RANIA (11)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Rania!!!!... Kwahyo huyu ni Rania!!!...alijisemea Dom moyoni akiwa haamini macho yake. Mmh..inaonekana nimekufananisha labda.. Alisema Rania baada ya kuona Dom haongei anashangaa tu. Rania.... Aliita Dom kwa kigugumizi Ndio..ni mimi Rani1a.. Alisema Rania kwa furaha... SASA ENDELEA.. Wee..mbona unaniangalia namna hiyo kama unaangalia maiti?..aliuliza Rania baada ya kuona Dom amemshangaa kwa muda mrefu. Rania... Kumbe ulikua hai muda wote... Alisema Dom. Ulizani nimekufa?...mimi nipo...alisema Rania. Dom alimkumbatia Rania kwa nguvu sana huku machozi ya furaha yakimtoka. Rania, nashukuru sana umerudi..hatimae naweza kua na furaha tena...alisema Dom. Hata mimi nafurahi sana Dom...alisema Rania. Walitoka shimoni kwa kupitia njia ya upande wa pili. Huku Hanna na Namadi walikua wakimtafuta Rania baada ya kuwakwepa maaskari wa ikulu Baada ya kuzunguka sana kwa muda mrefu walimwona Rania akiwa na Mtu wasiemfahamu...anacheka meno 32 nje h…