MY EVA (4)

0
JINA: MY EVA
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
Wanafunzi:Nawaona baba chanja na mama chanja..

Eva aliona aibu akainama chini huku danny yeye akijidai mkakamavu na kuvunga anaendelea kusoma..

SASA ENDELEA..
Muda wa prepo uliisha na watu wakaondoka kuelekea mabwenini kwao.

Eva kiherehere cha kuijua zawadi alikua wa kwanza kutoka darasani..alimuaga danny na kuondoka haraka huku akiwa amesahau hata baadhi ya vitu vyake...

Danny alibakia anatabasamu tu huku akimsindikiza eva kwa macho hadi alipoacha kuonekana.

Muda wote huo cathy aliku akiwaangalia tu wanayoyafanya na roho ilikua ikimuuma sana maana alimpenda sana danny lakini ndo hivyo tena,danny alikua hampendi cathy hata kidogo kutokana na kwamba cathy alikua na nyodo sana kwa vile kwao walikua pochi nene.

Cathy alikua na nyodo kama zote na alikua anajishaua sana na kuwaona wengine mavi...hata kuongea na watu ilikua shida..

Cathy na danny walikua majirani huko kwao lakini hawakua na mazoe kivile.. wakiwa shuleni kila mtu alijua hamsini zake.

Danny.. Aliita cathy lakin danny hata hakusikia maana mawazo yote yalikua kwa eva.

We danny... Hunisikii au kiburi...alisema cathy.

Aaah..cathy, nilikua sijakusikia...unasemaje?

Cathy alikasirika,alibetua midomo na kuondoka..

Cathy. Cathy... Aliita danny lakin cathy aliendelea kuondoka.

Kwendaa...kwani wewe nani?..kinajishebeduaga hiki...kinazani nitabembeleza...alijisemea danny kisha akaenda zake bwenini.

Huku victor alikua anawaza atatumia mbinu gani kuwatenganisha danny na eva..

Akiwa kwenye dimbwi la mawazo mara alikuja mkewe na kumshtua..

Baba danny, mbona huna raha mme wangu? Nini tatizo jamani?...aliulza rachel.

Aaah...nawaza maisha tu...alisema victor.

Mbona siku zote hauko hivi?..kwani hua huwazi maisha?...aliulza rachel.

Unajua mwanangu lazima asimzoee kabisa huyo eva... Alisema victor.

Jaman..hili ndo linakuwazisha kila saa!!...au kuna mengine?..niambie tu mme wangu.

Hakuna mengine, ni hilo tu..sitaki mwanangu aharibikiwe alisema victor.

Hilo lazima tulifanyie kazi.. Ondoa shaka mme wangu..alisema rachel huku akikaa karibu na mmewe

Unajua danny hawezi kuamini kirahisi wala kukubali kirahisi..lazima tufanye jambo kumwaminisha...alisema victor.

Tutafanya jambo gani hilo mme wangu...aliulza rachel.

Inabidi tumsingizie eva jambo kubwa hasa..tena kubwa kweli kweli ili Danny apoteze imani nae...alisema victor.

Haina shida..tutafanya lolote kumwokoa mwanetu..kwa gharama yoyote ile...alisema rachel..

Huku cathy alifika bwenini akiwa amevimba sana kama apasuke hivi baada ya kupuuzwa na danny licha ya kua yeye ni supa staa pale shule..mtoto lain👌kuvunja biskuti hawezi...

Wakat huo eva alikua kitandani kwake amepiga "tinted" kwenye neti yake ili mtu asimwone humo ndani akiwa anafungua zawadi aloyopewa na danny.

Alifungua zawadi ile kwa pupa kujua kapewa nini

Wooow...ulikua ni mkufu mzuri na saa ya mkononi Vyote vinaumbo la love❤...eva alifurahi sana hadi akahisi amehama dunia.

Aliivaa saa mkononi na kuazimia kulala nayo bila kujali ni usiku wala nini...

Aliijaribishia cheni nayo ilimtoa balaa😋
Kwakua mikufu hairuhusiwi kuvaliwa shuleni aliutoa na kuutunza kwenye begi lake,yaan kule chini kabisa..

Wakati anatoka kutunza cathy alimkata jicho moja la kimataifa..

Cathy aliumia zaid baada ya kuona mkufu ule na saa ile mpya alivyopewa eva...roho ilomuuma hadi akatamani kulia...

Kwa hasira alipnda kitandani na kulala..

Eva alipomwona cathy kwenye hali alishtuka kidogo na kuamua kumuuliza:
Cathy... Mbona uko hivyo... Umepatwa na nini??..

Cathy alitoa kichwa kwenye shuka na kumwangalia eva vibaya sana....kisha akajifunika tena bila kusema kitu..

Eva alishangaa sana maana haikua kawaida ya cathy kumkasirikia vile....

Eva alipotezea tu na kurudi kulala huku anafurahia zawadi zake.

Siku zilizidi kwenda.. Cathy alizidi kumchukia eva kwakua alikua anambani riziki yake kwa danny.. Yaana danny tangu amjue eva hana mda kabisa na cathy wakati kwao ni majirani...kitu hiki kilimuuma sana cathy.

Huyu eva hanitishi...kwani yeye ni nani?..ngoja..mimi nawafahamu wazazi wa danny na tunafahamiana sana..kwanza najua hawatamkubali kutokana na kwamba ni maskini...

Ataachwa tu na danny.. Labda sio mimi niamue...hanishindi kitu huyu kinyago...alijisemea cathy..Nini kinafuata? ..

USIKOSE SEHEMU YA TANO

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)