
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Nini wewe?..Rania hayupo kwenye kasri ameondoka?. Aliuliza Faritha kwa hasira baada ya kupata habari hizo kutoka kwa shushushu wake.Ndip mkuu..alisema mtumishi..
Faritha na wenzie bila kuchelewa waliagiza wapambanaji mashuhuri wawili kumfuatilia Rania..
SASA ENDELEA..
Wale watu waliondoka kwa kasi kubwa sana kuhakikisha wanamkamata Rania maana ndio kiapo walichokula mbele ya Faritha.Walitembea kwa kasi hadi wakafika kijiji alichokuwepo Rania maana Rania alikua na mwendo mdogo kwa kua alizani hakuna wa anaemfuata nyuma.
Akiwa ndani mara Hanna alikuja huku akihema sana..
Rania, nimewaona watu wa Faritha hapa kwenye eneo hili. Bila shaka wamekufuata wewe...tufanye haraka tuondoke..alisema Hanna.
Haaa...wamejuaje?.aliuliza Rania kwa mshangao..
Hatuna muda wa kusitasita wala kujiuliza maswali Rania, haraka tuondoke.. Alisema hanna.
Sawa..alisema Rania na bila kupoteza muda waliondoka mahali pale.
Wale watu wa Faritha wakiwa kwenye mizunguko ya kuwatafuta mara waliona msafara na watu wale walikua wamevaa mavazi ya watumishi wa ikulu ya nchi ya Lazi
Wale paleee..hakikisha hatuwakosi...alisema mmoja kati ya watu wale .
Wale watu walianza kuufuatilia msafara ule kwa kasi. Muda mfupi baadae waliufikia msafara huo.. Bila kuchelewa waliukinga kwa mbele.
Hawakuamini macho yao baada ya kuona Rania hakuwepo kwenye msafara huo...
Semeni haraka..Rania amepitia njia gani kuondoka??. Waliuliza watu wale kwa ukali...
Rania hajaondoka bado yupo hapa kijijini..alisema mtu mmoja katika msafara.
Nini?.. Kwahyo mnataka kutufanya sisi vichaa?..Yaan amebaki nyuma halafu nyinyi mnaenda wapi?.. Aliuliza mmoja wa watu wale.
Wale watu wa Rania wakaanza kuogopa na kutetemeka sana..
Haya sema alipoenda haraka sana...alisema mmoja wa watu wa Faritha huku amemkaba mtu wa Rania shingoni.
Amepita njia ile kule...alisema mtu yule kwa kuogopa kukatwa shingo..maisha matamu jamani ohooo😋
Watu wa Faritha waliifuata njia ile kumkimbiza Rania.
Huku Rania alikua bado hata hajatoa mguu pale kijijini
Wakati akiwa njiani na watu wake aliwaambia kua anabadili njia ili watu wa Faritha waufuatilie msafara halafu wamkose Rania.
Lakini alipohakikisha wenzie wa msafara hawamuoni ghafla alibadili njia na kurudi kijijini tena.
Rania, mbona ghafla tumeahirisha safari na kurudi?..aliuliza Hanna.
We hujajua Hanna.. Wale watu ni waoga sana,hawawezi kuhatarisha maisha yao eti kisa kuficha nilikopita..mimi najua tu ikitokea watu wa Faritha wakawakamata lazima watasema yote.. Alisema Rania
Mmmh..sasa mbona umewaambia ukweli kwamba waseme hujaondoka hapa?..si umgewaambia uongo mwingine?. Alisema hanna.
Watu hua hatupendi kuamini ukweli.. Hivi hata wewe ungekua wale watu wa Faritha ungekubali eti sijaondoka..halafu msafara wangu wanaondoka kwenda wapi bila mimi?...aliuliza Rania.
Mmmh..ila kweli..alisema Hanna.
Najua wanazani nimepita njia tofauti, na wananitafuta kwa sasa...sasa mimro nitapitia huku chinichini nielekee Tharia maana watu wale waoga wanaweza hata kusema nchi ninayoelekea..sasa hapa nabadili upepo....alisema Rania.
Usiku ulipoingia Rania, hanna na mlinzi mmoja wa kuaminika walipita njia tofauti sana na kuelekea Tharia badala ya kwenda katika nchi ya lashfa.
Walipita misitu minene sana na ya kutisha lakini hawakua na namna..usiku ulikua mrefu sana kwao.. Waliingoja asubuhi kama walinzi wa zamu😨
Ndani ya siku chache walifika Tharia..
Woooow...mazingira mazuri kweli Jaman.. Miaka mingi sana imepita tangu niondoke hapa...pamebadilika sana hapa..alisema Rania
Rania na wenzake walinunua nyumba ya kuishi maana Mfalme alimpatia Rania pesa na madini mengi sana ya kutosha kumhifadhi maisha yake yote.
Shenzi kweli... Sasa unazani tutarudi vipi kwa faritha ilihali tumeshindwa kumkamata Rania?. Aliuliza mmoja wa wale watu wa Faritha (kiza)..
Kweli yaani.. Tuliapa kwamba hatutarudi bila Rania.huyunp mama atatumeza kabisa.. Mimi naona bora tutokomee hukuhuku...alisema Fuma.
Kweli.. Kama vipo twende nchini kwetu Tharia.. Ila sijui tutafikia wapi..alisema kiza.
Hayo tutajua huko mbele muhimu twende tu.. Alisema fuma.
Walikubalina na wakaenda zao Tharia kula bata
Siku nyingi zilipita bila kiza na fuma kurudi.
Hakika huyu Rania anabahati sana..wamemkosaje hawa wapiganaji mashuhuri?...alisema Faritha.
Yule Rania ni mjanja..itakua amewakwepa.. Alisema waziri
Sasa kwanini hawajarudi...alisema Faritha.
Sijajua lakini itakua waliogopa kua tutawaadhibu...lakini wale watu walikua muhimu sana kwetu..alisema Azza.
Rania na wenzake waliishi Tharia kwa amani kwa mudavwa miezi mitatu.
Siku moja wakiwa wanatembea tembea mara walikuja askari wa ikulu wakimtafuta dada mmoja ambae alikua mtumishi wa ikulu na inasemekana aliiba baadhi ya vitu vya thamani ikulu na kukimbia navyo...
Wakiwa wanamtafuta mara Rania a na wenzake walisikia..huyo hapo kamataaaa..
Wote walishtuka kusikia hivyo na alikua akinyoishewa kidole alikua Rania.
Mimi???!!! Nimekuaje?.. Alijiuliza Rania kwa mshtuko mkubwa..
Kimbia Rania, watakukamata..alisema hanna.
Nikimbie nini sasa..sijafanya kitu mim.. Alisema Rania.
Wewe hayo utayajua baadae sasa hivi tukimbie tu..alisema Hanna huku akimvuta Rania mkono na kumlazimisha kukimbia.
Rania, Hanna na yule mlinzi wa kuaminika (Namadi) walianza kukimbia bila hata kujua sababu..
Kilichofanya Rania akimbizwe ni kwamba alikua amevaa nguo kama za mwizi yule.sasa walipomuona yeye wakaza ni ni yule mwizi..
Walikimbia sana lakini askari wale walikua na kasi sana na waliwakaribia.
Rania pita njia nyingne ya uchochoroni sisi tutawapoteze huku.. Alisema hanna.
Hanna na Namadi waliwachezea mchezo wale askari hadi wakapoteza uelekeo na wakampoteza Rania..
Wale maaskari walilaani sana na kujitahidi kumtafuta mwizi bila mafanikio.
Rania alikatiza njia ya uchochoroni na kujikuta akiteleza na kuangukia kwenye shimo moja pana sana ingawa halikua refu sana..ila lilikua refu kidogo.
Mamaaa...alipiga kelele Rania kwakua aliteleza..
Humo kwenye hilo shimo alikuemo mtu ambae yeye aliingilia upande wa pili wa shimo ambako kuna mteremko mdogo.
Alisikia kelele za Rania na kumwona jinsi anavyotaka kuanguka..
Mtu yule aliwahi na kumdaka Rania na wote wakaanguka ingawa kwa kasi ndogo sana wala hawakuumia.
Rania alifumbua macho Baada ya kunusurika ajali ile...
Mtu yule hakuamini macho yake baada ya kumwona Rania.. Alishtuka sana,akashangaa na akajihisi labda ni ndoto tu..
Au nimemfananisha maana ni miaka mingi imepita bila kumwona..alijiuliza mtu yule huku amemkodolea macho Rania.
Dom!!!!!...aliita Rania baada ya kumwangalia vizuri mtu aliemwokoa.
Huh.. Dom..aliita Rania mara ya pili akiwa haamini macho yake.
Rania!!!!... Kwahyo huyu ni Rania!!!...alijisemea Dom moyoni akiwa haamini macho yake.
Mmh..inaonekana nimekufananisha labda.. Alisema Rania baada ya kuona Dom haongei anashangaa tu.
Rania.... Aliita Dom kwa kigugumizi
Ndio..ni mimi Rania.. Alisema Rania kwa furaha.
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO