
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Yuko wapi hanna?.. Aliuliza Rania..Nilimwacha usiku..Alisema Namadi.
Waliita hadi wakachoka lakini hanna hakuitika..
Walijua labda anawachezea kamchezo tu..
Wakiwa bado wanashangaa mara walijikuta wamewekwa kati na watu waliovalia vinyago...
SASA ENDELEA..
Rania alishtuka sana..kwenye habari za kupigana alikua sifuri kwa kwakweli.Namadi aliwahesabu wote na akacheka kidogo..
Namadi tunafanya nini sasa?..aliuliza Rania kwa woga..kwenye kufa hakuna ujasiri..😸
Namadi hakujibu chochote.. Aliwatembezea kichapo cha adabu...Namadi alikua mmoja wa wapiganaji walioaminiwa na mfalme wa lazi na ni mmoja wa mashujaa wa hiyo nchi..kwahiyo vibaka wadogowadogo kama hawa hawakumpa shida.. Aliwacharaza kama vile hawana mikono👊💪
Rania sasa..ni mwendo wa kujibana ukutani tu kama anampango wa kuingia kwenye ukuta.
Namadi aliwapiga sana...walikimbia kwa kasi ya ajabu ila mmoja wao alikamatwa na Namadi.
Binti mliemkuta humu ameenda wapi?...Namadi alimuuliza mtu yule.
Hatujamuona...na sisi tulikua tunamtafuta..alisema mtu yule.
Unanitania?..sasa ngoja..alisema Namadi huku akijipanga kumdunda tena.
Namadi... Aliita Hanna..
Namadi aliahirisha kutoa kichapo na kugeuka..
Hanna... Uko salama?.. Aliuliza Namadi kwa hofu.
Niko salama...walikua hawajanipata..alisema hanna.
Walifurahi sana....Rania aliwahi na kumkumbatia Hanna.
Namadi alimkamata yule mtu akamfunga mikono na miguu kwa maswali zaidi.
Enhee kwanini mnawaua hawa watu?.. Aliuliza Namadi.
Sijui..alijibu mtu yule.
Namadi alimtembezea kipigo cha nguvu..ilibidi tu anyooke aseme.
Kwanini mnafanya hivi?.? Aliuliza tena Namadi.
Ni wazawa wa mfalme aliepinduliwa...lazima wafe wote..alisema mtu yule.
Hata kama wakimwondoa yule sijui ndo NADISH sijui NASHIDI..aliuliza Rania.
Haaa...kumbe wewe unajua!!..ndo hivyo.. Watauawa tu hata kama NADISH akifa leo..maana wakiachwa wanaweza kuleta uasi baade..alisema mtu yule...
Nani kawatuma?..aliuliza Rania.
Sijui bwana..mna maswali mno..alisema mtu yule.
Ni akina nani hao wanaoshugulika na hili swala...aliuliza Namadi.
Kabla yule mtu hajaongea ghafla alipigwa mishale mingi tu na wale wenzie ili asiendelee kusema.
Namadi na Rania walishtuka na walipogeuka hawakuwaona wale watu tena...
Yule mtu haikuchukua muda mrefu akafa..
Sasa tunafanya nini?..aliuliza Namadi lakini Rania alikua kimya...
Rania... Aliita Namadi lakini Rania alikua kimya tu...Namadi aligeuka na kumwangalia Rania.Rania alikua amekunja sura sura,anahema kwa hasira na mawazo yakiwa mbali sana.
Rania alikua mtu mwingine kabisa muda huo.. Si Rania wa masihara tena.. Alijua hata akisema ajitoe sadaka hamna litakalo badilika..hivyo ni kupambana nao tu hamna jinsi.
Rania... Aliita Namadi huku akimwangalia Rania usoni....
Rania hakujibu.. Aliamka na kuanza kuondoka.
Alitoka na kwenda chumba cha pili akajifungia huko.
Namadi na hanna walikwenda kumstili yule maiti kwa siri na kurudi nyumbani.
Walikuta Rania amejifungia ndani mwenyewe.. Waliiita wee lakini hakuitika wala kufungua.. Muda wote alikua kimya.
Usiku uliingia Rania akiwa bado amejifungia ndani.
Hivi Rania anatatizo gani jamani?..kwanini amekua vile ghafla?.. Aliuliza Hanna.
Na mimi nashangaa kama unavyoshangaa wewe..alisema Namadi.
Ngoja niende nikamwite aje ale maana tangu mchana hajala eti.. Alisema hanna.
Rania... Rania... Aliita hanna Lakini Rania hakuitika wala hakufungua mlango.
Raniaaaa....njoo ule...mbona unakua hivyo... Alilalamika hanna Lakini Rania hakuthubutu kuitika wala kufungua mlango...
Dom alifanikisha kurudi ikulu salama...lakini hata hivyo Fasha alijua kua Dom alitoroka.
Akiwa anaangalia huku na kule mara alisikia sauti..
Unajua ni kosa kubwa kiasi ulilofanya?...
Dom aligeuka na kukuta ni mwanamfalme anaemsemesha.
Dom alikaa kimya tu hakujibu..
Unajua kua linaweza kukukosesha kazi?..aliuliza Fasha.
Haina shida maana na wewe unajua hapa kilichonileta ni nini..sasa ninafaida gani kumwacha akapotelea msituni wakati hapa nilikuja kwa ajili yake?..alisema Dom.
Dom..unaongea na mwanamfalme hapa..unathubutuje kunijibu kirahisi rahisi hivyo?... Alisema Fasha
Sijui namna nyingne ya kukujibu tofauti na hivyo Mwanamfalme.. Alisema Dom.
Hauhofii kupoteza kazi yako Dom?... Aliuliza Fasha.
Rania akiwa hayupo hapa wala sihofii kupoteza kazi..alisema Dom.
Kwani wewe huoni ni muhimu kuwa hapa hata kama Rania hayupo?.....aliuliza Fasha.
Ni muhimu sana kuwepo..lakini kama Rania yuko hatarini ninamaana gani ya kukaa hapa nikamwacha adhurike...alisema Dom.
Sawa... Ila jua kwamba sio wote wanafahamu kilichokuleta...siku mwingine akikuona tofauti na mimi itakua balaa kwako...alisema Dom.
Nashukuru sana mwanamfalme kwa moyo wako wa kujali..alisema Dom.
Fasha aliondoka zake kuelekea anapoishi..
Zilipita siku mbili Rania hali wala hajafungua mlango....
Mimi nabomoa mlango. ..alisema Namadi.
Weee..ubomoe nyumba ya ya kupewa!!..au umesahau kama hapa sio kwetu?. Alisema hanna.
Mimi sijali hilo...nitalipa..nabomoa tu.. Sasa tutamwacha Rania afe kisa nyumbaa sio yetu?.. Aliuliza Namadi.
Ila kweli...bomoa tu tutalipa..alisema hanna
Mlango ule ulikua umechoka hasa...Namadi wala hakuhangaika kuubomoa..kidogo tu ulikua umeshaanguka..
Walipoingia walishangaa Rania hakuwepo..
Haaa..kaenda wapi huyu.. Au atakua alipita dirishani?..aliuliza Namadi.
Itakua. Tumfuate nyuma.. Alisema hanna.
We baki na huyu mtoto hapa mimi nitamfuata..alisema namadi.
Sawa... Alisema hanna.
Lau.. Usilie mtoto mzuri sawa ee.. Alisema hanna akiwa na yule mtoto baada Namadi kuondoka..
Sawa dada..alikubali Lau.
Rania alimlaza mtoto yule kifuani kwake..alimwonea sana huruma.
Huku Namadi alikimbia kwa kasi kubwa...alipita kile kijiji hadi akafika kule ambako walikua wakiishi zamani lakini hakumwona Rania.aliendelea kutembea hadi akafika kwenye msitu ule ambao Rania alipotea siku ile..
Alitembea kwa kasi huku akiangaza huku na kule... Kwa mbali alimwona Rania amekaa chini ya mti akila matunda maana alikua na njaa ya ajabu.
Alimkaribia na kumwita..Rania!!..
Rania wala hakugeuka .aliendelea kula matunda huku amekasirika kama mwanzo.
Rania huijui njia...kama unaelekea ikulu nitakupeleka..alisema Namadi huku akikaa pembeni ya Rania ambae alikua haongei hata kidogo.baada ya muda Namadi alimwongoza Rania njia wakaenda ikulu.
Rania alielekea hadi kule wanakoishi watumishi wa kasri.. Alikuta sare zao zimeanikwa kambani...aliiba zinazomtosha kakavaa na akaendelea na safari.
Muda huo Namadi alikua amekaa nje kabisa ya ikulu akimsubiri Rania kama ikitokea akarudi..
Rania alinyoosha moja kwa moja hadi anakoishi Dom huku akiwa amevaa mavazi ya watumishi wa ikulu asije akashitukiwa.
Alifika hadi nyumba chenyewe anachoishi Dom na kubisha hodi kama vile kuna kazi amekuja kufanya kama mtumishi wa kasri.
Dom alifungua mlango akizani ni mtumishi.
Alipoangalia vizuri alishangaa kuona Rania yuko mbele yake!!!!..NINI KINAFUATA?...
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA NANE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO