RANIA (10)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (10)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Nini wewe?..Rania hayupo kwenye kasri ameondoka?. Aliuliza Faritha kwa hasira baada ya kupata habari hizo kutoka kwa shushushu wake. Ndip mkuu..alisema mtumishi.. Faritha na wenzie bila kuchelewa waliagiza wapambanaji mashuhuri wawili kumfuatilia Rania.. SASA ENDELEA.. Wale watu waliondoka kwa kasi kubwa sana kuhakikisha wanamkamata Rania maana ndio kiapo walichokula mbele ya Faritha. Walitembea kwa kasi hadi wakafika kijiji alichokuwepo Rania maana Rania alikua na mwendo mdogo kwa kua alizani hakuna wa anaemfuata nyuma. Akiwa ndani mara Hanna alikuja huku akihema sana.. Rania, nimewaona watu wa Faritha hapa kwenye eneo hili. Bila shaka wamekufuata wewe...tufanye haraka tuondoke..alisema Hanna. Haaa...wamejuaje?.aliuliza Rania kwa mshangao.. Hatuna muda wa kusitasita wala kujiuliza maswali Rania, haraka tuondoke.. Alisema hanna. Sawa..alisema Rania na bila kupoteza muda waliondoka mahali pale. Wale watu wa Faritha wakiwa kwenye mizunguk…