Notifications
  • MWALIMU MKUU (5)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Mama roly alivyosikia rameki anataka kumwaga alimtema yule nyoka na kumficha pangoni mwake, rameki alimpambu mama roli kwa kasi ya ajabu kama ndege ya vita ikimbiavyo angani“Ramekiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!! tombaaaa”rameki na mama roli walipiga madafu kama manne “heeee rameki siamini???!!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwannn??”rameki aliuliza“DUDU LOTE HILI…
  • MWALIMU MKUU (4)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Mwalimu mkuu alistuka kuguswa na kitu kwenye makalio yake alijua rameki atakuwa kaweka mzigo nyuma yake rameki alivyoona ajakaa vizuri alisogea ili akae vizuri mwalimu mkuu alistuka kitu kama tango kikimgusa tena alipitisha mkono ili aone nn alistuka “MUNGU WANGUU”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Rameki alistuka mwalimu mkuu alivyoshika tango lake akapaza sauti“AAAAAA MWALIMU…
  • MWALIMU MKUU (3)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA TATUILIPOISHIA...chausiku alishangaa kuziona zile sale “JAMANI NANI KAKUPA MWANANGUU??!!”aliuliza chausiku kwa mshangao“Kaka juma”alijibu ramekiIKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“Oooh juma jamani mungu akubariki ooooh asante mungu”alitamka mama rameck uku akinua mikono juuRameck alizijalibu zile nguo hakika alipendeza sana adi mama ake alimfagilia kwa vigeregere “jamani juma mungu akuwekee…
  • MWALIMU MKUU (2)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA MBILIILIPOISHIA...“MUNGU WANGU YULE SI MZEE ALINANI???!!!”aliuliza chausiku kwa mshangao chausiku alimuangaria mzee alinani ambae amepoteza furaha yake ya kusomaMzee alinani alikuwa anakuja kuangaria bishala zake pale sokoni kwa kina chausiku.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Mzee alinani alistuka kumuona chausiku alikwepesha macho yake kwa aibu alitoka kwenye soko lile, chausiku alimpitia…
  • MWALIMU MKUU (1)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA KWANZA“MAMA USIFE MAMA NITAISHI VP NA HII MIMBA MAMA”ilikuwa ni sauti ya mdada aitwae chausiku akimwambia mama ake asifee bado anamtegemea mama ake na mimba yakee“CHAUSIKU MWANANGU NAJUA MIMI NDIYO TEGEMEZI LAKOO NILIPAMBANA NA KILIMO ILI USOMEE LAKINI UMECHEZEA SHIRINGI CHOONI MWANANGU UMESHIKA MIMBA BADO MWAKA MMOJA TUU UMALIZE LAKINI NDO IVYO MWANANGU MIMBA NDO ISHAINGIA SINA BUDI KUKUFUKUZA INGALI UKO MOYONI MWANGU NAKUPENDA MWANANGU CHAUSIKUU ILA…
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…
  • THE NIGHTMARE (5)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa…

RANIA (3)

JINA: RANIA
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Rania akiwa anaendelea na kazi yake ya kunusanusa maua,mara alivutwa na mtu  uchochoroni..

SASA ENDELEA..
Rania alishtuka sana na kugeuka ili kuangalia  nani kamvuta.
Alipogeuka tu alishangaa kuona ni Mwanamfalme Fasha.

Rania alitumbua macho kwa mshangao..

Wewe ume...alijaribu Rania kusema lakini mwanamfalme alimziba mdomo.

Shiiii....kaa kimya,ukisikika hapa umekufa...alisema Fasha.

Kufa?..nani aniue?..Aliuliza Rania baada ya kutoa mkono ww Rania mdomoni

Fasha alimziba tena Rania mdomo kwa kiganja chake maana aliona kwa maneno tu haelewi..

Muda mfupi baadae Mfalme na watu wake walifika mahali pale.

Mbona hakuna mtu Mfalme?..aliuliza omandi.

Atakua ameenda wapi?..aliuliza mfalme.

Labda itakua alitoroka baada ya kutuona...alisema omandi.

Basi tumfuatilie...alisema mfalme na wote wakaondoka kweda mbele huku wakimwachwa nyuma Rania.nyuma .baada ya mfalme na watu wake kuondoka,Rania na Fasha walitoka kwenye korongo lile waliokua wamejificha.... Aliita Rania.

Mwanamfalme.. Aliita Rania.

Naam...aliitika Fasha.

U..u..mefikaje hapa?..kwanini.. Aliuliza Rania.

Nimefika kwa miguu...alijibu Fasha.

Kwahyo unazani mimi sijui kama unamiguu...mwone huyu nae...alisema Rania baada ya kujibiwa utumbo.

Lakini mwanamfalme, umejuaje kama kuna watu wananifuata?...aliuliza Rania.

Niliwasikia....alisema Fasha.

Ni akina nani?..aliuliza Rania.

Ni watu wabaya kutoka ikulu...alisema Fasha.

Mmmh...sasa mimi wananitafuta kuniua kwa sababu gani?..aliuliza Rania.

Fasha alimgeukia Rania na kumwangalia jicho baya..

Nini?.kwahyo nimuulize nani haya maswali?...alisema Rania baada ua kukatwa jicho la mke mwenza😕

Mimi sijui nia yao...halafu unaongea sana wewe... Alisema Fasha.

Rania alimwangalia Fasha kama anataka kumtapika vile,halafu wakaendelea na mazungumzo.

Sijui nikuweke kundi gani wewe.. Sijui la watu wabaya..sijui la wema...alisema Rania huku anazungusha kichwa huku na kule.

Nani,mimi?..aliuliza Fasha.

Hapana...naongea na nyani yule pale mbele...alisema Rania.

Fasha alitikisa kichwa tu na kukaa kimya.

Fasha, siijui njia ya kutoka hapa.?nisaidie basi....alisema Rania huku amemshika Fasha mkono kwa nguvu.

We nani amekuruhusu kunigusa?...aliuliza Fasha.

We nae unajiona bora wakat....(hsakhshshdgdhsh)...alisema Rania maneno yasioeleweka.

Unanitukana wewe?..alisema Fasha.
Kwani umesikia tusi gani hani hapo?....alisema Rania.

Wakiwa wanabisha mara alikuja Dom.

Raniaaaaaa...aliita Dom akitabasam.

Doooooom...alijibu Rania.

Rania, mimi naondoka...atakupeleka huyu kwenu,bila shaka anapafahamu maana inaonekana mnafahamiana...alisema Fasha na kuondoka.

We nenda tu hata hivyo amekuja Dom...atanipeleka kwetu..alisema Rania.

Hata halina shukurani...alisema Fasha kisha akaondoka....

Rania alikua anamwangalia tu Fasha wakati akiondoka..alipofika mbali akasema:

Mwanamfalmeeeeee....asante sana..ufike kwenye kasri salamaaaa.

Fasha aligeuka akampungia mkono Rania na kutokomea.

Aaah...Dom,umewinda wanyama wote hawa...alisema Rania.

Eee..si ndo maana mimi na kwambia kua mimi ni noma...yaan mimi mjanja sana...mtaani kwetu waschana wote wanataka nikikua niwaoe...alisema Dom kama kawaida yake.

Dom alipomaliza kuongea akatua macho yake kwenye uso wa Rania na kukuta Rania anamwangalia  kama anaangalia kinyesi.

Nini wewe?...unaniangaliaje hivyo?.. Aliulza Dom.

Nimeshakupata...enhee...nimeshakujua wewe....alisema Rania.

Umejua nini?..aliuliza Dom macho yamemtoka.

Kwaheri Dom, alisema Rania huku akitembea kwa kudunda kama yuko kwenye mashindano ya miondoko.

Nyambaafu...hivi haka kadada mbona hakapendi kunikubali kua mimi mjanja?..hadi nijisifieje?...alijiuliza Dom.

We Raniaaa...unaenda wapi?..unaijua njia wewe?..aliuliza Dom..

Rania aligeuka akimwangalia Dom kisha akageuka na kuendelea tu kudunda.

Haya kwenda..alisema Dom na kugeuza njia ya kwenda kwao.

Kabla hajaenda mbali alisikia sauti ya Rania ikiomba msaada kama ametekwa vile.

Dom alirudi kwa kasi ili kuja kumsaidia Rania.

Alipofiaka sehem aliposikia kelele hakumwona Rania..Dom alichanganyikiwa zaidi.

Akiwa anawaza mara Rania alitokea kichakani akiwa anacheka... Hihhihihi..Dom jamani

Tse...tse...tse...yaaani wewe nitaku....alisema Dom huku akitishia kumpigia Rania kofi..

Rania alicheka kwa kuona amemkomesha Dom.

Dom nipeleke kwetu..alisema Rania hukua amemkazia Dom macho ya kutaka msaada.

Dom alimwangalia  tu,akajishaua shaua ila akakubali

Baada ya muda walikua wamefika kwao Rania.

Kaasha alikua amevimba macho kwa ajili ya kulia..

Akiwa analia mara mlango uligongwa...bibi hakuamini kumwona Rania akiwa mzima...alimkumbatia kwa furaha kwa muda mrefu.

Ulikua wapi mwanangu?... Mbona hukuaga?..aliuliza bibi.

Rania alikaa chini na kumsimulia bibi kila kitu..

Heee..mwanangu jamani.. Ila tumshukuru Mungu umepona jamani..

Kijana, Asante kwa msaada wako mwanangu... Alisema bibi akimtazama Dom.

Unaitwa nani kwani?.. aliuliza bibi.

Naitwa Dom...

Jina zuri sana kama ulivyo..alisema kaasha.

Dom alitabasam tu..

Baada ya chakula Dom aliaga na kwenda kwao..kaasha na Rania walimsindikiza hadi mbele kidogo.

Kwaherini..tutaonana siku nyingine.. Alisema Dom na kuondoka..

Rania alikua akimwangalia Dom alipokua anaondoka hadi alipotokomea

Wewe..unaangalia nini?.. Alisema bibi.

Aaah...mimi... Hamna kitu.. Alisema Rania na wakaondoka na kaasha kurudi nyumbani.

Wakati huo Mfalme na watu wake baada ya kumkosa Rania waliamua kurudi kwenye kasri.

Mfalme... Nakuomba utulie..atapatikana tu huyo mtoto.  Alisema omandi.

Omandi.... Aliita Mfalme.

Naam.... Aliitika omandi.

Unajua sijawahi kukwambia vizuri kuhusu NADISH.. We unachojua tu ni kitu hatari kwa ufalme wetu..lakini ukweli wenyewe uko hivi:

Miaka mingi iliyopita,Mfalme wa himaya hii alipinduliwa kwenye nafasi yake baada ya kudhoofu sana kimadaraka na kijeshi pia.

Waliompindua,mmoja wapo ni babu yangu marehem Mfalme aliepita.baada ya kumpindua babu yangu alitawala na alipokufa alirithishwa baba yangu.

Wakati wa utawala wa baba yangu mganga wa ikulu alitabiri kutatokea "NADISH "  Maana yake atakuja kuzaliwa mtoto ambae atasababisha ufalme huu utoke mikononi mwetu kwa na kurudi kwenye ukoo wa Mfalme aliepinduliwa enzi zile kwa kua sisi si watawala halali.

Baada ya utabiri huo baba alikasirika sana na kuamuru mganga huyo auawe maana anautukana ufalme na kuutabiria mabaya..

Mganga aliepo sasa analitambua hilo ila kwa hofu ya kufa hakumweka wazi baba yangu..alikuja kuniambia hilo pale nilipokua Mfalme na kusema natakiwa kumkamata huyo mtoto alietabiliwa nimuue...alisema Mfalme

Omandi alishangaa sana kusikia hayo.

Mfalme,sasa mbona mtoto mwenyewe ni wa kike?..aliuliza omandi.

Kwakweli hata mimi nashangaa....nashindwa kuelewa kwakeli..alisema Mfalme.
*******

Mganga, umeniita...alisema malikia suya wa Tharia.

Ndio nimekuita mtukufu malikia...Nimekuitia jambo moja tu hapa:

NADISH imerejea..alisema mganga.

Nini?.. Alishtuka malikia.

NADISH imerejea..cha ajabu ni mtoto wa kike... Alisema mganga.

Sasa mtoto wa kike atawezaje kufanya mapinduzi na kututawala?...alisema malikia.

Sijajua kwakweli.. Alisema mganga.

Lakin si uliweka dawa kua mtu yeyote wa damu ya mfalme yule aliepinduliwa (kelkun) akikanyaga ikulu kwamba atakufa?..aliuliza malikia.

Ndio niliweka..alisema mganga.

Sasa amewezaje kutoka salama huyo binti?.. Aliuliza malikia.

Huyo binti sio damu ya kelkun,wala sio ndugu wa kelkun..alijibu mganga.

Sasa iweje atupindue??yeye kama nani?....aliuliza malikia.

Hapo sijui hata mimi..alisema mganga.

Hujui nini wakati wewe mganga?... Aliuliza malikia kwa ukali.

Mganga sio Mungu mtukufu malikia... Alisema mganga.

Hakikisha unashughulikia hili swala hadi nijue kama sivyo nitakutoa hapa mara moja.. Alifoka malikia.

Ndio malikia.. Alijibu mganga.
******
Kuna aliekuja hapa kuniulizia?..aliuliza Fasha baada ya kurudi kutoka mstuni..

Hapana... Alijibu jao.

Wakiwa wamekaa,jao alimuuliza mwanamfalme.

Mwanamfalme, kwanini umehatarisha maisha yako kiasi hichi kwa mtu aliekukosea?..

Mimi sio katili jao..bali nafanya hivi, nataka watu waninyenyekee kwa sababu fulani.. Alisema Fasha.

Kwanini mwanamfalme?.. Aliuliza jao.

Jao..mda wangu wa kukaa ikulu utaisha wakati wowote... Mimi si wa hapa siku zote.. Kwahyo nikiwa hapa nitaitumia nafasi hii kuogopwa vilivyo na kuheshimiwa.....alisema Fasha.

Una maana gani kusema wewe si wa hapa?..aliuliza jao...

Jao...bila shaka hukujua hili jambo...naomba leo nikwambie ukweli.. Lakini uwe msiri...ukilopoka tu kichwa huna.  Tunaelewana lakin?... Alisema Fasha.

Ndio mwanamfalme.. Alijibu jao...

Ukweli kuhusu mimi ni huu....alisema mwanamfalme na jao akatega sikio..Fasha alimsogelea sikioni na kumnong'oneza kitu..

Jao hakuamini alichokisikia...alihisi ni ndoto.NI NINI HICHO?..

USIKOSE SEHEMU YA NNE

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
1 Rania Simulizi Z1
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni