RANIA (12)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Fasha hakuamini macho yake... Alifurahi kupita kiasi kuona Rania yupo hai tena..kwa Furaha alimkumbatia ingawa Rania hakuonesha ushirikiano. Fasha aliporidhika alimwachia. Rania, aliita Fasha... Baki hapa ikulu na mimi Rania... Alisema Fasha. Heeee..nini?. Nibaki hapa?..alisema Rania kwa mshtuko.. SASA ENDELEA.. Rania, tafazali naomba ubakie hapa na mimi..alisema Fasha huku akimwangalia Rania usoni. Hapana mwanamfalme, siwezi kubakia hapa..alisema Rania. Kwanini usiweze?...miaka imeshapita..walipokutafuta bila shaka walikufa vitani,unahofia nini?..aliuliza Fasha. Hata kama..siwezi bado kubakia hapa..nia yangu ilikua kupata hela na si vinginevyo..kuna watu wananitegemea..alisema Rania Kama ni hilo tu basi mimi nitawahudumia kwa watakachokitaka chochote.. Alisema Fasha. Uwepo wangu kwao ndo nachomaanisha..alisema Rania. Dom?...aliuliza Fasha Rania alishtuka kidogo... Ila hakujibu swali lile. Kwaheri mwanamfalme, tutaonana siku nying…