MY EVA (22)
Zephiline F Ezekiel
3 min read
JINA: MY EVA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Mara kazmoto aliingia na kukaa upande wa eva kama shahidi wa eva...Kazmoto!!!!...aliropoka victor bila kujali kua yuko mahakamani...
SASA ENDELEA..
Kesi iliendeshwa kwa masaa kazaa..ilipofika zamu ya kazmoto kusimama kama shahid alisimama na kusema kua victor ndie mhusika wa yote...Unaushahidi wowote?...aliuliza hakimu
Ndio...ninao.
Mda huo victor alikua ana anamwangalia kazmoto...alikua na waswas kazmoto atasema nini..
Haya ulete huo ushahidi....alisema hakim
Kwanza kabisa...mimi mwenyewe ndie niliekua nikishirikiana nae hadi hatua ya mwisho ya kuwaua adrian na mkewe..
Watu wote mahakamani walishangaa sana kusikia hivyo..
Umesema mlishirikiana!!??...aliulza hakimu
Ndio...
Kwahyo na wewe ni mtuhumiwa?..
Ndio....
Eva alimgeukia kazmoto na kuangalia kwa macho yaliyojaa maswali mengi....
Kazmoto alitikisa kichwa aliashiria kukubali aliyoyasema...eva alichoka kabisa...
Kazmoto aliwataja hata wale ndugu wa marehem waliohusika
Kesi iliendelea na eva alishinda...watuhumiwa wote walihukumiwa miaka 30 jeka kila mmoja.
Hongera eva... Alisema miriam baada ya eva kushinda kesi..
Nashukuru sana miriam maanankama sio wewe na familia yako nisingefika popote....waliongea mengi sana..
Halaf kumbe kazmoto nae alihusika kweny mauaji...alisema eva
Mmh nan kasema..victor??
Yeye mwenyewe...
Mmmh makubwa..
Yaan hadi nimeishiwa pozi huko mahakamani..alisema eva.
=========*
Victor akiwa amekaa anasubir kupelekwa jela...alikua akijiona mtu wa ajab na kujutia sana aliyoyafanya Kwa eva..akiwa na mawazo mara jaji massawe alikuja...alikua kaja kuangalia kesi ilivyoenda...alikutana na eva na eva akamweleza yote..
Hongera eva...mungu amekusaidia...
Baada ya victor kumuona jaj....alimwita.
Unashida gan victor?
Kuna kitu naomba unisaidie...
Kitu gani hicho?....
Kuna mambo nataka niieleze jamii kabla sijafungwa jela.
Yapi?
Victor alimweleza jaji massawe na jaji alikubali kumsaidia...alimwandalia waandish wa habari.
Eva akiwa njian mara sim yake iliita...alikua ni Danny.
Eva...mama anaomba uje huku nyumbani..alisema danny
Mmmh...haya..alikubali eva huku akiwa na waswasi mkubwa.
Aliahirisha kwenda kwake na akaenda kwao danny.
Alipofika alipokelewa vizur na mama danny.
Walikaa pamoja pale sebuleni na kuongea mengi huku rachel akisisitiza kua eva amsamehe... Wakiwa wamekaa walishangaa kumuona victor kwenye tv...
Mmh...anataka kusema nini victor...alisema rachel.
Victor alianza kusema:
Mimi naitwa victor kama wengi wanavyonifahamu.
Mwaka 1994 nilikua nafanya kazi za kusafirisha madini kwenda nje ya nchi...eneo nililokua nafanya kazi alikuepo bwana mmoja anaitwa adrian...
Siku moja alimshuhudia bossi wangu akimpiga risasi mfanya kazi mwenzetu...bossi alipojua kua adrian amemuona aliniagiza nikamuue ili kupoteza ushaidi..aliniagiza nishirikiane na mfanyakazi mwenzangu ambae ni kazmoto.
Nilipomueleza kuhusu kazi tuliyopewa alikataa, maana adrian alikua shemeji yake...
Nilienda kumweleza bossi kua kazmoto amekataa...boss alimuita na kumtishia kumuua mke na wazaz wake kama akiendelea kukataa....kazmoto hakua na jinsi ilibidi akubali.
Tulipanga kuwauwa kwa kuchoma nyumba yao na kutoroka ili ionekane ni ajali.mimi ndie nilietekeleza huo mpango kwa kushirikiana na ndugu wa marehem waliotaka kurithi mali za ndugu yao...baada ya kuchoma nyumba nikatoweka....adrian na mkewe wote walikufa ila mtoto wao alipona.
Baada ya kumaliza kaz nilimtumia barua kazmin kumtaarifu lakin bahat mbaya ilimfikia mkewe ambae ni dada wa marehem
Baada ya kugundua siri..mke wa kazmoto aliachana na mmewe...
Maria,mke wa kazmoto alimchukua mtoto wa marehem kaka yake baada ya ndugu wa marehem kuchukua mali zote za wazaz wake...alimchukua akamlea...
Na mtoto huyo ni huyu muigizaj maaruf mnaemjua sasa kwa jina la eva( Evalinda Adrian)
Baada ya miaka mingi kupita...mtoto yule alikua akasoma na akaingia kidato cha tano shule moja na mwanangu Danny...
Siku moja tulienda shjule kumtembelea danny (victor alieleza yote tangu mara ya kwanza kumuona eva mpaka leo hii)..
Kwahiyo naomba watu wote mumtue eva laana na na tuhuma zote mlizomtwisha..hata ile tuhuma ya kumuua jamila ni Mimi nilimzushia...
Asilimia tisini ya skendo chafu za nilikua nahusika Mimi.
Eva nakuomba ulipo unisamehe...mke na mwanangu naombeni pia mnisamehe..shabiki wote wa eva pia kama mkiweza naomben mnisamehe....asanteni kwa kuusikiliza upuuzi wangu hadi mwisho...alisema victor na kuondoka kuelekea jela...
Mama!! kumbe ndo nyiniy mlimzushia eva ile skendo?....mnajua kias gani mliyaharibu maisha yake?..
Rachel alibaki kimya.....
Danny hayo yameshapita na mm nimeshasamehe yote...alisema eva
Siku hyo mitandao ya kijamii ilijaa watu wakifuatilia habari za victor..
""Sasa mmeona nyie mliokua mnarefusha midomo et eva muuaji?""
"Hahaaaa haters wote kimewashuka..mmuache eva wetu"
Zilikua ni kauli za mashabik wa eva ambao walikua wakijigamba sana siku hiyo...
eva akiwa amekaa na danny na miriam...mara alikuja mtu akamuita eva..
Eva alishtuka sana baada ya kumuona shangaz yake.
Shangaz!!!!!!
Mwanangu...mimi nipo hai mwanangu...sijafa.
Shangaz... Eva alienda kumkumbatia shangaz yake kwa machoz ya furaha yakimtoka...
Walikaa wakaongea mengi sana.
Shangaz,, vp..umemsamehe mme wako?
Nishamsamehe maana ameshajutia makosa yake na ametusaidia..halaf hata nisiposamehe sitabadili kitu..
Eva alifrah kuona kazmoto amesamehewa na shangaz yake.
**********MIAKA MITANO BAADAE*******
Adrian,jennifer, msalimieni babu...alisema eva akiwaambia watoto wake mapacha aliowaita majina ya wazaz wake.maana walipatikana baada ya tabu ya kesi ya mauaji yao kuisha.
Shkamoo babu..
Marahabaa...aliitikia victor aliekua akitumikia kifungo chake mda huo na familia yake ilikua imeenda kumtembelea..
Eva mwanangu ish vizur na danny... Muwalee wajukuu zangu vizur..
Sawa baba aliitikia eva...familia ilimuaga victor na kuondoka.
Baada ya kutoka pale gerezan...danny miriam na eva walienda kutembelea makaburi ya wazaz wa eva..
Miriam...wewe ni rafik mzuri..alisema eva..hata cha kukulipa sina nashkuru sana shost..
Usijali eva..maisha ni kusaidiana..
Baada ya misukosuko yote eva alirudi kwenye chat na kua maaruf kuzid mwanzo....alikua kama jamira..
Aliikumbuka ndoto yake iliyokua ikimsumbua siku zile na kuona kua imetimia maana ni kama alirith nafas ya jamira....
Akiwa anafikiria mambo yaliyopita..alikuja danny huku akinyata na kumkumbatia eva kwa nyuma.
*********MWISHO*********
ASANTENI MLIOKUA NAMI HADI MWISHO
KAMA HAUTOJALI NAOMBA UNIAMBIE UMEJIFUNZA NINI KWENYE SIMLIZI HII YA MY EVA💖💓💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖
👇👇👇👇
BONYEZA HAPA KUCHANGIA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
ASANTENI MLIOKUA NAMI HADI MWISHO
KAMA HAUTOJALI NAOMBA UNIAMBIE UMEJIFUNZA NINI KWENYE SIMLIZI HII YA MY EVA💖💓💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖💖
👇👇👇👇
BONYEZA HAPA KUCHANGIA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni