
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
Jao,ukweli kuhusu maisha yangu hi huu..alisema Fasha kisha akamsogelea jao na kumnong'oneza kitu fulani.Jao hakuamini maskio yake kwa alichokisikia..
SASA ENDELEA..
Mwanamfalme!!!... Aliita jao kwa mshtuko.Ni kweli jao...mimi sio mtoto halali wa Mfalme,Mfalme hana uwezo wa kupata mtoto..nilimsikia mama yangu malikia akiongea na mganga... Alisema Fasha kwa unyonge sana.
Jao alibaki mdomo wazi... Hakuamini alichokisikia.
Kwahyo, wazazi wako wako wapi?.. Aliuliza jao.
Sijui walipo... Siwafahamu...alisema Fasha.
Kwa mujibu wa malikia na mganga, mimi sio mtoto halali na wa Mfalme na hata malikia sio mama yangu mzazi.. Siku nilipojua huo ukweli sikulala usiku mzima..si unakumbuaka?..aliuliza Fasha.
Nakumbuka mwanamfalme.. Alisema jao.
Basi nilikua nikisumbuliwa na ukweli huu unaouma..alisema Fasha.
Sasa, utafanya nini siku ikijulikana?..aliuliza jao kwa wasiwasi.
Nitaondoka kama wakitaka..na ndio maana nakua mbabe na katili maana najua mwisho wangu wa kuishi hapa umekaribia ..alisema Fasha.
Lakini mwanamfalme, sio kwamba ungewatendea watu wema ili siku ukitoka hapa wakuhifadhi....alipendekeza jao.
Mwanamfalme alitabasam tu maana alijiua mwenyewe cha kufanya siku mambo yakiharibika..
Huku Mfalme alimwita omandi...
Niko hapa mfalme.. Alisema omandi baada ya kuitwa na mfalme.
Muda mfupi baadae Fasha nae alikuja maana nae pia aliitwa na mfalme.
Fasha,... Aliita mfalme.
Naam... Aliita fasha.
Unajua sehemu anayoishi yule binti aliekutukana siku ile?..Aliuliza mfalme.
Fasha alishitushwa na swali lile...alipata kigugumizi kujibu..
Fasha.. Nimekuuliza...alisema Mfalme
Sipafamahu...alisema Fasha.
Fasha, wewe ndie Mfalme ajae...na wewe unalijua hilo bila shaka...yule binti ni tishio kwa ufalme huu....alisema mfalme.
Tishio?....kiaje?...aliuliza Fasha.
Asipouawa,ufalme huu utatoka mikononi mwetu.. Yeye ni mtu hatari kwa usalama wa utawala wa ukoo wetu..mganga aliamuru auawe ama ufalme huu tutaupoteza...alisema Mfalme kisha akaweka kituo.
Fasha alitumbua macho yake kwa mshangao.
Ni jukumu lako wewe kama mwanamfalme wa sasa na mfalme ajae kuulinda ufalme huu...utaongoza kazi hii ukisaidizana na omandi.. Hakikisheni mtu hafahamu kuhusu hili... Alisema mfalme
Fasha alikua bado hajaelewa hasa nini kosa la Rania, lakini mfalme hakutaka maswali zaidi.
Fasha akiwa mwenyewe aliwaza sana...
Kwanini Rania?... Amekosa nini?...alijiuliza Fasha.
Akiwa anawaza mara jao alifika...
Unawaza nini mwanamfalme?.. Aliuliza jao
Mwanamfalme alimsimulia yote jao..
Haaa.. Sasa utafanya nini?...aliuliza jao..
Hata sijui cha kufanya....alisema fasha.
Fanya maamuzi sahihi ambayo hautakuja kuyajutia mwanamfalme.. Alisema jao
Ndio najaribu kuangalia...alisema Fasha.
******
Raniaaaa... Aliita Dom baada ya kufika kwao Rania bila taarifa.
Abeee...aliitika Rania.
Twende tukacheze kule bwawani...alisema Dom.
Rania bila kupoteza muda aliungana na Dom kwenda bwawani kucheza maana kulikua na maua mazuri sana..Rania aliyapenda.
Bibi naenda kucheza.. Alisema Rania kumuaga bibi yake.
Wapi?.unaenda na nani?.. Aliuliza kaasha.
Kule karibu na bwawa .kwenye maua... Naenda na Dom huyu hapa... Alisema Rania.
Haya.. Dom,mwangalie huyo asiangukie majini...maana hatulii huyu.. Alisema bibi.
Sawa bibi ..namjua huyu hatulii..alisema Dom huku akimwangalia Rania aliekua amenuna..
Katika matembezi ya mwanamfalme,alipita katika eneo fulani lililo karibu na bwawa kubwa la maji.
Alipoangaza huku na kule aliona watu wawili wanacheza na kukimbizana
Mwanamfalme aliwasogelea ili wamsujudie kama kawaida yake.
Alipowakaribia aligundua kua walikua Dom na Rania.
Kipindi anafika wao hawakua wamemwona..wakaendelea kucheza maana mchezo ulikua umenoga.
Nyinyi..hamjamwona mwanamfalme mkampa heshima yake?..aliuliza jao.
Aaah...mwanamfalme... Kumbe upo hapa..alisema Rania.
We unaongeaje hivyo na mwanamfalme?.. Aliuliza jao kwa ukali..
Fasha alimtuliza..kwakua alijua Rania alivyo jeuri wangeishia pabaya.
Dom na Rania walitoa heshima yao kwa mwanamfalme.
Karibu kwenye mchezo wetu kama utapenda...alisema Rania huku anatabasamu...
Hebu nielelekeze kidogo na mimi nione...alisema mwanamfalme.
Ni hivi....alianza Rania kuonesha..kwa bahati mabaya aliteleza na kudondokea bwawani.
Raniaaaa...aliita Dom kwa mshtuko.
Mwanamfalme alishtuka sana kuona vile.
Dom na Fasha wote kwa pamoja waliingia bwawani kumwokoa Rania maana hakujua kuongelea.
Baada ya muda mfupi walikua wamefanikiwa kumwokoa Rania.. Wote wakiwa wamemshika mkono ..Dom kulia na Fasha kushoto.
Rania,unajisikiaje?..aliuliza Fasha huku akitumia ubabe kumfanya Dom amwachilie Rania mkono...hapendi kushea..alaa😏.
Mwanamfalme umenisaidia tena leo..nashukuru sana...alisema Rania.
Mwanamfalme alibaki amemkodolea macho Rania maana hakujua kama Rania nae hua anaongea kistaarabu..maana sio kwa jeuri alomwonesha siku ile.
Wakati huo Dom alikua amevimba kama andazi lililozidiwa hamira hasa pale Rania alipoonesha kumshukuru sana mwanamfalme wakati wameshirikiana kumsaidia.
Baada ya muda Fasha alimwachia Rania na akasema:
We kijana (Dom), mpeleke huyu nyumbani mapema.. Hii ni amri...alisema Fasha ili ajioneshe yeye ni bora na ili kumkomoa Dom.
Baada ya hapo mwanamfalme alimuaga Rania tu na kuondoka zake kama hakua akimwona Dom.
Baada ya fasha kuondoka,Dom alibaki na Rania.
Rania, hata sasa bado hujaikalili njia?.. Aliuliza Dom maana hata hakutaka kuambatana na Rania.
Lakini mwanamfalme amekupa amri unipeleke...sasa nitaendaje peke yangu?. Alisema Rania.
Dom aligeuka na kumwangalia vibaya Rania hadi Rania akajishtukia maana hakuwahi kumwona Dom kwenye hali ile.
Dom...umekasirika?..aliuliza Rania.
Wala sijakasirika hata ..alisema Dom.
Siajawahi kukuona hivi Dom.. Umekasirika..alisema Rania.
Lakini Dom..wewe ni rafiki yangu tu.. Tena wa kwanza kabisa.. Usiwe hivyo et Dom.. Na wewe umeshanisaidia mara nyingi sana...alisema Rania huku akimwangalia Dom usoni kuona kama maneno yake yanafanya kazi.
Dom ndo kwanza alikua amevimba bado..abembelezwe zaidi😋.
Rania aliendelea kumbembeleza Dom akimsihi asinune lakini wapi.... Baada ya kumbembeleza kwa muda mrefu bila mafanikio Rania akamwangalia Dom na kugundua kua Dom alikua akicheka na kuendelea kujikausha kama amevimba.
Heeee... Yaani kumbe wewe unacheka!!!...aliongea Rania huku amekodoa macho huku anabinua binua midomo.
Dom uvumilivu ulimshinda ikabidi aangue kicheko..hihihihi..
Rania akakasirika na kunza kwenda kwao huku akitukana njiani...shenzi.. Shenzi kweli.. Yaani mimi nabembeleza mtu ..shenzi kabisa...hivi nimeanza lini kwanza?..pumbafu..
Huku Dom alikua akicheka sana baada ya kumshuhudi Rania akimbembeleza..
Raniaaaaa....nisubiri nikupeleke kwenu.. Alisema Dom.
Sitaki naenda mwenyewe.. Alisema Rania huku akiongeza mwendo
Ni amri ya mwanamfalme lakini... Alisema Dom
Sijali hilo.... Alisema Rania.
Dom alimkimbilia Rania na kumshika mkono halafu akasema;
Nakupeleka kwenu...tangu lini nakaidi amri za kifalme mimi?.alisema Dom.
Niache...alisema Rania huku akitoa mkono
Dom alimbebelea Rania begani kama swala mfu na kwenda nae kwao.
Njia nzima Rania alienda anapiga makelele..nishushe..nishusheeee...lakini Dom hakujali..alimpeleka kwao hivyo hivyo.
****
Dom akiwa nyumbani kwao baada ya kumpeleka Rania, alikua akicheka kama chizi kila akikumbuka alivyobembelezwa na Rania.
Hahahha....alichelelea Dom huku akiruka ruka na kusema "Rania"..." Rania.."
Hivi huyo Rania ni wa wapi?..naomba nimwone siku moja..naona umeshakua chizi wewe...alisema mama yake Dom.
Dom alishtuka na kuacha kurukaruka.
Na leo umeenda kwa Rania?..aliulza mama Dom.
Hamna mama...alisema Dom huku akijaribu kuondoka ili kumkwepa mama yake.
Njoo hapa.. Alisema mama Dom huku akimrudisha Dom.
Kaa hapa leo unieleze huyo Rania ni wa wapi..maana sikuelewi siku hizi.. Alisema mama Dom.
Huku kaasha alikua anaongea na mwanae pame.
Pame,naomba niondoke na Rania twende mahali pengine nje ya Tharia...alisema kaasha.
Kwanini mama?..aliuliza pame.
Jana niliota ndoto mbaya sana juu ya Rania.. Niliota Mfalme anamchinja..alisema kaasha.
Mfalme?... Aliuliza pame kwa mshangao
Ndio, mfalme...hii ni dalili mbaya sana...lisema kaasha.
Kaasha alimweleza hata ya siku ile ambapo Rania alikamatwa na Fasha.
Hee mwanamfalme?.. Alishangaa pame.
Ndio mwanamfalme... Alisema kaasha.
Mmmh... Aliguna pame
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu walikubaliaba Rania ahame. Pame alikubali maana mama yake alikua akiota ndoto mara nyingi hutokea kweli.
Rania akiwa amekaa, alikua akionge mwenyewe: hivi nani rafiki yangu zaidi?
Dom au Fasha, Dom au Fasha, Dom au Fasha Dom...
Amefanya nini Dom?. Aliuliza kaasha.
Aaah.. Ni rafiki yangu... Alisema Rania
Haya mwanangu.. Kuna jambo nataka nikwambie...alisema kaasha.
Niambie bibi.... Alisema Rania.
Utakubali lakini Rania?.. Aliuliza kaasha.
Nitakubali maana wewe ni bibi yangu... Alisema Rania.
Mwanangu nataka tuhame nchi...alisema kaasha huku akimwangalia Rania usoni..
Heee...tuhame?....aliuliza Rania kwa mshangao
Mwanangu, ni kwa ajili ya usalama wako tu..alisema kaasha
Kiaje bibi?.. Alisema Rania kwa mshangao.
Kabla kaasha hajajibu kitu mara walisikia farasi wakija kwa vishindo vikuu..
Wote kaasha na Rania waligeuka kuona ni nini hicho..NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA TANO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO