
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Bila shaka unajua Rania anamaanisha nini kwenye ufalme wenu....kwahyo unataka umuue kimyakimya kwa kisingizio kua umemficha umlinde?.. Hautaweza Fasha...alisema Dom huku amemkazia Fasha macho.Fasha alishtuka na macho yalimtoka ...
SASA ENDELEA..
Fasha alibaki macho kodo...Dom...unajua kumbe... Alisema Fasha.
Hakuna kitu kinaweza kua siri milele...alisema Dom.
Fasha alitabasam kidogo ka furaha...
Dom alishangaa kuona Fasha anatabasamu...pengine alizania kua labda mwanamfalme ametabasamu kinafiki tu kuna mpango mbaya anataka kuufanya...
Ulijuaje?..aliuliza Fasha.
Unataka nikwambie alieniambia ili nae ummalize?..aliuliza Dom.
Mhh...ila ni halali uhisi hivyo..sikulaumu..ila siku mpja utakuja kujua nia yangu ya kweli alisema Fasha.
Mimi naondoka..ila nakupa taarifa tu kua kaa mbali na Rania.. Hutompata kamwe..alisema Fasha.
Rania yeye hajasema nikae mbali na yeye..au nakosea?..alisema Dom.
Fasha ilimchoma maana ni kweli kichwani kwa Rania amejaa Dom.
Nitamfanya aseme siku moja..alisema Fasha.
Itakua rahisi unazani?. Aliuliza Dom.
Usiwe na hakika sana na Rania, kumbuka kwa sasa naishi nae mimi... Alisema Fasha.
Vyovyote vile.. Ila naomba tafazali mtunze Rania salama..sijui unawaza nini ila nahisi hautakua mtu mbaya kwake ingawa sikuamini asilimia zote... Alisema Dom.
Fasha alimsikiliza Dom kisha akaondoka bila kujibu.
Dom akiwa nyumbani alikua hatulii kama kuku anaetafuta kutaga kila alipokumbuka maneno ya Fasha.
""...ila nakupa taarifa tu kua kaa mbali na Rania.. Hitompata kamwe..""
""Usiwe na hakika sana na Rania, kumbuka kwa sasa naishi nae mimi... Alisema Fasha""
"Nitamfanya aseme siku moja""
Kauli hizi tatu zilimkosesha Dom amani..aliwaza huenda aliyosema Fasha ni kweli lakini alijipa moyo kua huenda Rania anampenda yeye.
Huku Fasha nae alikua akiwaza..alikumbuka jinsi ambavyo Rania anahitaji kumwona Dom kila saa wakati yeye yupo..aliumia ila alipanga kumfanya Rania ampende yeye.
Mama...mwanao nimekua sasa..hata hii pete uliyoninunulia hainitoshi kwa sasa.. Natamani ningewahi hata kukufahamu mama yangu.. Alijisemea Rania akiwa peke yake chumbani huku akiangalia pete ile ambayo muda huo ilikua haimtoshi.
Akiwa anaiangalia pete hiyo alikumbuka miaka mingi iliyopita alipokua anataka kuporwa hiyo pete na vibaka Dom alikuja kumsaidia...alikumbuka jinsi Dom alivyojigamba
"hata simba napiga mimi"
Rania aliishia kutabasamu tu akikumbuka enzi zile kabla ya vita.
Akiwa anawaza mara ghafla mlango ulifunguliwa..Rania hakuamini macho yake kumwona Hanna na Namadi mbele yake.
Aliamka na kwenda kuwakumbatia kwa hamu na furaha kubwa..
Namadi na Hanna hawakuamini kumwona Rania mbele yao..kwanza wao walizani wanaletwa kwenye kifo.
Rania kumbe uko huku!!?..aliuliza hanna.
Hamna siko huku niko kule.. alisema Rania na wote wakacheka.
Enhee nani amewaleta?. Aliuliza Rania.
Mmnh yaliyotukuta hata siamini kama tuko hai..alisema Hanna.
Nini tena?..aliuliza Rania kwa wasiwasi.
Tulikua tumekaa mara tukavamiwa,tukakamatwa na kufungwa vitambaa vyeusi machoni na kuambiwa tusipige kelele la sivyo tutakufa..tukapandishwa juu ya farasi na tukaletwa huku..hapo mimi nilikua najua tunaenda kufa...tumefika hapa mlangoni ndo tukafunguliwa macho na ndo kukutana na wewe hivi..alisema Hanna.
Haaa...jamani..si angewachukua kistaarabu?..alisema Rania.
Ni nani kwani?..aliulza Hanna.
Aah..hebu tutaache hayo..nipatieni habari za mtaani...alisema Rania.
Mmh..huko hakuna jipya..alisema Hanna.
Dom aliwahi kuja?..aliuliza Rania kwa unyonge.
Hua anakuja..vipi umeshamkumbuka?...alisema Hanna huku akimwangalia Rania kwa jicho la wizi wizi.
Aaah.. Yaani wewe nae..alisema Rania huku ameangalia chini.
Waliongea sana tu hadi asubuhi ikakaribia..Namadi yeye alikua anaongea kwa kulenga na manati kama kawaida yake.
Baada ya muda alikuja mtu alieagizwa na Fasha kuwachukua na kuwafunga vitambaa kama mwanzo kisha walirudishwa kwao bila kuona njia ya kuja pale mafichoni
Kabla hawajaondoka Rania aliwakabidhi kibox fulani hivi na kuwaagiza wakipeleke kwa Dom.
Huku Mfalme aliwaita watu wake wa karibu waliokua wakilifahamu swala la NADISH ili kujadili zaidi.
Alimwita Mganga,mlinzi mkuu (omandi) na mwanamfalme Fasha..hakumwita malikia suya maana alizani malikia hajui.
Sasa hapa nimewaiteni tujadili hili swala..tena wewe Fasha ndo mhanga mkubwa.alisema Mfalme.
Fasha nazani uliwahi kusema kua yule binti amekufa.. Sasa mbona anaoneka tena?. Aliuliza Mfalme.
Kiukweli hapo hata mimi sielewi maana nilifanya uchunguzi kwa kina nikagundua alikufa...lakini sasa amerudi..ajabu kweli hii..alisema Fasha.
Mtukufu Mfalme, mimi naona kwa sababu NADISH imeoneka kurudi hatuna haja ya kujadili ya nyuma..sasa tuone tutafanya nini..kwanza inabidi tuliongeze jeshi letu nguvu.. Alisema omandi.
Kweli kabisa Mfalme.. Alikazia mganga.
Tunafanya nini sasa kuliongeza jeshi nguvu?...aliuliza Mfalme.
Tukusanye vijana washindane kwenye upiganaji na watakao shida watakua wanajeshi wa nchi..alisema Mganga.
Halafu tutoe tangazo kua atakaepigana na mwanamfalme na kumshinda atapata cheo kizuri hapa hapa ikulu..hapo vijana watajituma na watakua wenye nguvu alisema omandi.
Unasemaje Fasha kihusu hili?.. Aliuliza Mfalme.
Haina shida ni wazo zuri..alisema Fasha.
Mmejadili nini?.? Aliuliza malikia suya baada ya Mganga kurudi.
Mganga alimweleza yote Malikia suya.
Sawa.. Nitajua la kufanya...kwanza nimeshapata wazo jipya...alisema Malikia suya.
Kesho yake asubuhi na mapema askari wa ikulu walikwenda kutangaza tangazo hilo.
Namadi na Hanna walilisikia tangazo hilo.
Enheee..hapa na mimi naenda kweye mashindano.. Nikaishi ikulu tena kama nilivyokua Lazi....alisema Namadi.
Nini wewe?. Uende wapi?. Aliuliza Hanna kwa mshtuko.
Ikulu, kwani hujasikia tangazo?.. Aliuliza Namadi.
Nani umwache peke yake wewe?.. Thubutu..huende popote..alisema Hanna.
Weee...kwani mimi mmeo hadi unikatalie?...alisema Namadi.
Ona huyu nae....Unauwezo wewe wa kua mme Wangu?..alisema Hanna kwa jeuri.
Sasa mbona unanikatalia?. Alisema Namadi.
Kwavile tu naogopa kukaa mwenyewe.. AngekuwepoRania hata usingenisikia nasema hivi.. Ila wewe kama unaenda nenda tu.. Alisema Hanna huku amenuna na kuamua kwenda zake.
Hanna...aliita Namadi huku akijaribu kumrudisha Hanna.
Hanna aliendelea tu kwenda.
Siendi bwana we nae...alisema Namadi.
Hanna alitabasam na kusimama
Namadi alimwendea karibu.. Haya umefurahi sasa..alisema Namadi.
Hanna alitabasam tu.
Wakiwa hapo mara walimwona Dom..walimwita na akaja.
Dom.. Huu hapa mzigo wako kutoka kwa Rania.. Alisema Hanna huku akimkabidhi kibox fulani hivi
Dom alienda pembeni na kuanza kufunua kwa hamu kilichomo..
Alikuta ni ile pete ambayo ilimkutanisha na Rania siku ya kwanza... Dom alitabasamu kwa furaha.
Alifungua kikaratasi kile ambacho kiliandikwa
" nimekukumbuka sana Dom, itunze pete yangu hiyo.. Nilipewa na mama yangu kwa sasa hata hainitoshi"
Dom alifurahi sana kuoa kua Rania anamkumbuka na kumthamini...alifurahi mno.
"Nimekukumbuka pia Rania,pete yako nitaitunza"
Alijisemea Dom kama kwamba Rania anasikia.
Akiwa kwenye furaha mara alikumbuka kua amesikia tangazo la mashindano ya ngumi.
Alikaa pembeni na kuanza kutafakari na mwishoe alimua kujiunga.
Lazima nijiunge,lazima nishinde na niingiie ikulu ikiwezekana nipambane na Fasha nipate uongozi..hii itakua rahisi zaidi kumsaidia Rania.. Allijisemea Dom na bila kuchelewa alikwenda nyumbani kwao kumtaarifu mama yake kuhusu maamuzi yake.
Dom mwanangu..uende ikulu?. Unataka nikupoteze?..alisema Rai mama yake Dom.
Mama... Nahitaji kumsaidia Rania ikiwezekana atoke huko mafichoni akaishi sehemu nyingine ambako atakua na amani.
Ni kweli nina kazi ya kumlinda huyu mtoto lakini sio kwa kumtoa sadaka mwanangu.. Alijisemea Mama yake Dom kimoyomoyo
Mama unawaza nini?.. Aliuliza Dom Baada ya kuona mama yake kakaa kimya muda mrefu.
Mwanangu... Hautaweza kupambana na ufalme hata kama utapata cheo..tafazali nakuomba.. Alisema Mama yake Dom.
Mama...nahitaji kumlinda Rania.. Niruhusu tafazali mama yangu.. Alisema Dom.
Mwanangu,kwa jinsi asili ya Rania ilivyo huwezi kumlinda..vita yake ni kubwa kuliko wewe..alisema Rai.
Mama tafazali nakuomba...sitakurupuka..nitahakikisha najipanga...hiyo vita ya Rania basi mimi nitakua nae...hana mtu upande wake..alisema Dom.
Mama yake Dom alitafakari kwa muda kisha akasema.
Sawa mwanangu.. Nakutakia ushindi na maisha mema kama ukifaulu...jichunge sana mwanangu usije ukapata madhara..kumbuka nina mtoto mmoja tu ambae ni wewe..alisema Rai.
Asante mama yangu.. Naahidi nitakua makini sana.. Alisema Dom akimkumbatia mama yake.
****
Baada ya hapo Dom alikwenda kupiga mazoezi nkwa nguvu sana na juhudi...alikua akizingatia sana mafundisho ya mwalimu wwk
Siku ya mashindano iliwadia...watu walijipanga sawa sawa kwa ajili ya mashindano.Dom nae alipata kibali.
Ndani ya siku saba hatua zote za chini za mashindano zilikua tayari zimekamilika na mtu alietakiwa kupambana na mwanamfalme alikua ameshapatikana.
Mtu huyo alipewa siku tano zaza kujiandaa kwa ajili ya fainali.
Fasha alikua mpiganaji mashuhuri sana aliefahamika na watu wote hasa baada ya kuiongoza nchi kupata ushindi vitani miaka mingi iliyopita..kiufupi alikua shujaa wa nchi.
Mpinzani wake sasa (Dom) yeye hata hajawahi kupata tuzo kwenye mapambano ya vibaka😸.
Dom alikua hapumziki..alipiga mazoezi mchana kutwa usiku kucha kwa ajili ya mashindano.
Hata Dom nae hakua vibaya sana maana aliweza kuepuka kifo bila kutoroka nchi yeye na mama yake😛
Mwanamfalme yeye hata hakua na hofu.. Alijua kushinda ni lazima maana hao vijana wote wanauwezo mdogo sana na hawajawahi kuingia vitani.
Hata hivyo hakuwahi kumjua mpinzani wake kwenye mapambano maana alikua hahudhurii kwakua aliamini atashinda tu kwakua hakuna anaemzidi uwezo.
Hatimaye siku ya mapambano ilifika..mpambanaji alikuja na kinyago uwanjani..mwanamfalme nae alikua amejiandaa sawa sawa.
Muda wa pambano ukafika na Dom akaamuliwa kuweka chini kinyago..
Dom alikitoa kinyago usoni na kukutanisha uso na fasha.
Fasha ali.....
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA NNE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO