RANIA (12)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Fasha hakuamini macho yake... Alifurahi kupita kiasi kuona Rania yupo hai tena..kwa Furaha alimkumbatia ingawa Rania hakuonesha ushirikiano.

Fasha aliporidhika alimwachia.

Rania, aliita Fasha...

Baki hapa ikulu na mimi Rania... Alisema Fasha.

Heeee..nini?. Nibaki hapa?..alisema Rania kwa mshtuko..

SASA ENDELEA..
Rania, tafazali naomba ubakie hapa na mimi..alisema Fasha huku akimwangalia Rania usoni.

Hapana mwanamfalme, siwezi kubakia hapa..alisema Rania.

Kwanini usiweze?...miaka imeshapita..walipokutafuta bila shaka walikufa vitani,unahofia nini?..aliuliza Fasha.

Hata kama..siwezi bado kubakia hapa..nia yangu ilikua kupata hela na si vinginevyo..kuna watu wananitegemea..alisema Rania

Kama ni hilo tu basi mimi nitawahudumia kwa watakachokitaka chochote.. Alisema Fasha.

Uwepo wangu kwao ndo nachomaanisha..alisema Rania.

Dom?...aliuliza Fasha

Rania alishtuka kidogo... Ila hakujibu swali lile.

Kwaheri mwanamfalme, tutaonana siku nyingine..alisema Rania na kuanza kuondoka.

Fasha alimvuta Rania na kumrudisha.

Huwezi kwenda Rania.. Alisema Fasha.

Siwezi kubakia hapa Fasha... Alisema Rania.

Ni amri ya kifalme sio ombi..alisema Fasha.

Basi mimi nakiuka kama ukipenda niue..alisema Rania.

Rania... Utanisamehe kwa hili nitakalokufanyia.

Jao...mpeleke Rania chumba cha peke yake umfungie huko..alisema Fasha.

Nini???? Anifungie?..aliuliza Rania

Jao na walinzi wenzie bila kuchelewa alimkamata Rania na kumpeleka mkikimkiki chumbani.

Niache...we Fasha ngoja hunijui...alilalama Rania njiani.

Hatimaye walimfikisha walikoagizwa na kumfunga mikono,miguu na mdomo ili asilete fujo.

Rania alikasirika sana nusu apasuke.

Dom na wenzake, Hanna na Namadi walikua wakimsubiri Rania muda wote huo.

Mbona haji?..aliuliza Hanna.

Kama tu nilivyowaza..Fasha atakua kamzuilia kuja..alisema Dom kwa sauti ya chini.

Umesemaje?..aliuliza Hanna.

Aaah..hamna kitu.. Alisema Dom kisha akaanza kuondoka polepole.

Unaenda wapi?...aliuliza Hanna.

Dom aliendelea kuondoka kwa unyonge sana.

Mwanamfalme.. Mbona umemfanyia hivyo Rania?.. Unazani atakuelewa?..aliuliza jao.

Rania akibaki huko mtaani ni hatari kwake maana atauawa halafu yeye hajui lolote.

Hata sasa hivi bila shaka mganga ameshajua uwepo wa Rania hapa ikulu... Nitampeleka mafichoni akakae huko na na hakuna mtu atajua..alisema Fasha.

Mmmh...sasa hujui kua uwepo wake unahatarisha ufalme huu?.?alisema jao.

Mimi hata hainihusu maana Mimi si wa hapa..sasa nikose ufalme na Rania pia?..aliuliza Fasha.

Mmmh... Ngoja tujitahidi tuone...alisema Jao.

Usiku ulipoingia Fasha alikwenda kumwona Rania.alipoingia ndani tu Rania alimwangalia jicho la hasira kweli kweli

Rania, najua umekasirika lakini sikufungulii hadi nimalize kukwambia yafuatayo maana wewe nakuelewa.

Siku ile msitini waliokua wanakuwinda waliagizwa na mfalme.. Sijui kivipi lakini inasemekana kua wewe utakuja kuupokonya mfalme huu mikononi mwa familia yetu. Sasa unatafutwa uuawe..alisema Fasha.

Nakuomba uwe mpole tu nikupeleke mafichoni maana hata sasa hivi tu tayari unatafutwa maana wewe ukikanyaga hapa tu ikulu mganga anajua..utakaa hapa hadi nipate jinsi ua kukutorosha..alisema Fasha.

Baada ya maneno hayo Fasha alimfungua Rania mdomo.

Rania alikua ametumbua macho kwa habari alizosikia.

Mwanamfalme, wewe ndo umesababisha hadi sasa wananisaka maana ungeniachia mapema ningeshaondoka..alisema Rania.

Rania, unapokanyaga tu ikulu tayari mganga anajua..walikua washaweka walinzi wa kukuzuia kuondoka kwa kisingizio umeimba vizuri hivyo uonane na mfalme... Umefanya la maana sana kuziba uso wako.. Alisema Fasha.

Fasha... Sio kwamba na wewe ni walewale?..kama mimi nina asili ya kupokonya ufalme wenu kwanini unilinde..nahisi na wewe unataka ukanifyekelee mbali.. Alisema Rania.

Kuna kitu hujajua bado, ukikijua hicho utajua kwanini nafanya hivi wakati ninatakiwa kukuaa.

Fasha, kama unahitaji kuniua tafazali niache niwaone marafiki zangu.. Alisema Rania.

Dom?.. Aliuliza Fasha kwa wivu.

Ndio, ila sio yeye tu na wengine wawili..alisema Rania.

Fasha alikaa kimya kwa muda kisha akasema, nitawaleta wale wawili tu wakuone kabla hujaenda mafichoni.. Alisema Fasha

Tafazali.... Nakuomba mwanamfalme.. Dom ata...alisema Rania kabla hajaendelea.

Hivi Dom ni kila kitu kwako?..aliuliza Fasha akiwa amepoa.

Rania alinyamaza kwa muda kisha akasema.
Nakuomba tafazali... Niletee Dom.

Rania, mbona mimi niko hapa?..alisema Fasha.

Wewe ni wewe na Dom ni Dom.. Wote nyie ni muhimu kwangu..alisema Rania.

Fasha aliondoka bila kumpa Rania jibu lolote lile .

Rania alibakia mwenye mawazo..kichwani mwake hakuamini kama kweli Fasha anampango wa kumsaidia...aliwaza huenda nae ndio walewale tu kina Mfalme.

Usiku ulipofika Fasha alimtoa Rania nje ya ikulu na kumpeleka mafichoni kwa siri kubwa mno.

Baada ya muda mrefu walikua wameshafika mafichoni. Rania alikaa ingawa kwa wasiwasi mkubwa.

Dom sijui anajisikiaje huko aliko..ningejua nisingekuja Tharia haya yote yangetoka wap?..najuta..alijisemea Rania.

Rania akiwa anawaza Mara aliingia Fasha.

Mwanamfalme, kwanini huwaleti rafiki zangu?. Aliuliza Rania kwa pupa.

Haitawezekana Rania.. Hii ni sehem ya siri.. Siwezi kumwamini yeyote aje hapa. Alisema Fasha.

Unafanya hivi ili tu Dom asije?. Aliuliza Rania.

Rania... Hivi huwezi kuacha kumwongelea Dom mbele yangu?..aliuliza Fasha.

Rania alimwangalia vibaya akanyamaza tu.

Huku ikulu tabu si tabu tena..Mfalme na watu wake walikua wanamtafuta Rania kwa udi na uvumba..Mganga alisimama kwenye njia zote wanazopita watu waliokua kwenye sherehe lakini hakumwona Rania.

Mara ghafla aligundua kua Rania ameshaondoka tayari..

Amepita wapi?...alijiuliza Mganga

Baadae mganga alirudi kwa Mfalme na kumtaarifu kua NADISH haipo tena na hajui alikopotia.

Mnawezaje kufanya uzembe kiasi hicho?.. Alifoka Mfalme.

Nisamehe sana Mfalme sitarudia. Alisema mganga.

Kurudia?..lini hiyo unasema hutarudia?...hii nafasi unahisi itajitudia tena?..aliuliza mfalme kwa hasira.

Mganga alikaa kimya...

Nini????...haujamkamata?..alifoka malikia suya.

Nisamehe sana malikia.. Inaonekana kuna mtu kamsaidia kuondoka hapa...asingeweza kwenda mwenyewe wakati nilitega dawa kila njia ya kutokea ikulu.. Alisema mganga.

Malikia suya alishusha pumzi kutafakari huyo aliemsaidia ni nani.

Unahisi ni nani?..aliuliza malikia suya.

Sijui kwa sasa....Naomba unipe muda nichunguze. Alisema mganga.

Nakupa wiki moja..tunaelewana?. Alisema malikia suya

Sawa malikia.. Alijibu Mganga.

Mama yake Dom alikua amekaa anawaza sana.

Maskini mwanangu Dom. Sijui mkosi gani huu...Rania ninmtu mwenye safari ndefu na ngumu.. Dom wangu akijarubu kumsaidia si atakufa? Alijisemea mama yake Dom.

Mama yake Dom (Rai) aliwahi kua msaidizi wa mganga zamani.

Habari za NADISH anazijua kama zote.siku Rania anakuja pale mama yake Dom tayari alimjua..hakutaka kujionesha kama ameshtuka ili asiwanyime amani watoto.. Ila walipoondoka tu aliwaza sana na alishangaa sana.

Dom alipofika kutoka kwenye sherehe alikua amepoa sana.

Mwanangu, umekuaje? Aliuliza mama yake.

Doma alikaa chini na kumwambia mama yake anahisi huenda Fasha akawa amemkatalia Rania maana hajarudi hata sasa.

Kwani ameshinda mchezo wowote?..aliuliza mama yake Dom.

Hapana hakupewa tuzo na waamuzi ila mwanamfalme mwenyewe ndo kampa eti amemfurahisha sana...alisema Dom.

Rai (mama yake Dom) alihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikua hivyo.

Mama..mbona umekua hivyo?.. aliuliza Dom Baada ya kuiona hali ya mama yake.

Mwanangu, Rania atakua hatarini sasa..alisema Rai.

Kwanini mama?..aliuliza Dom.

Rai alimweleza yote Dom kuhusu Rania na ufalme.

Haaa...mama!!!!alisema Dom kwa mshangao

Kweli mwanangu... Na mimi ndo nilipewa jukumu la kumlinda..na sasa nimeshindwa...alisema rai.

Mama...nitafanya lolote lile nimsaidie Rania.. Alisema Dom.

Utafanya nini mwanangu wakati wale ji watawala?..aliuliza rai.

Mama...usijali...siwezi nikamwacha Rania afe kizembe...kwa vyovyote vile nitampata..alisema Dom.

Baada ya hapo Dom alitoka na kwenda msituni kukaa akiwaza atafanya nini.

Rania, kama tu nilivyohisi Fasha amekukatalia..nitafanya nini mimi..?aliwaza Dom.

Dom akiwa amekaa hapo mara alikumbuka Hadithi ambayo mama yake alimsimulia..hakika ilimsumbua sana na ilimuumiza kichwa na akakosa raha

Akiwa amekaa hapo mara alifika mtu na kusimama pembeni yake

Dom aligeuka na kumtazama aliesimama na kukuta ni mwanamfalme.

Alisimama na kumpa heshima yake kisha akasema:
Mwanamfalme, Rania yuko wapi?.

Nimekuja hapa kukutaarifu kua hata siku moja usiote kua na Rania.. We potezea tu na ufuate maisha yako mwenyewe.. Alisema Fasha.

Dom aliumizwa Sana na majibu ya mwanamfalme.

Siwezi kufanya unavyotaka mwanamfalme.. Utanisamehe tu.. Alisema Dom.

Kwahyo unataka kusema utamtafuta Rania hadi umpate?..aliuliza Fasha.

Sijui...ila sewezi kupoteza kama ulivyosema....alisema Dom

Unazani utaweza kunishinda? aliuliza Fasha.

Sijui ila nina hakika nitampata Rania...alisema Dom

Fasha alimsogelea Dom karibu kisha akamwambia

Dom.. Rania hatarudi kwako hata siku moja..nakuomba umsahau..wewe huna uwezo wa kumlinda Rania...anatakiwa kuwa na Mimi ili awe salama.

Usalama?.. Au kifo?..alisema Dom.

Fasha alishtuka sana kusikia hivyo.

Unamaana gani kusema kifo? Aliuliza Fasha.

Bila shaka unajua Rania anamaanisha nini kwenye ufalme wenu....kwahyo unataka umuue kimyakimya kwa kisingizio kua umemficha umlinde?.. Hautaweza Fasha...alisema Dom huku amemkazia Fasha macho.

Fasha alishtuka na macho yalimtoka ...Nini kinaendelea?..

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TATU

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni