmmh...kwanini mme wangu?

Victor: yule binti mimi namfahamu vizur sana.anaishi na shangaz yake na ni yatima.familia yao ni watu hatari sana.halafu kwanza istoshe sio wa hadhi ya danny..ni maskini sana yule.

Rachel:sasa kama ni maskini anasomaje shule ya gharana kiasi kile?

Victor: baada ya wazazi wake kufariki alijitokeza msamalia mmoja ambae alikua rafiki wa mama yake akamsomesha hadi hapo alipo..shangaz yake yule hana kitu.hapo kila kitu wanamtegemea huyo msamalia...huyo msamalia akikwama tu hawana chao labda wakaombeombe kwa watu.

Rachel:Mmmh,kama ni hivyo kwakwel bora huo urafiki ukome tu maana Danny atakuaje na rafiki wa namna hiyo? Hatutaki maombaomba sisi kwenye familia yetu.

Victor: kweli kabisa inabidi tufanye mpango wa haraka.

Rachel: lakin umesema kwamba familia yao sio watu wazuri..una maana gani kwenye hili?

Victor:ni wachawi wakubwa wale,ndio waliowauwa wazazi wote wa eva.hebu fikiria mtu kama huyo awe rafiki wa danny, si atatumalizia mtoto wetu...alisema victor huku akijua kabisa kua sio kweli hata chembe.

Rachel: heee...kama ni hivyo basi bora huo urafiki ufe kabisaa..mtoto mwenyewe huyu mmoja tu kama jicho halafu akaangukie mikononi mwa wachawi na sisi turuhusu!!..haiwezekani..alisema rachel kwa msisitizo.

Lakin baba Danny...

Victor: naam

Rachel: ila mimi sioni kama kuna ulazima kivile kuwatenganisha maana urafiki wao ni wa kawaida tu..baada ya shule kila mtu anajua yake.

Victor: hapana!!....hapana kabisa...kwa jinsi nilivyowaona sizani kama kuna urafiki wa kawaida hapo..hata kama hawajakubaliana ila wanapendana hao.sitakubali hata kidogo mwanangu awe na mtu kama yule.. Anamshusha hadhi bwana.

Rachel: basi sawa nitahakikisha wanaachana kwa vyovyote vile,huyo eva asije akatuchafulia ukoo.

Huku shuleni,mapenzi kati ya Eva na danny yalizidi kukolea.kadri siku zilovyoenda ndipo hawa viumbe walizidi kupendana sana.

Siku moja ilikua ni siku ya kuzaliwa ya Eva.
Siku hiyo Eva alikwenda darasani na kukaa kwenye kichake ajisomee.
Alipogeuza macho kuangalia sehem ambayo danny hua anakaa kujisomea hakumwona.

Siku hiyo danny alichelewa sana night prepo (muda binafsi wa kujisomea wa usiku)

Eva alizoea kumkuta danny kila siku akiwa ameshafika darasani lakini siku hiyo ilikua tofaut sana maana Danny alichelewa sana.

Eva alikosa raha baada ya kuona danny hafiki.alikua ameshamzoea sana.alikua akijaribu kusoma havisomeki,anajaribu tena lakini wapi... Shida yake ilikua ni kumwona danny tu..akimwona tu basi mambo shwari.

Akiwa anaangaza huku na kule kuona kama danny anakuja mara danny aliingia.Eva alipata amani ya moyo ghafla baada ya kumwona danny.. Sura yake nzuri ikajaa tabasamu.

Danny aliingia kwa pupa na kufikia kukaa kwenye kiti karibu na eva huku anahema kama mtu alienusurika kifo.

Eva:we danny.

Danny: Naaaaaaaam...aliitika danny kwa masihara.

Eva:mbona unahema kiasi hicho kama mwizi anaefukuzwa..kulikoni,umekutana na nini huko?au umemwona mkwe w shetani..alitania eva.

Danny: haha..et mke w shetani...ila wewe nae una mambo.

Eva: sasa je...sasa wewe unakuja unahema kiasi hiki jamani..shida nini kwani?

Danny:nilikua nakimbizwa huko na mlinzi wa shule..ila nimefanikiwa kumkwepa.hapa akija najikausha kama sio mimi vile.

Eva:siku hizi umeendelea..yaani unakimbia hadi unamshinda mlinzi.

Danny: mmmh, sasa yule mara akimbie,mara shuka lake la masai lianguke aokote,atanikamata saangapi sasa?..alisema danny na wote wakacheka.

Eva: lakini umefanya nini hadi ukimbizwe na mlinzi?

Danny hakumjibu eva bali akimgeukia na kumwangalia usoni kama dakika tano hivi bila kukwepesha macho.

Eva:mbona hujibu..unanikodolea tu macho yako hayo ya kurembua rembua kama dem.

Danny alitabasamu lile tabasamu la shavu moja kisha akaanza kumsogelea eva.

nini wewe mbona sikuelewi..alisema eva huku akisogea nyuma nyuma..danny nae alizidi kumsogelea.

Danny:Nimekimbizwa na mlinzi kwa sababu yako wewe hapo..alisema danny akiwa amemsogelea eva..eva alishindwa kusogea nyuma zaid maana alikua ameshafika ukutani..ilibidi atulie tu huku ametumbua macho.

Eva: hee,mimi tena!?..kiaje ukamatwe kwa sababi yangu?.

Danny:ee kwa sababu yako..kwani umesahau leo ni siku gani?..

Eva aliviuta kumbukumbu kisha akasema:aaaaah..leo siku yangu ya kuzaliwa.

Danny alimsogelea eva sikioni kisha akasema :nilitoroka kukununulia zawadi wewe apo.

Eva alilopoka kwa sauti ya juu:ulitoroka?!!!

Danny: shiiiii..ongea taratibu bwana watu wanasoma..alisema danny kisha akatoa kibox flani hiv na kumpa eva kwa chini chini kisha akamwambia akafungulie bwenini.

Eva: asante Danny

Wakiwa wanafanya hivyo vioja Vyote sijui walisahau ku wako darasani!?hata mimi sijui.....mara akasikikika mwanafunzi mmoja anasema:

Aisee baba mchungaji njoo ufungishe ndoa hapa...

Eva na danny walishtuka wote....danny ilibid akae vizur kwenye kiti chake sio kumsogeleasogelea eva.

wanafunzi: heheee...nawaona baba chanja na mama chanja..

Eva aliona aibu akaangalia chini huku danny yeye akivunga mkakamavu ajikajifanya anaendelea kusoma...tena akajikunja ile mbaya🙇.

USIKOSE SEHEMU YA NNE

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)