RANIA (6)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Hapana....msimfanye baya lolote...alisema Mfalme wa Lazi. Mfalme!!!..amekudharirisha huyu!!!. Alisema mlinzi wa mfalme kwa hamaki Nimesema mwacheni..mimi najua la kufanya... Alisema mfalme... SASA ENDELEA.. Mfalme!!!.... Aliita mlinzi mkuu wa Mfalme. nimesema mwacheni!!...allipayuka Mfalme na wote wakatii amri. Mleteni ikulu mara moja.... Alisema mfalme huku akipanda farasi wake na kuelekea ikulu.. Niacheni nikamuage bibi kwanza...alisema Rania. Mlinzi wa Mfalme alimwangalia vibaya sana kisha akaamuru vijakazi wahakikishe anafika ikulu haraka. Vijakazi walimchukua haraka na kwenda nae. Nyie niachieni bwana mimi niende kwa bibi...alilalamika Rania. Wewe binti, tulia.. Hapa sio nyumbani kwenu kwamba unaweza ukaongea lolote utakalo...utaumia..alisema hanna(kijakazi mmoja wapo). Kuumia!!!.??..nani aniumize?..aliuliza Rania kwa sauti kubwa. Hanna na wenzake ilibidi wamuwahishe mbele maana alikuaa kashaanza vurugu. Kaasha... Kaasha.. Rania am…