
SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Hatimaye siku ya mapambano ilifika..mpambanaji alikuja na kinyago uwanjani..mwanamfalme nae alikua amejiandaa sawa sawa.Muda wa pambano ukafika na Dom akaamuliwa kuweka chini kinyago..
Dom alikitoa kinyago usoni na kukutanisha uso na fasha.
Fasha ali.....
SASA ENDELEA..
Fasha alishangaa kuona Dom ndo mpinzani wake Lakini hakujali kivile.Kwa ajili ya Rania ndo umeamua kuja kupambana na mimi?..aliuliza Fasha kwa sauti ya chini.
Muda wa mapambano umeshafika mwanamfalme,.. Alisema Dom.
Najua..lakin hukupaswa kuja..Rania yuko salama.. Humiamini?..aliuliza Fasha.
Nakuamini ingawa sio asilimia zote.. Alisema Dom.
Haya ngoja na tuone..alisema mwanamfalme na kuanza mapambano muda huo.
Walipambana kwa muda mrefu kidogo.. Baada ya muda Dom alionekana kuzidiwa..
Watu walianza kushangilia maana walimpenda Fasha.
Kwa dakika chache Dom alikua ameshayasoma madhaifu ya Fasha pamoja na sehemu ambazo alizitumia sana kwenye mapambano.
Walikwenda mzunguko wa pili..mapambano yalikua makali zaid zamu hii.
Baada ya muda kupita Fasha alikua ameshapoteza pambano..Fasha hakuamini kama kapoteza pambano...aligeuka na kumwangalia Dom marambilimbili..hata watu wote waliokua pale hawakuamini pia.
Dom akawa ameshinda mapambano yale na kuacha watu kwenye taharuki.
Fasha, umefanya nini sasa.. Heshima yako itapotea..alisema Mfalme baada ya kusikia Fasha kapoteza.
Baba nisamehe sana..kosa nililofanya ni kujiamini kupita kiasi..alisema Fasha
Nahitaji kumwona alikushinda...huenda atakua wa manufaa sana kwetu kwenye hili swala la NADISH...lisema Mfalme
Baba..ni mapema sana kumshirikisha mtu usiefahamu nia yake ya kuja ikulu kwenye hili swala wakati hata malikia mwenyewe hajui.. Alisema Fasha.
Ila ni kweli..alisema mfalme.
Mfalme..Dom hawezi kushirikiana na wewe kumwangusha Rania... Alijipisemea Fasha kimoyomoyo.
Basi watu wote waliothubutu kuingia mashindanoni waliruhusiwa kujiunga na jeshi la nchi.
Dom alipewa kua kiongozi mmoja wapo kwenye jeshi kama ilivyokua ahadi.
Baada ya kukabidhiwa cheo Dom alianza kuishi ikulu rasmi.
Akiwa anatembeatembea ikulu mara alikutana na Fasha.
Alisimama na kutoa heshima yake kwa mwanamfalme wake..
Dom.. Unazani cheo ulichonacho ni kukubwa sana kunishinda?..alisema Fasha.
Mwanamfalme.. Hata ningepewa cheo kipi bado nisingekua juu yako..alisema Dom.
Sasa kwanini umekuja wakati unajua Rania ninae na yuko salama?..aliuliza Fasha.
Wewe unahofu na mimi na mimi nina hofu na wewe...alisema Dom.
Sasa unazani utafanya nini?..aliuliza Fasha.
Sijajua bado..alisema Dom..
Fasha alimwangaliaaaa...akaondoka
Fasha alikua na wasiwasi muda wote ingawa alivunga kama hana wasiwasi.
Rania akiwa chumbani amekaa kama mwali mara mlango ulifunguliwa na akaingia Fasha.
Mwanamfalme,nitakaa hapa hadi lini mimi?..aliuliza Rania.
Unataka kwenda wapi?... Hujui ni hatari..alisema Fasha.
Hata kama..kama ni wa kufa acha nife maana hata hapa nitagundulika tu siku moja na nitakufa pia..acha niende zangu mtaani..alisema Rania.
Rania kwanini hutaki kukaa na mimi?..kwani nimekufanyia nini kibaya sana?..kwanini lakini Rania?.. Aliuliza Fasha kwa hisia kali..
Mwanamfalme, nisamehe tu...mimi sikuchukii lakini sipendi maisha ya namna hii..tafazali niache tu niende.. Alisema Rania.
Kwa sababu ya Dom ndo unakua hivi?.. Aliuliza Fasha.
Sio tu Dom.. Hanna na na Namadi pia...alisema Rania.
Kwanini lakini Rania... Aliuliza Fasha.
Mwanamfalme.. Wewe ni mtu mzuri sana...unanijali,nashukuru sana lakini sitaweza kuishi hivi.. Nisamehe kwa hilo tu..alisema Rania.
Fasha aliumia sana moyoni mwake..aliamua kutoka ndani ya chumba kile na akafunga mlango..
Akiwa pale mlango moyo ulimuuma sana hadi akajikuta machozi yakimtoka bila kujua..alipiga moyo konde na kwenda kwenye makazi yake.
Rania alibaki peke yake mule chumbani anawaza.
Mwanamfalme.. Nisamehe mwenzio kwa kukosa shukrani..lakini moyo wangu hautulii kwq sababu ya Dom.. Mimi na wewe hatukujaliwa kupendana...nisamehe sana Fasha.. Alijisemea Rania kimoyomoyo baada ya kuoan maumivu ya Fasha.
Hivi hata lini tutahangaika na hii NADISH?.. kwanini asipatikane?. Aliuliza mfalme kwa hasira baada ya kuona mambo hayaendi..
Mfalme, huu sio muda mwafaka wa kukosana..hii kazi ni nzito mno..nipe muda zaidi..alisema mganga.
Kila siku nikuongeze muda?...yaani wewe hufai kabisa..sasa nakupa nafasi ya mwisho ukamilishe hii kazi...alisema Mfalme.
Ndio mkuu..alijibu mganga.
Wakati huo Dom alikua amekaa anawaza yote aliyoambiwa na mama yake mzazi kabla hajaja ikulu..
"Mwanangu, kama kweli umeamua kumsaidia Rania ujue sio kazi nyepesi hata kidogo.. Ni kazi ngumu haina mfano...nitakupa maelekezo yafuatayo.
Pale ikulu kuna dawa iliwekwa ili kwamba Rania akiingia tu Mganga anajua wakati huo huo...hiki ndio kitu cha kwanza unatakiwa kushughulika nacho..bila kulitoa hili tatizo basi Rania atakua na wakati ngumu sana..
Pale ikulu kuna chungu cha shaba ndio kina hiyo dawa..kimewekwa kwenye kona moja wapo kwenye kasri ingawa sijui ni wapi... Unatakiwa ukipate hicho chungu na uvunje kijiti cha mwanzi kilichomo ndani ya chungu kwa kutumia hiki kisu kidogo..hapo kila kitu utakua umemaliza..
Kufanya hivyo kutamwezesha Rania kuishi au kukanyaga ikulu bila madhara""
Haya yote aliyasema Rai mama yake Dom kwa mwanae.
Dom aliwaza sana ni jinsi gani ataweza kufanya hiyo kazi ya kupata ilipo hiyo dawa.
Dom alipanga kufuatilia mienendo ya Mganga na ni kwenye kona gani Mganga hua anakwenda mara kwa mara.
Dom alifanya uchunguzi huo kwa siku siku kumi na kuigundua kona ambayo Mganga anapendelea kwenda mata kwa mara..
Usiku huo Dom alivaa mavazi ya walinzi wa usiku wa ikulu na kuvunga kama mlinzi na yeye.
Usiku wa manane Dom alianza kunyata na kuatafuta kilipo kile chungu...
Alitafuta sana mwisho akafika kilipo chungu ingawa alikua hajajua kama ni hapo..
Muda huo huo mganga alikua anakuja kwa ajili ya kuongeza viungo kwenye dawa yake kuiboresha zaidi ili kumkamata Rania..NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TANO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO