RANIA (11)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Rania!!!!... Kwahyo huyu ni Rania!!!...alijisemea Dom moyoni akiwa haamini macho yake.

Mmh..inaonekana nimekufananisha labda.. Alisema Rania baada ya kuona Dom haongei anashangaa tu.

Rania.... Aliita Dom kwa kigugumizi

Ndio..ni mimi Rani1a.. Alisema Rania kwa furaha...

SASA ENDELEA..
Wee..mbona unaniangalia namna hiyo kama unaangalia maiti?..aliuliza Rania baada ya kuona Dom amemshangaa kwa muda mrefu.

Rania... Kumbe ulikua hai muda wote... Alisema Dom.

Ulizani nimekufa?...mimi nipo...alisema Rania.

Dom alimkumbatia Rania kwa nguvu sana huku machozi ya furaha yakimtoka.

Rania, nashukuru sana umerudi..hatimae naweza kua na furaha tena...alisema Dom.

Hata mimi nafurahi sana Dom...alisema Rania.

Walitoka shimoni kwa kupitia njia ya upande wa pili.

Huku Hanna na Namadi walikua wakimtafuta Rania baada ya kuwakwepa maaskari wa ikulu

Baada ya kuzunguka sana kwa muda mrefu walimwona Rania akiwa na Mtu wasiemfahamu...anacheka meno 32 nje hana hata habari.

Jamani Rania sisi tunahangaika kumtafuta kumbe yeye hana hata habari.. Alisema hanna akiwa ameshika kiuno kwa uchovu..

Waliondoka na kuelekea alikokua Rania.

Rania... Aliita Hanna baada ya kufika alipo Rania.

Aaah...Hanna..huyu ni rafiki yangu anaitwa Dom.. Alisema Rania huku akimshika Dom kwenye bega.

Haya twende sasa mmeshaonana...alisema Namadi.

Aaah...sasa hivi tu...bado hatujamaliza kuongea.. Alisema Rania.

Wote walikaa hapo na kuanza kuongea mawili matatu..

Waliongea muda mrefu sana baadae wakaagana na kika mmoja kwenda kivyake

Dom alikua na furaha sana siku hiyo hadi mama yake akawa anamshangaa.

Dom... Aliita mama yake Dom.

Naaaaaam...aliitika Dom kwa mbwembwe.

Mmh...leo umekula nini huko mbona unafuraha kiasi hiki?.. Aliuliza mama yake Dom.

Aaah.. Mama..kawaida tu..alisema Dom.

Niambie bwana,tangu lini tunafichana?..aliuliza mama yake Dom

Mama...nimemwona Rania, kumbe hakufa..yuko hai mama..alisema Dom kwa furaha.

Haaaa....Mungu ni mwema sana...afazali hata umeonana nae nitapumzika hapa nyumbani.. Alisema mama yake Dom.

Mama na wewe umeanza...alisema Dom..wote walicheka na maisha yakaendelea.

Halafu Dom nataka nimwone Rania... Nataka nihakikishe kama ni mzuri kunishinda mimi nilipokua binti.. Alisema mama yake Dom.

Mama nawe..alisema Dom.

Kesho yake Dom alikwenda kwa Rania ba kumweleza hitaji la mama yake.

Wow.. Twende hata sasa hivi.. Alisema Rania kwa mapepe.

Walienda hadi kwao Dom.

Karibu jamani Rania, ingia ndani jamani,Dom hata akibaki nje haina shida. Alisema mama yake Dom huku akimwingiza Rania ndani.

We mrembo kweli kama Dom alivyosema..alisema mama yake Dom.

Alisema!!!?..aliuliza Rania kishankupe.

Hamna bwana...alikana Dom.

Wee...ulisema..alikazia mama yake Dom.

Rania alishinda huko siku hiyo wakopifa storybna mama wa Dom na Dom mwenyewe.

Baadae Dom alimrudisha Rania nyumbani.. Wakiwa njiani wanaenda Rania akaanza..

Jamani mimi mrembo.. Alisema Rania huku akijigeuza geuza.

Nani kasema.. Alisema Dom.

Wewe umesema...mi mrembo kweli.. Alisema Rania.

Dom akicheka tu maana sio kwa mcharuko huo.

Hatimae walifika sehem ambayo Rania anaweza kwenda peke yake akafika nyumbani.

Haya Rania.. Nenda sasa...alisema Dom.

Asante Dom.. Safari njema.

Rania aliondoka zake..Dom alikua akimsindikiza Rania kwa macho.

Dom...bado upo.. Unanishangaa mimi mrembo wa mtaaa? Aliuliza Rania baada ya kuona Dom bado hata hajaondoka alipomwacha.

Dom alikurupuka na kuanza kwenda kwao huku njia nzima Rania anazunguka kichwani

siku nyingne tena Rania na wenzake walikua wakila mitaa huku na kule. Wakiwa njiani walikutana na askari wa ikulu..

Askari wale walikua wanatangaza jambo fulani:

TANGAZO!!!!!

Juma lijalo kutakua na na sherehe ya kuzaliwa kwa Mwanamfalme Fasha.. Kwahyo watu weye vipaji mbalimbali wanakaribishwa kuhudhuria.watakaojitolea kuburudisha waje wajiandikishe na watachujwa ili kuchagua wachache watakao fanya vyema kwenye sherehe.

Mshindi kwenye kila burudani atapewa zawadi kubwa sana..wote mnakaribishwa..

Heeee.. Zawadi.. Itakua hela hizo.. Siwezi kuacha hela zipite Rania mie jamani..ngoja nikatengeneze shairi moja matata...nataka hela mimi jamaniiiiii...alisema Rania huku akirudi nyumbani kwa kasi kuandaa shairi..

Daaah..yaani hiyu mapepe kweli kweli.. Alisema hanna huku anatikisa kichwa..

Walianza kumtafuta nyuma maana hawana jinsi..ndo alivyoumbwa.

Rania alifika nyumbani na bila kuchelewa alianza kuandika shairi lake..

Muda sio mrefu Hanna na Namadi walifika.

Rania hakula siku nzima anatunga shairi....alikua anabadili mkao kila baada ya dakika mbili...shari lenyewe fupi kweli.

Baada ya kuhangaika siku nzima Rania alitunga shairi aliloliona yeye kua ni zuri sana.

Haya nimemaliza kutunga.. Yaaani hapa nitakua nahesabu hela tu mimi...oooh mambo matamu hayataki haraka.. Alijisemea Rania.

Hebu lete hapa na mimi nisome...alisema Hanna.

Mmmhhh....hili shairi hata sio zuri..mimi silielewi..Alisema Hanna baada ya kulisoma.

Jinga nini....hata hivyo wewe sio lazima ulipende lakini mwanamfalme atalipenda...alisema Rania.

Siku ya mchujo iliwadia..siku hiyo Dom alikuja kumtembelea Rania.

Rania alimweleza kua atashiriki mashindano kitengo cha mashairi...

Kweli?.. Aliuliza Dom.

Kweli.. Nataka nipate hela..yaani nisiposhinda hata senti moja watanijua...sherehe nitaigeuza chungu..alisema Rania.

Hahaaa...sasa kama umeandika visivyoeleweka ushinde?..alisema Dom.

We..ni vyakueleweka..alisema Rania.

Leta nione..alisema Dom.

Dom alilisoma shairi lile.. Aliliona zuri ingawa lilimfanya ajisikie vibaya kua Rania anamkumbuka saba Fasha kuliko yeye..ila alikaushia tu akalisifia.

mmmh..hakika mwanamfalme lazima afurahi...utashinda Rania.. Nina hakika utashinda..alisema Dom.

Asante Dom... Alisema Rania.

Walitembea muda mrefu wakiongea na baada ya hapo Rania alielekea kwenye mchujo.

Baada ya mchujo Rania alitemwa jamani daaah..

Jamani we mwamuzi naomba uniruhusu.. Nakwambia lazima nishinde..we utaona mwanamfalme atalipenda shairi langu ingawa wewe hulipendi....nikishinda nitakupa zawadi kubwa..alisema Rania huku kamkamatilia mwamuzi mkono kwa nguvu.

Wewe hebu niache..alisema mwamuzi kwa ukali.

Rania alimbembeleza sana mwamuzi.

Haya...nakupitisha..najua utashindwa tu wewe huko mbele..alisema mwamuzi.

Rania alifurahi sana..alirudi nyumbani na kuwasimulia wenzie.. Tena akawadanganya kua amepita kirahisi kumbe kabembeleza kwa sana tu😹.
****

Siku ya mashindano ilifika na watu wote wakiongozwa na mwanamfalme Fasha walikua tayari kusikiliza na kuangalia burudani.

Vikundi mbalimbali vya michezo vilipita na hatimae ikafika zamu ya mashairi.

Kulikua na vukundi viwili vya mashairi..Rania alikua peke yake na aliwekwa wa mwisho kuburudisha maana yule mwamuzi alimwona hana la maana sana.

Wote waliimba na kushangiliwa na watu.

Hatimae zamu ya Rania ilifika..

Rania aliingia uwanjani akiwa amejifunika kitambaa cheupe chenye matundu madogo madogo..

Kila mtu alimshangaa maana hata hakua na shamrashamra zozote...

Alifika na kutoa heshima mbele ya meza kuu na kuanza kuimba

"Nilizani ni adui,nilipouona mwanzo"
"La nilikua sijui ,tulipokutana mwanzo"
"Kumbe mwanga si adui, yalikua tu mawazo"
"Siku njema iliyoje, mwanga uliyozaliwa"

"Mwanga uliniokoa,msituni kwenye giza"
"Pale walipopania,mimi kunimaliza"
"Hata sikufikiria, kama ungenipoza"
"Siku njema iliyoje,mwanga uliyozaliwa"

"Katika dimbwi la maji,ulininusuru kifo
" sikua mwogeleaji, hata niepuke kifo"
"Wawili waokoaji,waliepusha kifo"
"Siku njema iliyoje, mwanga uliyozaliwa..

" alikwenda ugenini,miaka imeshasonga"
"Na sasa yuko nyumbani, bado haujamtambua?"
"Hajakwenda ardhini,kama ulivyosikia"
"Yupo hapa hadharani,nawe wamshuhudia"

Rania aliimba shairi hilo fupi na kukaa kimya.

Fasha alibaki anashangaa na kujiuliza ni nani hasa aliekua anaimba.

Msituni?..kwenye dimbwi la maji mwanga ulimwokoa?...ni Rania huyu au ni mawazo yangu yananipotosha...alijisemea Fasha.. Hakuweza kumtambua Rania maana Rania alikua ameziba usoni kwa kitambaa.

Rania.. Ni Rania... Kumbe Rania hajafa..alitahamaki Fasha.

Hakuna aliekua akielewa shairi lile katika watu wote waliokua pale tofauti na Fasha,Rania mwenyewe na Dom.

Hivi wewe umeelewa hilo shairi?..aliuliza mwamuzi mmoja wa mashindano.

Hata halieleweki....anapata 2% huyu...shairi lenyewe fupi kama miguu ya fisi ya nyuma...alisema mwamuzi

Haha..unamatusi wewe..alisema mwenzie.

Baada ya hapo waliamuliwa kuondoka na baada ya masaaa mawili wataitwa kusoma washindi.

Rania alienda moja kwa moja alipokua Dom.

Dom...nimemba vizuri eee..aliuliza Rania kwa kiherehere.

Umeimba vizuri.. Alisema Dom ila si kwa uchangamfu

Dom... Nimeimba vibaya ee..mbona unaitikia kinyonge?...aliuliza Rania.

Rania... Aliita Dom..

Abeee..aliitika Rania kwa mashaka.

Dom alibaki amemwangalia Rania bila kusema kitu.ila macho yake yalikua yakisema kitu.

Aaah.. Nimejua kumbe...nimejua ninachokufanya unune...alisema Rania.

Dom alibaki kimya tu..akiwa amepoa sana.

Lakini Dom, wewe umenisaidia mara nyingi...nitaandaa siku nzuri kwa ajili ya kukushuru. Usiwe hivyo bwana..alisema Rania kisha Dom akamkatisha..

Wala sina hayo mawazo...lakini Rania,huenda mwanamfalme hatakuacha urudi unapoishi atakutaka ukae ikulu...unazani mimi nitafanya nini Rania.

Haa....hawezi bwana..atafanyaje hicho kitu?... Alisema Rania kujihami.

Rania, utakataa amri ya kifalme?.. Hujui kua unaweza kufa kwa hilo kosa? Alisema Dom huku akimwangalia Rania kwa wasiwasi.

Rania alimsogelea Dom na kumshika mikono yake yote miwili.

Dom..usiwaze hayo..haitatokea sawa eee..alisema Rania kumwondoa Dom wasiwasi.

Dom alikaa kimya tu maana yeye aliwaza yatatokea.

Kwaheri Dom naenda kwa Hanna na Namadi.. Tutaonana baadae... Alisema Rania na kuanza kuondoka.

Kabla hajapiga hatua hata mbili Dom alimvuta akamkumbatia.

Rania, unatakiwa urudi...nakuomba.. Alisema Dom.

Nitarudi Dom.. Siendi mimi popote..alisema Dom akiwa amepakatwa😜😍.

Muda wa kutoa tuzo na zawadi ulifika na wasanii wote walikwenda.

Kila kitengo alisomwa mshindi na kupewa zawadi yake.

Kwenye upande wa mashairi walipewa tuzo watu wengine tu mbali na Rania. Rania alijisikia vibaya maana liona amefanya kazi bure na hajaambulia hata senti.

Ulifika muda wa mwenye sherehe yake kuchagua nani alimfurahisha zaidi..na mshindi huyo ndo alihesabiwa kua mshindi mkuu.

Fasha alisimama na kusema "mtu alieniburudisha kuliko wote ni alieimba shairi akiwa peke yake na akiwa wa mwisho"

Watu wote walibaki wanashangaa maana wao waliona kua ndie aliefanya vibaya zaidi.

Rania alijitokeza na kuchukua zawadi yake hivyo hivyo ameziba uso.

Fasha aliomba kuonana na Rania.

Walipokua peke yao Fasha alimwomba Rania afunue sura yake ba Rania alifanya hivyo.

Fasha hakuamini macho yake... Alifurahi kupita kiasi kuona Rania yupo hai tena..kwa Furaha alimkumbatia ingawa Rania hakuonesha ushirikiano.

Fasha aliporidhika alimwachia.

Rania, aliita Fasha...

Baki hapa ikulu na mimi Rania... Alisema Fasha.

Heeee..nini?. Nibaki hapa?..alisema Rania kwa mshtuko..NINI KINAFUATA?

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MBILI

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni