RANIA (3)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Rania akiwa anaendelea na kazi yake ya kunusanusa maua,mara alivutwa na mtu uchochoroni.. SASA ENDELEA.. Rania alishtuka sana na kugeuka ili kuangalia nani kamvuta. Alipogeuka tu alishangaa kuona ni Mwanamfalme Fasha. Rania alitumbua macho kwa mshangao.. Wewe ume...alijaribu Rania kusema lakini mwanamfalme alimziba mdomo. Shiiii....kaa kimya,ukisikika hapa umekufa...alisema Fasha. Kufa?..nani aniue?..Aliuliza Rania baada ya kutoa mkono ww Rania mdomoni Fasha alimziba tena Rania mdomo kwa kiganja chake maana aliona kwa maneno tu haelewi.. Muda mfupi baadae Mfalme na watu wake walifika mahali pale. Mbona hakuna mtu Mfalme?..aliuliza omandi. Atakua ameenda wapi?..aliuliza mfalme. Labda itakua alitoroka baada ya kutuona...alisema omandi. Basi tumfuatilie...alisema mfalme na wote wakaondoka kweda mbele huku wakimwachwa nyuma Rania.nyuma .baada ya mfalme na watu wake kuondoka,Rania na Fasha walitoka kwenye korongo lile waliokua wamejificha...…