
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Namadi tatizo nini? Aliuliza Rania kwa pupa...Namadi alieleza kila kitu hadi mwisho kisha akanyamaza.
Nini?.. Alisema Rania macho amemtoka..
Fasha nae alishtuka sana..
SASA ENDELEA..
Nani ametoa hii amri?.. Ni mfalme au..alijiuliza Fasha.Haya unaweza kwenda sasa...alisema Fasha akimwambia Namadi.
Mwanamfalme, bila shaka hii ni kazi ya baba yako...alisema Rania.
Hivi Mfalme anaweza kutoa amri ya namna hii kweli!!..alisema Fasha.
Huenda na mimi ni wa huo ukoo unaowindwa...watanutafuta muda sio mrefu... Alisema Rania.
Wewe sio wa huo ukoo...la sivyo siku ya kwanza tu kukanyaga ikulu ungeshakufa tayari...Alisema Fasha.
Na hiyo dawa ipo?..aliuliza Rania kwa mshtuko.
Ndio ipo...alisema Fasha.
Mungu wangu.. Mimi kukosekana ndo kunafanya watu wasio na hatia kufa!!!...alisema Rania.
Usiseme hivyo Rania..alisema Fasha.
Wakati Namadi anaondoka alikutana na Dom..
Namadi...mbona uko hapa?..aliuliza Dom.
Namadi alimsimulia yote..
Haaaa.....alishtuka Dom.
Bila kuchelewa alikwenda walikokua Fasha na Rania.
Dom...umeshasikia kilichotokea?..aliuliza Rania..
Nimeshazipata habari kutoka kwa Namadi....alisema Dom.
Sasa tunafanya nini...alisema Rania..
Wote walikaa kimya wakifikiria ni nini wafanye.
Rania aliwaza moyoni mwake kua ajipeleke kwa Mfalme wakamuue yeye lakini alijua wenzie hawatakubali hata kidogo.. Vilevile alijua Mfalme hataamini kama ni yeye maana tayari dawa ile ya kumtambua ilishavunjwa.
Mimi ngoja kwanza niende nyumbani kwa Namadi na hanna..alisema Rania
Ukafanye nini?..aliuliza Fasha.
Hapa ikulu sio salama kwangu kwa sasa..alisema Rania
Sasa si ungerudi mafichoni?.. Alisema Fasha.
Hamna haja ya kujificha wakati kwanza mimi sio wa ukoo wa mfalme kelkuni...nani atanifuata?..aliuliza Rania.
Fasha alibakia kimya..hakutaka kabisa Rania aondoke ila aliona kiukweli hakuna hoja angeitoa kumbakisha Rania ikulu.
Basi mimi nitakupeleka..alisema Dom.
Fasha alimkata jicho moja la kichawi Dom kisha akasema.
Nitampeleka mimi... We baki uendelee na kazi zako.
Siendi na mtu yeyote... Tukionekana tunaweza kushtukiwa...alisema Rania.
Mimi nitakupeleka...alisisitiza Fasha.
Hapana mwanamfalme... Nitaenda peke yangu... Alisema Rania.
Hujui kumwongoza Farasi..utaendaje?...aliuliza Fasha.
Kwaheri mwanamfalme, kwaheri Dom tutaonana siku nyingine..alisema Rania na kuanza kuondoka..
Rania... Aliita Fasha..
Kabla Rania hajajibu alikuja mtumishi mmoja wa ikulu.
Mwanamfalme, mfalme anakuhitaji.... alisema mtumishi yule..
Fasha ilibidi aitikie wito na kuondoka kwenda kwa Mfalme.
Dom alibaki pale peke yake.
Rania alitembea kwa kasi sana ili awahi..
Nyumbani kwao palikua mbali sana ingawa palifikika hata kwa kutembea tu kwa watoto wasio wa kishua.
Rania alitembea hadi akaingia mstuni...msituni kulikua na vinjia vingi ambavyo hata havieleweki vinaishia wapi.. Kwa mtu ambae hakua mzoefu wa huo msitu ni rahisi Sana kupotea.
Ilifikia wakati Rania akapoteza uelekeo..yaani alishindwa aelekee wapi maana hakua mzoefu kwenye msitu huo.
Ee Mungu wangu.. Maskini jeuri mimi leo nitakoma.
Nimejidai kukataa msaada ona sasa nimepotea..leo mimi ni supu ya simba aki ya nani...alijisemea Rania baada ya kukosa njia.
Baada ya kutanga tanga sana aliamua kukaa..
Sijui nirudi ikulu.. Si aibu hii jamani.. Ujuaji mwingine sio mzuri kabisa..
Akiwa amejiinamia mara aliona miguu ya farasi mbele yake.
Rania aliinua kichwa kuona ni nani huyo..
Alipoinua kichwa alikutanisha macho na Dom..
Dom.....umekuja..unajua nilikua napunga upepo hapa niendelee na safari..usizani kua nilikua nimepotea..alisema Rania
Kwani nani kasema ulikua umepotea..au unajishtaki.. Alisema Dom
Aaaah...hamna bwana.. Alisema Rania kujitoa kwenye aibu.😊
Haya kuja hapa haraka... Alisema Dom
Rania hakua na jinsi..ilibidi tu akubali kukaa kwenye farasi...
Fasha.. Siku hizi sikuoni ikulu mara kwa mara..hua unakua wapi?.. Aliuliza Mfalme.
Aaah...hua napunga upepo tu huko nje. Alisema Fasha
Wewe badala ya kushughulikia hili swala unakalia kupunga upepo!!!.. Alisema Mfalme
Fasha alikaa kimya..
Baba...sasa tunachukua hatua gani kuhusu hili tatizo maana naona mganga ameshindwa..aliuliza Fasha ili apate kujua kama mfalme anahusika kwenye hayo mauaji
Mwanangu, mwanzo nilihofia kukushirikisha lakini unatakiwa ujue ..alisema mfalme.
Nini?...aliuliza Fasha.
Ni kwamba,nimetuma watu wawauwe wazawa wote wa kelkuni... Alisema Mfalme.
Baba!!!!!...alisema Fasha kwa mshtuko
Sasa unazani nitafanya nini?.. Aliuliza Mfalme
Baba,ukae ukijua kua unafanya kazi bure... NADISHI sio damu ya kelkuni maana ingekua hivyo angekufa siku anaingua hapa...sasa ukiwaua hao utakua umefanya nini?..aliuliza Fasha
Hata mimi nalijua hilo...tukiwaua wote atakosekana wa kua mfalme hivyo hiyo binti atakosa nguvu na Vilevile haitawezekana yeye kutawala kwakua sio wa kiume..alisema mfalme.
Sasa unahakika utawamaliza wote?. Aliuliza Fasha
Ndio nina hakika halafu sitaki maswali zaidi...alisema mfalme kisha akasimama na kuondoka maana aliona Fasha analetea mauzauza tu.
Fasha aliishiwa nguvu kujua kua mfalme ndo ametoa hiyo amri... Alichoka hasa.
Dom alimpeleka Rania hadi alipokua anaishi na akina Namadi..
Kwa bahati nzuri kipindi wanafika tu na Namadi ndo alitaka kuondoka kwenda kwa hanna..hivyo walimuwahi
Rania.. Mfike salama huko mnakoenda..alisema Dom
Haya na wewe safari njema.. Nakuombea usikamatwe kama ulikua umetoroka ikulu. Alisema Rania.
Dom aliondoka.. Rania na Namadi waliondoka hadi alikokua hanna..
Kwakua palikua mbali,walitembea muda mrefu na walifika usiku...
Hanna....aliita Rania kwa pupa kwa kua alikua na hamu sana ya kumwona.
Cha ajabu hanna hakuitika..
Yuko wapi hanna?.. Aliuliza Rania..
Nilimwacha usiku..Alisema Namadi.
Waliita hadi wakachoka lakini hanna hakuitika..
Walijua labda anawachezea kamchezo tu..
Wakiwa bado wanashangaa mara walijikuta wamewekwa kati na watu waliovalia vinyago...NINI KINAFUATA?..
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA SABA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO