MY EVA (22)
JINA: MY EVA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI ILIPOISHIA... Mara kazmoto aliingia na kukaa upande wa eva kama shahidi wa eva... Kazmoto!!!!...aliropoka victor bila kujali kua yuko mahakamani... SASA ENDELEA.. Kesi iliendeshwa kwa masaa kazaa..ilipofika zamu ya kazmoto kusimama kama shahid alisimama na kusema kua victor ndie mhusika wa yote... Unaushahidi wowote?...aliuliza hakimu Ndio...ninao. Mda huo victor alikua ana anamwangalia kazmoto...alikua na waswas kazmoto atasema nini.. Haya ulete huo ushahidi....alisema hakim Kwanza kabisa...mimi mwenyewe ndie niliekua nikishirikiana nae hadi hatua ya mwisho ya kuwaua adrian na mkewe.. Watu wote mahakamani walishangaa sana kusikia hivyo.. Umesema mlishirikiana!!??...aliulza hakimu Ndio... Kwahyo na wewe ni mtuhumiwa?.. Ndio.... Eva alimgeukia kazmoto na kuangalia kwa macho yaliyojaa maswali mengi.... Kazmoto alitikisa kichwa aliashiria kukubali aliyoyasema...eva alichoka kabisa... Kazmoto aliwataja hata wale ndugu wa marehem waliohusika Kesi …