MY EVA (4)

Zephiline F Ezekiel
MY EVA (4)
JINA: MY EVA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Wanafunzi:Nawaona baba chanja na mama chanja.. Eva aliona aibu akainama chini huku danny yeye akijidai mkakamavu na kuvunga anaendelea kusoma.. SASA ENDELEA.. Muda wa prepo uliisha na watu wakaondoka kuelekea mabwenini kwao. Eva kiherehere cha kuijua zawadi alikua wa kwanza kutoka darasani..alimuaga danny na kuondoka haraka huku akiwa amesahau hata baadhi ya vitu vyake... Danny alibakia anatabasamu tu huku akimsindikiza eva kwa macho hadi alipoacha kuonekana. Muda wote huo cathy aliku akiwaangalia tu wanayoyafanya na roho ilikua ikimuuma sana maana alimpenda sana danny lakini ndo hivyo tena,danny alikua hampendi cathy hata kidogo kutokana na kwamba cathy alikua na nyodo sana kwa vile kwao walikua pochi nene. Cathy alikua na nyodo kama zote na alikua anajishaua sana na kuwaona wengine mavi...hata kuongea na watu ilikua shida.. Cathy na danny walikua majirani huko kwao lakini hawakua na mazoe kivile.. wakiwa shuleni kila mtu alijua ham…