RANIA (5)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Mwanangu nataka tuhame nchi...alisema kaasha huku akimwangalia Rania usoni..

Heee...tuhame?....aliuliza Rania kwa mshangao

Mwanangu, ni kwa ajili ya usalama wako tu..alisema kaasha

Kiaje bibi?.. Alisema Rania kwa mshangao.

Kabla kaasha hajajibu kitu mara walisikia farasi wakija kwa vishindo vikuu..

Wote kaasha na Rania waligeuka kuona ni nini hichsana

SASA ENDELEA..
Walipogeuka walishangaa kuona kundi la watu wengi wakikimbia huku na huko kuokoa maisha yao.

Walipoangalia zaidi waliona jeshi kubwa nyuma likija...

Bibi...akina nani hao?..aliuliza Rania kwa uoga.

Wanajeshi wa nchi ya Baseki...alisema kaasha.

Haaa..wamekuja kufanya nini?...aliuliza Rania.

Kufanya vita na hii nchi yetu...alisema kaasha.

Rania alikodoa macho kwa uoga sana..walikimbia na kwenda kujificha kweli handaki.

Vita ilipigwa kati ya nchi ya Tharia na Baseki kwa muda wa miaka saba.watu wengi wa pande zote mbili waliuawa na wengine walikimbia nchi Zao.

Wakati wa vita familia ya Rania walikimbia nchini sababu ya vita pamoja na hofu ya Rania kupata madhara kutoka familia ya kifalme.

Licha ya kua Tharia walishinda vita  vile,lakini walikua wameathirika vibaya sana hasa kiuchumi maana Baseki waliharibu mambo mengi kwenye nch hiyo.

Baada ya hiyo miaka saba vita viliisha na yalibakia makovu ya vita.

Iliwagharimu muda kama wa miaka mitatu mingine kuirudisha nchi kwenye hali yake.

hadi hapo ilikua imepita miaka kumi.Rania alikua na umri wa miaka  20,Dom 25 na mwanamfalme Fasha alikua na miaka  23
********
Baada ya vita kuisha,Dom alikwenda alikokua akiishi Rania kwends kuona nini kilitokea maana hawakuwahi kuonana maana familia ya Dom walikimbia nchi pia.

Dom alifika na kukuta nyumba waliokua wanaishi Rania na familia yake imeharibiwa vibaya sana.

Aliamua kwenda kuwauliza majirani waliokua pale.

Kijana,pole sana...Rania alipoteza maisha wakati wa viita..alisema jirani.

Dom alihisi kuishiwa nguvu.. Alijikuta akitokwa na machozi mfulilizo..

Aliondoka pale kwa unyonge sana... Alikua bado hajaamini kama hatamwona Rania tena.

Alikwenda nyumbani kwao akiwa mnyonge sana akaingia ndani na kukaa machozi yakimtoka.

Mwanangu, umekuaje..mbina unanitisha?..aliuliza mama yake Dom.

Rania...alisema Dom kwa unyonge.

Alikufa vitani?..aliuliza mama.

Dom hakujibu bali aliendelea kulia.

Pole mwanangu...pole.. Alisema mama Dom huku akimkumbatia mwanae.

Fasha.. Aliita Mfalme

Naaam.. Aliitika Fasha.

Sasa vita imekwisha na nchi iko katika hali ya utulivu tena.. Alisema mfalme.

Ndio baba...alisema Fasha.

Nina imani hujaisahau kazi yako inayokupasa...kuhusu yule binti...anza kumtafuta sasa na ukimpata auawe mara moja... Alisema mfalme.

Ndio baba...alijibu Fasha.

Kesho yake Fasha alitoka na kwenda mtaani kuangalia hali ya maisha ya watu wachache walio kua katika nchi ya Tharia.

Akiwa njiani anatembea mara alimwona Dom.

Alimfuata alipokua na wakasalimiana...baada ya salamu walitoka na kuelekea sehemu tulivu kwa ajili ya maongezi zaidi.

Ni muda mrefu sasa...kidogo hata nikusahau...alisema Fasha.

Ni kweli ..muda mrefu umepita..

Vipi..unapafahamu alipokua akiishi Rania?.. Aliuliza Fasha.

Napafahamu...lakin kwa sasa Rania hayupo...alisema Dom..

Hayupo?..alienda wapi?....aliuliza Dom.

Sifahamu. Nilikwenda kwao siku moja lakin nyumba yao ilikua imeharibiwa vibaya sana...alisema Dom kwa maumivu moyoni mwake

Mwanamfalme aliingiwa na mashaka makubwa..

Ulimuuliza yeyote?... Aliuliza Fasha.

Dom alikaa kimya kwa muda kisha akasema,walisema Rania alikufa wakati wa vita muda mrefu uliopita....

Fasha alihuzunika sana kujua Rania alishapoteza maisha..roho yake ilimuuma sana hasa akikumbuka ucheshi na vituko vya Rania.

Rania, pumzika kwa amani huko uliko..nitakukumbuka sana...alijisemea mwanamfalme.

Fasha alimtaarifu Mfalme kua Rania alishapoteza maisha kipindi cha vita.

Mfalme alishusha pumzi nzito sana akiona mzigo ameutua.

Malikia suya na mganga nao walifurahi pia.

Dom hakua mwenye furaha hata kidogo tangu vita iishe..alimmis sana Rania na vituko vyake..alikua akitembea tembea mule porini na kukumbuka siku ile alipokutana na Rania..siku zingine alikwenda kwao Rania na kusimama muda akipaangalia na kukumbuka vingi.

Bibi...hivi ikitokea wakawauliza majirani si nitajulikana niko hai?..alisema Rania.

Nilishawaambia waliulizwa waseme umekufa..alisema kaasha.

Ila mimi mfalme ananionea tu hata sina huo mpango na ufalme wake..alisema Rania huku amevuta mdomo.

Rania na bibi yake walitoka na kwenda kutembea mtaani...walipo fika sokoni walisikia tangazo kutoka ikulu likitanganzwa na maaskari wa ikulu..

Pisha njia mfalme anakujaaaaa..pisha njia mfalme anakujaaaaa...pisha njaaaaa..

Wote walipisha njia Mfalme apite..

Mfalme wa nchi ile ya Lazi alipita akiwa juu ya farasi wwke mweupe.

Mfalme alikua na mawaa kama yote..jeuri debe zima..

Akiwa anapita mara alimwona Rania.Mfalme akasimamisha farasi na kumwita mtumishi wake akamuagiza amletee Rania.

Mfalme alitembea sana na hatimaye alikwenda kujipumzisha sehemu moja tulivu ambako hakuna mwananchi wa kawaida alieruhusiwa kwenda kwa kua mfalme anapunga upepo huko.

Baada ya muda mtumishi wa Mfalme alimfikia Rania.

Samahani mama. Huyu binti yako anahitajika na mfalme mara moja.

Mfalme!!??.  Aliuliza kasha kwa mshangao.

Ndio Mfalme anahitaji kumwona..alisema mtumishi..

Kaasha alikua na hofu lakini Rania alimwambia asiogope.

Bibi..mimi naenda na nitarudi salama.. Wala usijali bibi.. Alisema Rania.

Rania alimuaga bibi yake na kwenda kuonana na mfalme.

Aaah..ni mzuri sana kuliko nilivyomwona mwanzo..alisema mfalme baada ya Rania kufika.

Rania alitoa heshima yake kwa Mfalme na akasimama kusubiri alichoitiwa.

Binti mrembo unaitwa nani?...aliuliza Mfalme.

Naitwa Rania... Alijibu Rania akiwa amemkazia macho mfalme bila hata hofu.

Wew bintu wewe ni nani hata umjibu mfalme ukiwa umemtazama?  Hebu inamisha uso wako haraka sana nguo chakavu wewe!!! Alisema mlinzi wa mfalme.

Rania aligeuka na kumwangalia vibaya mlinzi kwa tusi alilomtukana...

Wewe binti!!!... Unasubutuje kuleta dharau kwa mtumishi Wangu mbele yangu?..alifoka mfalme na kusimama.

Wala Rania hakuonekana na wasiwasi wowote... Alikua kawaida tu

Mfalme.. Sikiwahi kufika ikulu wala sijui sheria za kuongea na watawala...ningejuaje sasa?..aliuliza Rania.

Wewe ni nani kuniuliza maswali?.. Aliuliza mfalme kwa hasira huki akimkaba Rania shingoni kwa mkono wake.

Rania alibaki amemwangalia Mfalme bila wasiwasi ..

Mfalme alishtushwa na tabia ya Rania

Unawezaje kuniangalia kama mwananchi wa kawaida wewe gunia bovu?  Aliuliza mfalme kww hasira

Rania alitabasam tu huku akiendelea kumwangalia Mfalme.

Wewe ni kiongozi wa aina gani unaetaka kuongopwa kama Mungu?..kila mtu kuna anachoogopa. Mimi kunavitu naogopa lakini sio mwanadamu tu kama mimi... Utanisamehe sana mtukufu mfalme wa nchi hii..alisema Rania

Mfalme alishtuka na kumwachia Rania.

Huyu mtoto si wa kawaida...sijawahi kuona kama yeye.. Alijisemea mfalme wa Lazi.

Unathubutuje wewe kufanya hivi?..alisema mlinzi wa mfalme.

Mnafanya nini nyinyi wanajeshi wa ikulu?. Kamata huyu mfungeni haraka... Alisema mlinzi wa mfalme.

Hapana....msimfanye baya lolote...alisema Mfalme wa Lazi.

Mfalme!!!..amekudharirisha huyu!!!.  Alisema mlinzi wa mfalme kwa hamaki

Nimesema mwacheni..mimi najua la kufanya... Alisema mfalme...NINI KINAFUATA?..

USIKOSE SEHEMU YA SITA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni